Mtenda Akijitenda...!

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Siku moja mume aliwasili nyumbani akiwa na habari ya kusikitisha kwa mke wake ...!

Mume: Mke wangu, nimepokea simu, kuwa mama amefariki dunia. Tafadhali jitayarishe ili tupitie na sokoni ili kununua mahitaji kwa ajili ya mazishi. Tafadhali andika orodha ya vitu na kisha tunaweza kwenda.

Mke: Orodha si muhimu sana, tutaweza kununua tu, kilo tano za Maharage na Unga wa mahindi kilo tatu na nazi mbili za kupikia.

Mume: Eeh! Hivyo vitu kweli vitatosha!?

Mke:
Vitatosha tu mume wangu, hakuna haja ya kupoteza fedha, bila shaka vitatosha tu, wala usiwe na wasiwasi.

(Wakaondoka na kupitia sokoni na kununua Maharage Kg 5, Unga wa mahindi Kg 3 na nazi 2 za kupikia. Mume akauliza tena kama vile vitu vitatosha, mke wake akasisitiza kuwa hakuna sababu ya kupoteza fedha kwenye mazishi. Safari ya kuelekea msibani ikaanza.... Lakini badala ya kuelekea kijijini kwa mama yake mzazi mume, wakawa wanaelekea njia ya kwa mama wa mkewe...!)

Mke: Mume wangu, umepotea njia, uku tunapokwenda si kijijini kwa mama yako mzazi aliyefariki, ni kijijini kwa mama yangu...!

Mume: Hapana sijakosea njia, aliyefariki ni mama yetu, ambaye ni mama yako mzazi.

Mke (akiwa amepigwa na pumbao na kilio cha kwikwi): Lakini mume wangu, chakula tulichonunua, hakiwezi kutosha, bora turudi tukanunue vitu zaidi!

Mume: Hapana! Mimi nilikuuliza zaidi ya mara tatu kama vitu vitatosha, ukasema "Ndio" na hakuna haja ya kupoteza pesa! so we are not going back!

Uchoyo ni adui wa Nafsi... Tuwapende Wazazi wa wenzetu kama vile tunavyo wapenda wazazi wetu!
 
Hizi jamii zetu zina mambo kweli kweli. Mioyo na kuta zingekuwa zinaonge, na yaliyopo moyoni yangekuwa yanaandikwa usoni, tungekimbiana haswaa!
 
Haya mambo yapo kabisa,kuna watu ni wachoyo na roho mbaya sana,sasa huyo mwanamke,roho yake mbaya ilikula kwake.somo hilo.
 
Uchoyo sio ishu....ila kuna watu wasio na shukurani.

uchoyo ni nyeti kulichambua kwa sabau hata asiyetoa shukrani naye ni mchoyo tu............................wa kutambua mema aliyotendewa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom