Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Maneno ya kweli na mifano halisi likini katika matumizi mabaya.

Hatulazimishwi demokrasia tunatakiwa kuiheshimu demokrasia.

Kwa kushindwa kufuata na kuenda haki tutalia na kusaga meno.

Amerika ina haki ya kufanya hivyo. Tunawajibu wa kuilaumu CCM. Fikiria walivyokomalia umeya wa Dar, walivyokanyaga haki nyingi za binadamu. JPM analofanya hakuna bila haki, ni ubatili mtupu

Na Tanzania ina haki ya kuwa na msimamo huru usioyumbishwa na matakwa ya mabeberu wa nje! Eti Demokrasia! Mbona Misri inatawaliwa kijeshi na kwa mkono wa chuma na bado Marekani inawakumbatia? Nani asiyeyafahamu mauaji ya kimbari wanayofanyiwa Wapelestina na Mayahudi, lakini Marekani inauchuna tu kwa vile ina maslahi yao. Tanzania ikaze buti na kuachana na MCC 2 inayolenga kuwanufaisha mabepari wa Marekani Zaidi kuliko sisi. Na ma opportunist wa bongo wakome kushadidia ugandamizaji huo kwani hautaganga njaa zao.
 
Katika vitu ninavovipinga na kuvichukia ni misaada na mikopo

Kama wanatupenda kweli, watupe msaada au mkopo wa kujenga viwanda, Barabara na issue nyingine tutajenga wenyewe baada ya kuwauzia bidhaa badala ya malighafi

Wanakupa msaada/mkopo wakujenga barabara ila tenda lazima iende kwenye kampuni yao, na gharama za kijinga jinga kbs!

Ni wakati wakuanza kujitegemea ss, tufanye kazi tuache majungu
 
Tumefika mahali tulipo kwasababu ya watu kama akina Pole Pole. wamefungwa ufahamu, wanafikiria mambo kwenye narrow angel kisha wanatumia our weakest political system to lure our people. Utashangaa kuna watu humu ndani watamsifu Pole pole, kwa kukurupuka bila kufanya a critical analysis ya huu upupu wake.

Unakosea halafu unaanza kufit uongo na reasoning za kitoto to justify the lost game, only resulting from greedy and arrongance iliyochanganyika na chronic ego. That is not patriotism.

Wastage of our time. We need more of brain power in this country, not these cheap politics.

Ungeeleweka kama ungemjibu Bw. Polepole kwa hoja yakini kwa kila nukta aliyoijadili badala ya kulalama tu.
 
Kama ni mke walishachukua zamni. Urani yote ya nchi hii wameimiliki. Kuanzia Baahi hadi Namtumbo, hadi Mbinga hadi Mbambabay nk. Halafu leo unadaai unalinda mke? W vipi?
 
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.


“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

..tendo hili la Jecha kupora uchaguzi wa Zanzibar halina tofauti na kitendo cha Ian Smith kutangaza uhuru wa walowezi wachache, maarufu UDI, kule Rhodesia.

..yaani kilichotokea ni kubadilishana nafasi kati ya Tz na nchi za magharibi ikiwemo Marekani.

..Dr.Shein amekuwa ni sawa na Ian Smith. Kupora uchaguzi imekuwa sawa na uamuzi wa UDI. Zanzibar imekuwa sawa na Rhodesia. CCM imekuwa sawa na walowezi wa Rhodesia. Tanzania imekuwa sawa na Uingereza iliyo-support uharamia wa kina Ian Smith.

..sasa Marekani imekuwa sawa na Tanzani ya wakati ile--ya Nyerere. Marekani imesimama upande wa haki kupinga kufutwa kwa uchaguzi uliokuwa huru na haki.

..kuna mambo ya kutetea huko ccm lakini siyo hili la Zanzibar.
 
Eewa mantiki ya argument, si kwamba we have nothing to lose we will lose obviously.
Lakini mtu akitaka kukuchukulia mkeo kwa vile anakufadhili, siiku nyingine hata heshima ya kutetea utu wako unakuwa huna!!
.
Ati?
Zanzibar ni mke wa Tanganyika aliyetakakuchukuliwa na nani?
Hawakuhamua wazanzibar wenyewe Nov25 juu ya rais waliemtaka?
Huu ukurunzinza utatugharimu sana Isee
 
MTIZAMO WANGU KUHUSU BODI YA MCC KUSITISHA

MSAADA WA MCC 2 KWA SERIKALI YA TANZANIA


C:\Users\toshiba\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif


Na Alexander Mhando

Utangulizi;

Tukianza na nukuu ya Baba wa Taifa alisema “…….Inapotokea taifa kuuza uhuru wake kwa ajili ya misaada ya kiuchumi au kukubali kukaliwa na majeshi ya nje, taifa hilo linakuwa limepotea na litanyonywa na watu wake watakuwa wanakandimizwa popote pale……” alisema Mwalimu.

Katika swala la msaada wa pesa za Millenium Challenge Corporation’s (MCC) ambazo huwa tunapewa nchi zinazoendelea kama msaada kwa ajili ya Maswala ya maendeleo kwa Nchi zetu, Pesa hizi hutolewa na Bodi ya Shirika la changamoto za Milenium (MCC) ambayo inamilikiwa na serikali ya marekani ili kusaidia nchi zinazoendelea.

Katika kikao cha Bodi ya MCC kilichokaliwa jana tar 28/3/2016 kimefikia uamuzi wa kutishia kusitisha pesa za msaada za MCC kwa Tanzania kwa sababu walizozitoa wao ambazo ni swala la uchaguzi wa Zanzibar na swala la sheria za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii katika uchaguzi wa Zanzibar na wa mwaka jana.

Tukikumbuka Katika kikao cha tar 16 December mwaka jana cha Bodi ya MCC, Bodi ya MCC katika kikao chake ilijadili pendekekezo la mkataba mpya na serikali ya Tanzania wenye thamani za Dola za Kimarekani Millioni 472.8 na kuamua pesa hizo zitolewe baada ya Tanzania kutimiza kigezo cha kuzuia Rushwa. Msaada huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuimarisha secta ya umeme nchini, likiwa lengo ni kuwawezesha watanzania wengi zaidi kupata nishati hiyo kwa uhakika na kwa bei nafuu. Lakini pia kuimarisha taasisi zinazohusika na usambazaji wa nishati ya umeme na usimamizi wake.

Katika hali ya kushangaza swala la Rushwa limeshafanyiwa kazi na serikali ya awamu ya Tano kwa kasi kubwa kupambana na Rushwa na Ufisadi lakini bado Bodi ya MCC wanakuja na hoja nyingine nakuaacha ile ya kwanza ya Swala la Rushwa na ufisadi. Sasa swali la kujiuliza je, MCC wanataka tuuze uhuru wetu na utu wetu kwa pesa za msaada??



Mtizamo wangu;

Hatutakiwi tudharau misaada yoyote tunayopewa lakini tusikubali katu kuuza uhuru wetu au mali zetu kwa sababu ya msaada, tukikumbuka mwalimu Nyerere mwaka 1964 alikubali kuvunja uhusiano na Ujerumani Magharibi pale walipotaka kuingilia umoja wetu na Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar. Lazima tujue kuwa MCC ni sehemu tu ya Bodi inayojitegemea na sio serikali ya Marekani japo inasimamiwa na serikali ya Marekani, kwa hiyo kukosa msaada wa MCC hautatuathiri chochote katika uhusiano wetu na Taifa la Marekani kwani kauli ya MCC sio Kauli ya Serikali ya Marekani. Uhusiano wetu na Taifa la Marekani bado uko palepale na hautatetereka kwa sababu ya pesa za MCC.

Tukikumbuka AZIMIO LA ARUSHA la mwaka 1967 chini ya TANU lilikuwa na maudhui mbalimbali, moja lilikuwa ni swala la Pembe tatu za ukombozi ambapo lilitambua kwamba uhuru wanchi hautakuwa na maana wala hatutakuwa salama kama tukiendelea kuwa tegemezi , yaani kutegemea misaada , mikopo na uwekezaji kutoka nje. Kwa sababu mikopo haitapatikana ya kutosha na hiyo kidogo itakayopatikana itaambatana na masharti yatakayodidimiza nchi zaidi. Isitotoshe hata kama tungepata misaada, mikopo na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo vitahatarisha uhuru wetu. Mwalimu Nyerere katika kitabu cha Azimio la Arusha amesema, “Kujitawala ni kujitegemea, kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo kutoka Taifa jingine kwa maendeleo yake” mwisho wa kunukuu.

Pia tuambue kuwa Serikali ya Tanzania kwa awamu hii ya Tano chini ya Raisi Dr John Pombe Magufuli, imejipanga kikamilifu katika kukusanya kodi na kutafuta pesa kwa ajili ya kuendesha serikali bila hata kutegemea misaada ya wahisani ambayo ina masharti magumu na yenye ukandamizaji na unyonyaji ndani yake. Katika Pesa hizi za MCC lazima tujiandae kisaikolojia na sio kupotosha kwani Tukipatiwa pesa hizi au Tusipopatiwa pesa hizi bado tunaamini tutaweza endesha serikali yetu na maisha yetu kama kawaida. Tukumbuke kuwa pesa hizi zilianza kutolewa mwaka 2008 , Je, kabla ya hapo serikali ilikuwa inajiendesha vipi? Kama Tuliweza kujiendesha maisha yetu na serikali kwa kipindi hicho , hata sasa tutaweza. Hatudharau pesa za msaada na za wahisani lakini tusitumie kama kigezo cha kuondoa uhuru wetu na utanzania wetu kisa pesa za misaada. Lakini pia tutambue kuwa pesa za MCC sio marekani pekee anayechangia zipo nchi nyingine .

Lakini pia Vyama vyetu vya siasa nchini vijifunze utaifa na uzalendo, Ni aibu kuona chama cha Siasa cha Tanzania kinaungana na maadui wakutoka nje wasioitakia mema nchi yetu kwa kushabikia kila nia yao ovu juu ya maendeleo ya nchi yetu, tutambue kuwa si kila nchi kwa sasa inafurahia mafanikio ya Tanzania mfano uwepo wa Gesi, Madini yakutosha aridhini, wanyama pori wa kila aina, mlima Kilimanjaro,samaki wakutosha ziwani na baharini, ardhi ya kutosha, Bandal, misitu mikubwa, n.k hivi vyote tutambue si kila taifa litafurahia sisi kuwa navyo wanatamani tuvunje amani yetu ili waje wachukue mali zetu.

Rai yangu kwa Vyama vya upinzani nchini jaribuni kuweka utaifa kwanza na siasa baadae, swala la kukaa kushabikia vibaraka weupe wenye lengo la kutukandamiza sio jambo zuri hata kidogo na huo sio uzalendo. Katika Tamko lililotolewa na CHADEMA lenye kichwa cha Ujumbe “Hatma ya msaada wa Fedha za MCC kwa serikali ya Tanzania” ni tamko linaloonesha kushabikia swala la MCC kuikandamiza Tanzania. Tusilete siasa kwenye maswala ya kitaifa na maendeleo ya wananchi. Na hii inaonesha kuwa vyama hivi kama vitapewa dora vitaongoza nchi kwa kutegemea kuombaomba kwa wazungu na mwishowe vinaweza hata kuuza mali za nchi ili kutafuta msaada nje, kwa hili upinzani badilikeni wekeni utaifa mbele na sio tamaa ya uongozi.

Mwisho;

Lazima tujue kuwa msaada mtu anahiyari yake akusaidie au la. Vile vile misaada ni silaha kubwa kwa nchi za magharibi kulidumaza bara la afrika na kuhakikisha haliwezi kujitegemea bali liwategemee wao kwani misaada mingi inayotolewa na nchi hizi hailengi sehemu za maendeleo ya nchi na wananchi wake, na siku zote riba zake huishia kuwa kubwa kuliko misaada yenyewe na kwa kweli nchi yenye kujitambua haiwezi kujiendesha kwa kutegemea misaada hasa kutoka nchi kama marekani utanynyasika tu.


COPIED AND PASTED

Ni mtizamo wako juu ya MCC , binasfi namuunga mkono aliyeandika huu waraka kiukweli sio muda wa kumbembeleza msaada , bora tupambane tujitegemee.
 
Wewe nyie mijitu mkoje, Nyerere ni nani katika ulimwengu wa makosa, mbona mnamtukuza kama vile alikuwa Mungu ( and if at all Mungu exists). All men are fallible, no man is infallible , come on man
 
umeme wa kutoka shelui-mgongo-mingela-tulya-kidaru nishaukosa!mwigulu aliahidi kuendelea kuuvuta kutoka mgongo mpaka hapa nyumbani tulya,halafu utoke hapo uendelee mpaka kidaru,mwanga hadi manyara!nimeumia sana,sasa mpinzani wake yule mwanamke wa shoka jesica kishoa,ameshapata hoja ya uchaguzi wa 2020
 
Wewe nyie mijitu mkoje, Nyerere ni nani katika ulimwengu wa makosa, mbona mnamtukuza kama vile alikuwa Mungu ( and if at all Mungu exists). All men are fallible, no man is infallible , come on man
Mkuu,Nyerere ni kichaka cha CCM cha kujifichia pale mambo yanapo wawia ugumu
 
Ungeeleweka kama ungemjibu Bw. Polepole kwa hoja yakini kwa kila nukta aliyoijadili badala ya kulalama tu.


Kapongo, Kuna msemo wa siku nyingi unaosema: "Never wrestle with a pig, you will both get dirty and the pig likes it."

I thus chose not to wrestle with Polepole. Mwenye hekima hahitaji kujijustify mwenyewe, anaetetea hoja hii ya Polepole haitakii mema nchi hii. Lazima tutoke hapa, hizi approach zimefail, we need honesty and national interest at heart, not these selfish and greedy outlooks.
 
Maneno ya kweli na mifano halisi likini katika matumizi mabaya.

Hatulazimishwi demokrasia tunatakiwa kuiheshimu demokrasia.

Kwa kushindwa kufuata na kuenda haki tutalia na kusaga meno.

Amerika ina haki ya kufanya hivyo. Tunawajibu wa kuilaumu CCM. Fikiria walivyokomalia umeya wa Dar, walivyokanyaga haki nyingi za binadamu. JPM analofanya hakuna bila haki, ni ubatili mtupu

Ukifikiria kuwa maisha yako yanategemea Marekani basi utakuwa mtumwa wa kifikra. Bepari nambari moja hawezi kuwa rafiki yako ilhali lengo lake yeye ni kuendelea kunyonya na kuwa mnyonyaji mkuu wa dunia. Unapojiaminisha kuwa uhai wako unamtegemea huyu, du salaaaale sipati kusema, masharti yake magumu, ukianza kuyakubali haya basu ujue ni muda tu na yaleeee, lazima utakuja kuyakubali
 
Kapongo, Kuna msemo wa siku nyingi unaosema: "Never wrestle with a pig, you will both get dirty and the pig likes it."

I thus chose not to wrestle with Polepole. Mwenye hekima hahitaji kujijustify mwenyewe, anaetetea hoja hii ya Polepole haitakii mema nchi hii. Lazima tutoke hapa, hizi approach zimefail, we need honesty and national interest at heart, not these selfish and greedy outlooks.

Maneno kweli umeandika but you have just said nothing on the issue with lots of words,approach zipi zimefeli? Lini zilifanyika? Wewe unasema nini kifanyike, what is national interest at heart, Do MCC is for that thing you call 'national interest at heart? Who is for 'national interest at heart, you? Who else? Is MCC honesty, which are those 'honesty approach' you are suggesting to be adhered and followed? C'mon say something and not just words

https://www.google.com/url?sa=t&rct...E50LGg&usg=AFQjCNGjgU6Up1N9xcI627eIwEiXfm1Rmw
 
m
Africa bila misaada ni ngumu kuendelea tuache mbwembwe tuwe wakweli, Kwetu ni pigo kubwa sana
msingi wa MCC NI UTAWALA BORA. ukielewa ni nini utaona sababu ya kusitishwa kwa msaada huo. ni sawa na AMRI YA UPENDO KWA WAKRISTU kila kitu chema chahusika. MIMI NASIKITIKA KUUKOSa.JE HAWAELEWI ZANZIBAR NI ZANZIBAR NA TANGANYIKA NINTANGANYIKA.
 
Back
Top Bottom