Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Tangu lini muajiriwa wa kitengo akaipinga serikali yake?? Je tunafahamu umuhimu wa fedha za kigeni kwenye mzunguko?? Je unafahamu mataifa ya nje yakiacha kutoa nsaada thamani ya shilingi itashuka dhidi ya dola?? Je unafahamu uwezo wa nchi yetu kuuza nje ili kupata fedha za kigeni upo chini sana kiasi kwamba misaada ya wahisani ndio inaongeza fedha za kigeni kwenye mzunguko wetu, je unafahamu hali hii ikiendelea ya kukosa misaada ya wahisani bidhaa za nje zitakuwa ni ghali sana kiasi cha watanzania wengi kushindwa kuzipata?
Je wajua asilimia 50+ ya bajeti inahitaji fedha za wahisani, je wajua kukiwa na mdororo wa kiuchumi hayo makusanyo yatashuka hadi aibu? Yapo mengi ila ngoja nichangie taifa hapa kwa kunywa castle lager ya baridi
Umemaliza kabisa, fedha za kigeni zikipungua kwenye mzunguko uchumi wetu utaathirika sana na tutazidi kuingia kwenye mikataba mibovu ya kuuza rasilimali zetu.
 
Hakika hii ni sawa na lile shairi maarufu la kitabu cha primary liitwalo SIZITAKI MBICHI HIZI hii ilikuwa ni baada ya sungura kushindwa kuufikia Mkungu wa ndizi! Kaka yetu polepole anataka kutuambia pesa za MCC siyo nzuri na hazina manufaa yoyote zipo kwa ajili ya kutunyonya!

Nataka kujua kama hii kauli aliwahi kuipost hapa kipindi hicho tunapata hizi fedha hususani mwaka Jana! Miradi ya maendeleo ya umeme vijijini tumeianzisha tukitegemea hizi fedha na umeme utatufanikisha kufikia nchi ya viwanda leo hatuna hizi fedha kujibaraguza tunasema hatuzitaki mbichi hizi!

Kwanini Tanzania isijitokeze hadharani na kuitangazia dunia kuwa hatutaki misaada yoyote kuanzia leo kuliko huu unafiki wa kusubiri tukose ndiyo tuseme hatuzitaki mbichi hizi?

Unafiki ni jipu namba moja nchini Tanzania
 
naomba nikuulize, walipo sitisha msaada walitoa sababu za wao kufanya hivyo, je hizo sababu ni kwa manufaa yetu kama watanzania wa manufaa yao?
 
Tangu lini muajiriwa wa kitengo akaipinga serikali yake??

Je tunafahamu umuhimu wa fedha za kigeni kwenye mzunguko??
Je unafahamu mataifa ya nje yakiacha kutoa nsaada thamani ya shilingi itashuka dhidi ya dola??
Je unafahamu uwezo wa nchi yetu kuuza nje ili kupata fedha za kigeni upo chini sana kiasi kwamba misaada ya wahisani ndio inaongeza fedha za kigeni kwenye mzunguko wetu.

Je unafahamu hali hii ikiendelea ya kukosa misaada ya wahisani bidhaa za nje zitakuwa ni ghali sana kiasi cha watanzania wengi kushindwa kuzipata?

Je wajua asilimia 50+ ya bajeti inahitaji fedha za wahisani, je wajua kukiwa na mdororo wa kiuchumi hayo makusanyo yatashuka hadi aibu?
 
Mi sijamuelewa mtoa mada kama ishu sio (kukandamizwa kwa demokrasia) uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya makosa ya mtandaoni,
Je kwanini wasitishe jambo lenye maslahi kwao kuliko kwetu? Ingekua sisi ndy tumezikataa fedha za MCC 2 kwa kuwashtukia kama mtoa mada anavyosema (kuwa MCC 2 ina maslahi kwa makampuni ya kimarekani) hoja yake ingekua na mashiko otherwise ni ule utetezi wa Pro ccm kuwa we have nothing to loose kwa haya maamuzi ya MCC. Lengo ikiwa ni kuficha ukweli wa sababu ya TZ kunyimwa hizo fedha.tumenyimwa kwa sababu ccm imebaka demokrasia
Eewa mantiki ya argument, si kwamba we have nothing to lose we will lose obviously.
Lakini mtu akitaka kukuchukulia mkeo kwa vile anakufadhili, siiku nyingine hata heshima ya kutetea utu wako unakuwa huna!!
 
KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Uhuru upi unaousemea mkuu? Kuhusu zanzibar msitudanganye tunaelewa kila kitu
 
Tatizo kubwa la wachangiaji wa JF wanapenda sana kuchangia hoja mbalimbali kupitia itikadi zao za vyama hata kwenye mambo ya msingi. wakati mwingi huwa nachukia sana watu wa namna hiyo, ebu tujaribu kusoma kwa makini na kumwelewa vema mtoa mada, ukifanya hivyo utachangia vizuri sana.
 
Kama ni Huyu huyu Polepole kasema,basi sishangai maana yeye anafanya kazi ya kuwadi vilevile.Nasikitika kukosa umeme vijijini mwetu kisa Zanzibar.
 
Hahahah PolePole bwana, Angejiuliza maswali yafuatayo
(1) Je Pesa za MCC tulikuwa tunazihitaji au hatuzihitaji?
(2) Je tulisaini masharti ya MCC hapo awali au la?
(3) Je Kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kulizingatia sheria ya uanzishwaji na ufanyaji kazi wa ZEC au la?
(4) Mbona tulipokuwa tunaqualify kupata pesa za MCC kwa vigezo vilevile vya Demokrasia, kupiga vita rushwa n.k mbona tulikuwa tunafurahia na kujipongeza lakini tulikuwa hatuwaambii hao wahisani kuwa Tuacheni na mambo yetu ya ndani?
(5) Je Uchaguzi wa Marudio ulikuwa wa Kiuwakilishi?, Je unaweza Kusema uliridhiwa na Wananchi wa Zanzibar wakati Kisiwani Pemba tuliona wananchi wengi wakijifungia ndani badala ya kwenda kupiga kura?

Polepole ajiulize
(1) Ni uongozi gani uliooneshwa na tume katika uchaguzi wa marudio lakini uongozi huo huo ushindwe kuonyeshwa baada ya mtu mmoja kufuta uchaguzi wa awali kinyume cha sheria?

Ninachokiona
(1) Waroho wa madaraka wakishindwa kukidhi haja za Kidemokrasia hukimbilia katika "Utaifa" na Uzalendo
(2) Iweje Usaini masharti ya MCC, halafu at one point in time ushindwe hayo masharti usingizie "eti uzalendo" na "heshima ya nchi?

Namwambia PolePole
(1) Uzalendo ni kuheshimu Demokrasia
(2) Uzalendo si kuweka mbele maslahi ya chama na badala yake kuweka mbele maslahi ya Taifa
(3) MCC ni chombo cha serikali ya Marekani, Kauli ya Bodi ni kauli ya Serikali ya Marekani, Ndugu Polepole hapa usizunguushe maneno

Nimkumbushe PolePole

(1) Si miezi mingi iliyopita alikuwa akipigania katiba ya Warioba, Lakini akumbuke Katiba ya Warioba ilisisitiza sana jambo la Demokrasia na utawala wa sheria, basi iweje PolePole ashindwe kuona kuwa kwa misingi yote ya ufutwaji wa Matokeo ya awali hayakuzingatia sheria ya Tume, na Uchaguzi wa Pili ambapo CCM wameshinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba siyo Realistic na hivyo kunajisiwa kwa wazi kabisa kwa demokrasia?

Nimshauri Polepole
(1) Chagua kuwa baridi au moto, usiwe vuguvugu, haki na batili havitengamani
(2) Chagua kuwa kama Martin Luther King Jr kwamba Injustice anywhere is an Injustice everywhere, Na kwamba Justice is Indivisible, Ama Chagua kuwa kama Machiavelli "By any means Necessary"
 
We Polepole kweli unafikiria polepole .............. huo mtazamo wako wa upande moja tena defensive!!

Siku ukigeuka upende wa pili na kuutizama basi utaelewa!! Next time jaribu kufanya analysis siyo kutoa mitizamo yako binafsi kwa maslahi binafsi!!

Unachokifanya hapa ni kusisistiza Umaskini jeuri tu ....... nothing else!!
 
* YA DAMBISA MOYO, MCC NA RAIS MAGUFULI

Naomba nianze na nukuu zifuatazo.....

"In the past fifty years more than $1Trillion in development related aid has been transferred from rich countries to Africa. Has this assistance improved the lives of Africans? NO. Infact across continent, the recipients of this aid are not better of as a results of it, but worse- much worse"... Dambisa Moyo

"Dambisa Moyo makes a compelling case for approach in Africa. Her message is that, "Africans time is now" it is time for Africans to assume full control over their economic and political destiny. Africans should grasp the many means and opportunities available to them for improving quality of life" kofi Annan, Frm UN secretary


Mara baada ya kusikia na kusoma taarifa ya MCC nilijikuta nikiwakumbuka wanazuoni kama Salmin Amir, Mwalimu Nyerere, Prof. Issa Shivi na Dambisa Moyo....

Nilipoendelea kutafakari nikakumbuka yaliyojiri katika mkutano wa Q&A session, University of New South Wales ambapo tajiri No.1 duniani alipomshambulia wazi wazi mchumi huyo wa Zambia, "Dambisa Moyo" kutokana na kile alicho kiandika katika kitabu chake cha "Dead Aid, Why is Not Working and How There is Another Way for Africa"

Bill Gates alisema Dambisa Moyo hajui chochote kuhusu misaada inayotolewa katika nchi zinazoendelea badala yake kitabu chake kimejipambanua katika kueneza ushetani" Rejea "Bill Gates shocking personal attack on Dr. Dambisa Moyo and Dead Aid, 2013"..

Kwa kutarajia ama bila kutarajia leo hii watanzania na wanazuoni tunarudi katika maktaba zetu na kuanza kumsaka Dambisa Moyo. Hii ni baada ya shirika la MCC kusimamisha misaada yake na kupelekea Tanzania kukosa jumla ya 1trn ambazo zingeelekezwa kwenye umeme na umeme vijijini. Hofu kubwa iliyotanda kwa sasa, je jumuiya za ulaya na nchi zingine wahisani watachukua hatua gani?

Lazima tukubali ya kwamba, kama Nchi tusiruhusu mataifa ya kigeni kuingilia masuala yetu ya ndani. Pia lazima tukubali kuwa Tanzania sio kisiwa ama jangwa, tunaishi ndani ya jumuiya ya kimataifa. Lazima kuna mambo yanatulazimu kuyakubaliana nayo kwa misingi ya kimataifa huku tukiwa huru kuendesha mambo yetu ya ndani..

Haya yote yanapotokea, binafsi naamini na wote tunakubakiana kwamba ni katika kujitegemea ndipo maendeleo endelevu na ya kweli upatikana kama anavyosema Dambisa Moyo... Nchi masikini ikiwemo Tanzania tunapokea fedha nyingi sana kutoka nje lakini bado hatujaweza kutoka kwenye mtego wa kupambana na maadui watatu, ujinga, maradhi na umasikini. Ukweli ni kwamba fedha hizo na miradi mingi ya maendeleo inayotolewa na wageni hua na agenda za siri na mbaya zaidi hutufanya tuendelee kuwa wategemezi...

Juzi Mh. Rais Magufuli alipokuwa katika kanisa la Azania alikemea kwa nguvu zote dhana ya utegemezi na ndani ya dhamira yake alionyesha kupambana kwa nguvu zote ili kulifanya Tanzania kuwa Taifa huru kiuchumi ili kuendesha mambo yake kiuhuru zaidi Hatuna budi kumuunga mkono katika hili...

Dhana hii ya Rais Magufuli pamoja na hatua za MCC ni wito kwetu kuwa lazima watanzania tuchape kazi zaidi na zaidi, na kubwa zaidi ni kushiririki kikamilifu katika ukusanyaji wa kodi. Na katika hili ni vyema kila moja na kwa kila manunuzi afanyalo awe wakala wa TRA.... Ni jambo la wazi kwamba kwa kipindi fulani wananchi tutaumia hivyo itatulazimu kufunga mikanda kwa muda...

Kwa mantiki hiyo, ni muda muafaka kwa watanzania chini ya usimamizi ya serikali ya awamu ya tano kurudia misingi mikuu ya Azimio la Arusha ambayo mojawapo ni falsafa ya KUJITEGEMEA ili tuondokane na utegemezi uliokithiri.....

Mchambuzi Huru: Peter Kasera.... (BA Sociology, MA Development Management.... Phd (on progress)... )...
 
Ndg polepole anataka kutuaminisha kuwa kukosa fedha za maendeleo si tatizo ila utanzania wetu.why Tanzania ilikubali kupata huu ufadhili? Mimi kama mtanzania naumia sana maana Nchi yangu ingepata umeme vijijini na hivyo kuchochea maendeleo.Hii habari ya mtoa mada kweli haiingii akilini.
 
What good comes from you Polepole aka msaka tonge...you are not very smart ndugu...Kwa taarifa yako Muungano wa Unguja na Danganyika hakuna watu wengi wanaoupenda..labda wewe na ukoo wenu wa panya CCM...MCC wewe unaijua kazi yake Duniani..wenye akili ndogo kama wewe unadhani MCC ni sawa na kale ka NGO kako pale mabatini kijitonyama...ushabiki mpka unapoteza power of reasoning kaka..nakumbuka wakati ukija pale shirika la kazi (ILO) kazi house kuomba vibarua vya consultancy umenyonyoka nywele...sasa umepata matako yanalia mbwata..kaka kumbuka watanzania wengi watakaoteseka kwa ukosefu wa siasa bora kama alivyokuwa akitamani baba wa taifa Mwl J.K.Nyerere...baada ya MCC watakaofuata ni EU then IDAs nyingnge pengine ...kisha watu wa mkokoteni njaa zitawabana mpaka wakome...UGAIDI will be their next option..take it from me...na sifa ya kushamiri kwa ugaidi ni njaa na watu wa zanzibar wana hasira ya kupokwa haki yao ..utakiona na uchochezi wako kaka..bora ujifunze kukaa kimya maana umewaumiza watanzania wengi wanaodai haki na maisha yenye tija katika nchi yao...nenda youtube ujaribu kusikiliza some of your previous speeches especially during 2015 election campaigns...
 
Mimi siwezi kukupongeza unless ujibu maswali yangu yafuatayo;

Kwamba kama CCM na serikali walifahamu fika kuwa fedha hizi zina masharti ya "kuhamisha hamisha magoli" (kitu ambacho mimi sikiamini kwa sbb from the beginning mlishiriki kwenye majadiliano na kisha mkatia saini mkataba ule......na hapa maana yake mlikubaliana na vigezo vilivyowekwa ili kupata fedha hizo), kwa nini leo mnaleta hoja ya sizitaki mbichi hizi???

Kwamba, Bwana Jakaya Kikwete Rais wa awamu ya nne kusema kweli MCC ni zao la harakati zake ktk kuhakikisha miradi ya maendeleo inapata ufadhili, inatekelezwa. Ndiyo maana ilikuwa karibu kila siku (hapa nimechomekea) anakwea pipa kwenda USA hata tukampa jina la "Mr FastJet", hakujua impact ya hii kitu?


Aisee kusema ukweli, CCM nyie mnatuchanganya tu na hata hatuelewi mnakotupeleka mpaka hatua hii. Haiwezekani jambo ambalo nyie wenyewe mlilisimamia leo mnakuja mnasimama hapa mnalikana!!

Huu ni uwendawazimu 100%!!
 
Ubakaji wa demokrasia uliofanywa na CCM huko Zanzibar mchana kweupe (bila kificho) ni wa aibu sana na ingekuwa ni aibu kwa asasi ambazo zimekuwa zikisaidia kuchochea ukuaji wa demokrasia na utawala bora kuunga mkono ubakaji huu. Inawezekana kabisa hizo pesa ni kidogo sana na pengo linaweza kuzibwa na washikaji wengine kama vile China, lakini wenzetu hawa wa Magharibi huwa nyekundu wanaiita nyekundu, kijiko ni kijiko sio koleo - walichofanya hapa ni kueleza mtazamo wao. Ninawaunga mkono. Watanzania CCM imetuathiri kuwa na fikira mgando na tunataka kuwalazimisha watu wengine waione dunia kwa fikira hizo hizo zilizoganda!
 
Polepole hebu chukua muda soma hizi issue wanazozifufatilia na kuzi facilitate hao MCC...je kwako hazina umuhimu kwa ustawi wa taifa? inashangaza sana unachotaka kutuaminisha...unajifanya sijui nini? You are a great pretender!!!

Initiatives

Aid Effectiveness


Since its creation in 2004, MCC has been advancing and accelerating the conversation on aid effectiveness.

Climate Change
MCC is committed to helping our partner countries adapt to climate change and mitigate emissions through climate resilient, low carbon economic development.

Country-Led Poverty Reduction
Country ownership—or country-led development—has been broadly embraced by the international donor community as a critical element of international development aid.

Democracy
One of MCC’s core principles is that aid is most effective in countries with a sound commitment to accountable and democratic governance.

Digital Strategy
MCC has been at the forefront of transparency in delivering aid.

Environmental and Social Performance
MCC’s Environmental and Social Performance team works with partner countries to integrate internationally-accepted principles of environmental and social sustainability into the design and implementation of compacts.

Fighting Corruption
Controlling corruption a key indicator in selecting countries for compact eligibility and throughout the compact lifecycle. MCC—with the MCAs—promotes measures to prevent, detect and combat corruption before it occurs and to address problems after they emerge.

Food Security
With its partner countries in the lead, the MCC portfolio of investments has been on the forefront of addressing food security priorities since MCC’s first compact in 2005.

Gender and Social Inclusion
MCC recognizes that gender and social inequality are significant constraints to economic growth and poverty reduction.

Governance Data Alliance
MCC leads the charge to uncover the best data available to fight corruption by partnering with experts to form a Governance Data Alliance. MCC and the alliance are committed to filling the gaps for measuring governance.

MCC & The African Growth & Opportunity Act (AGOA)
MCC has obligated nearly $3 billion for trade capacity building in AGOA countries on infrastructure like roads and power, on upping productivity of small and medium-size businesses and export-heavy sectors, and leveraging policy and regulatory reforms.

MCC and Power Africa
Through its compacts in partner countries, MCC expects to invest nearly $2 billion to support Power Africa, the U.S. Government's effort to double access to electricity in sub-Saharan Africa.

MCC and the Sustainable Development Goals
MCC supports its partner countries in their efforts to achieve the SDGs and improve the lives of their people by fighting poverty through inclusive economic growth.

MCC and the U.S. Global Development Policy
MCC applies the principles of economic growth, strong policies, country-led plans and rigorous evaluation to create a more stable and prosperous future for the world's poor.

MCC's Public-Private Partnership Platform
Development needs around the world will not be met by foreign assistance alone. Official development assistance must increasingly catalyze other resources to finance development – including private-sector investment. Here's one way MCC is doing just that.

Measuring Governance
In selecting partner countries, MCC relies on independent public data that captures as clearly as possible the actions governments take to fight corruption. MCC is seeking improved and expanded indicators from the institutions that produce this data.

Open Government
MCC has been at the forefront of transparency in delivering aid.

Partnership for Growth
MCC and other U.S. Government agencies have joined together to coordinate Partnership for Growth (PFG), a partnership between the United States and a select group of high-performing developing countries to accelerate and sustain broad-based economic growth.

Smart Aid Series
Since its founding, MCC has sought innovative ways to reduce poverty through economic growth. Smart Aid brings together development practitioners and MCC staff to share best practices, lessons learned, and engage in a dialogue to effectively move aid forward.
 
Back
Top Bottom