Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Daah PhD yako ukifanikiwa kuipata, utakua unafanana akili na yule jamaa wa Moro anaye lialia.
 
Wachambuzi watakuwa wengi msimu huu..Bado kuna nafasi za wakuu wa wilaya kwa kigezo cha kujitegemea..Mboma CCM mmeshindwa kujitegemea kupata ushindi halali mpaka muuite jeshi kuwasaidia.
 
Ccm ndio ina ukoloni mamboleo, litakuwa jambo litakalowafurahisha wengi siku tukisema kwaheri ccm.
 
Watanzania wa kawaida hizo hela zitolewe, zisitolewe, tofauti kwao ndogo sana. Ugumu wa maisha uko pale pale.

Kwa hiyo zisipotolewa kwa kushinikiza demokrasia inaweza kuwa bora.

Bottom line, huwezi kupanga bajeti kwa hela za msaada. Mfadhili ana haki ya mwisho kuamua kutoa au kutotoa msaada.
 
Ningeunga mkono hoja kama kichwa cha habari kingesema kwaheri ccm,kwaheri mkoloni mweusi.Yaani wewe kwa akili yako,ni mpaka Marekani akwambie kwamba kile kilichofanyika Zanzibar ni ushetani?.Tatizo la nchi kuwa na kila kitui fake.
 
Hahahah PolePole bwana, Angejiuliza maswali yafuatayo
(1) Je Pesa za MCC tulikuwa tunazihitaji au hatuzihitaji?
(2) Je tulisaini masharti ya MCC hapo awali au la?
(3) Je Kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kulizingatia sheria ya uanzishwaji na ufanyaji kazi wa ZEC au la?
(4) Mbona tulipokuwa tunaqualify kupata pesa za MCC kwa vigezo vilevile vya Demokrasia, kupiga vita rushwa n.k mbona tulikuwa tunafurahia na kujipongeza lakini tulikuwa hatuwaambii hao wahisani kuwa Tuacheni na mambo yetu ya ndani?
(5) Je Uchaguzi wa Marudio ulikuwa wa Kiuwakilishi?, Je unaweza Kusema uliridhiwa na Wananchi wa Zanzibar wakati Kisiwani Pemba tuliona wananchi wengi wakijifungia ndani badala ya kwenda kupiga kura?

Polepole ajiulize
(1) Ni uongozi gani uliooneshwa na tume katika uchaguzi wa marudio lakini uongozi huo huo ushindwe kuonyeshwa baada ya mtu mmoja kufuta uchaguzi wa awali kinyume cha sheria?

Ninachokiona
(1) Waroho wa madaraka wakishindwa kukidhi haja za Kidemokrasia hukimbilia katika "Utaifa" na Uzalendo
(2) Iweje Usaini masharti ya MCC, halafu at one point in time ushindwe hayo masharti usingizie "eti uzalendo" na "heshima ya nchi?

Namwambia PolePole
(1) Uzalendo ni kuheshimu Demokrasia
(2) Uzalendo si kuweka mbele maslahi ya chama na badala yake kuweka mbele maslahi ya Taifa
(3) MCC ni chombo cha serikali ya Marekani, Kauli ya Bodi ni kauli ya Serikali ya Marekani, Ndugu Polepole hapa usizunguushe maneno

Nimkumbushe PolePole

(1) Si miezi mingi iliyopita alikuwa akipigania katiba ya Warioba, Lakini akumbuke Katiba ya Warioba ilisisitiza sana jambo la Demokrasia na utawala wa sheria, basi iweje PolePole ashindwe kuona kuwa kwa misingi yote ya ufutwaji wa Matokeo ya awali hayakuzingatia sheria ya Tume, na Uchaguzi wa Pili ambapo CCM wameshinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba siyo Realistic na hivyo kunajisiwa kwa wazi kabisa kwa demokrasia?

Nimshauri Polepole
(1) Chagua kuwa baridi au moto, usiwe vuguvugu, haki na batili havitengamani
(2) Chagua kuwa kama Martin Luther King Jr kwamba Injustice anywhere is an Injustice everywhere, Na kwamba Justice is Indivisible, Ama Chagua kuwa kama Machiavelli "By any means Necessary"
Mkuu watu kama PolePole nilisema ni hatari kwa ustawi wa Taifa, wanaishi kwa uongo na ubabaishaji.

1. Tulivunja uhusiano na Uingereza tukiamini thamani(values) si kikundi cha wachache

Pole pole haelezi miaka 9 baadaye wazee wa baraza la TANU walishinikiza kurudishwa mahusiano baada ya kuona sisi ndio 'loser' na kwamba tuangalie interest za Taifa

2. Rais Kiwete alitumia muda mwingi sana kwenda kushawishi MCC.
Tulipoa ahidiwa, Viongozi walitamba sisi demokrasia kubwa Afrika tumepata msaada.
PolePole hawakusimama hawakuhadharisha hatari ya mashrti, walishangilia

3. Shein na JK wakishangilia umeme kusambaa Pemba kupitia MCC.
Wakiweka malengo ya nchi kuwa na nishati hadi vijijini kwa muda mfupi.

4. Tujiulize, Jecha anafuta uchaguzi katibu mkuu kiongozi alitoa kauli majadilian yanaendelea yakikamilika MCC itapewa taarifa!! Serikali iliropiti MCC. Tulikaa kimya

5. Ni mazingira gani yametufanya tuvunje uhusiano na MCC?

Tunavunja uhusiano na MCC kwa picha mbaya. Huwezi kutenga MCC na Serikali ya Marekani. Hawa ni wababe wakisema Tanzani... tutakimbiwa na dunia. Ni ukweli tu

Tumevunja uhusiano kwasababu ya kumweka Shein madarakani.
Yaani kundi la Wahafidhiana wasiozidi kumi limeweka nchi ya watu milioni 45 rehani.

Kundi halina uzalendo wakati Jecha anatumbikiza Taifa la watu milioni 45 matatizoni.
Wakati Shein anagomea matokeo kwa kigezo cha demokrasia ya Afrika.

Wanatuaminisha kilichofanyika ZNZ ni demokrasia tuungane nao kwa uzalendo wa kihuni. Wanajua watakaposema sisi ni mazezeta tutawaunga wamkono!

Hapana! Wazalendo wa nchi hii tusimame pamoja na kumwambia Magu, ameliweka Taifa rehani kwa interest za Shein na wahafidhina wanaoishi 'peponi kwa sasa''

Masilahi ya watu wasiozidi 10 ni bora kuliko masilahi ya watu milioni 45!!!
Hapana tukatae na kumwambia Magu uzalendo huo ni kundi lake .

Uzalendo wetu ni kwa masikini milioni 40 wa Taifa hili.
Tunasema wazi, hili MCC wapo sahihi, wananchi milioni 45 wapo sahihi.

Waliokosea ni Magufuli akitetea watu wasiozidi 10 kwa gharama ya watu milioni 45

Tuweke siasa kando, tukemee, Wazalendo ni milioni 45 wanaoteseka kukosa MCC ni muhimu kuliko watu wasiozidi 10

Hili ni la Magufuli! Hakuna uzalendo isipokuwa wa watu milioni 45!
Tusimame na kumwabia Magufuli hapana! hili na wenzake wachache hautukubali
 
Ningeunga mkono hoja kama kichwa cha habari kingesema kwaheri ccm,kwaheri mkoloni mweusi.Yaani wewe kwa akili yako,ni mpaka Marekani akwambie kwamba kile kilichofanyika Zanzibar ni ushetani?.Tatizo la nchi kuwa na kila kitui fake.
Huo ni mtazamo wako wewe ambaye yawezekana unawaza sana mabadiliko ya chama. Mbona na wewe hujaja na hoja ya kuniaminisha kuwa Marekani ni wapenda haki na demokrasia?
 
The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation’s first trade and investment mission successfully concluded today in Malawi with nine American firms hearing from top U.S. and Malawian officials about opportunities in the country’s energy sector.

The trade and investment mission, organized with the U.S. Department of Commerce and the first in MCC’s 11-year history, began earlier this week in Tanzania. It promoted U.S. exports and expanded U.S. companies’ presence in Africa by introducing American firms to opportunities in the energy sector. The mission also contributed to the goals of Power Africa, a whole of U.S. Government effort designed to double access to electricity in sub-Saharan Africa.

“The Malawian power sector is primed for outside investment, which will make a significant impact on the country’s economic growth,” said Kamran M. Khan, MCC’s Vice President for Compact Operations and the mission lead. “Throughout this mission, delegates heard about the opportunities that could help create jobs at home and abroad.”

The companies met with key officials from the Government of Malawi—including President Peter Mutharika—as well as members from the Malawian private sector and civil society. The delegates also met with U.S. Ambassador to Malawi Virginia E. Palmer.

The mission delegates met with Bright Msaka, Malawian Minister of Natural Resources, Energy and Mining; Joseph Mwanamvekha, Minister of Trade and Industry, Joshua Nthakomwa, Director of Investment Promotion and Facilitation at the Malawi Investment and Trade Center; and high-level representatives from the Electricity Supply Corporation of Malawi Limited and the Malawi Energy Regulatory Authority.

MCC’s compact with Malawi will invest up to $350.7 million to revitalize the country’s power sector and improve the availability, reliability and quality of the power supply—ultimately attracting trade and investment and promoting economic growth.

While the trade and investment mission introduced American firms to opportunities in Tanzania and Malawi, MCC-funded investments are procured openly, fairly and transparently.
 
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).
 
CCM ijifunze kuheshimu demokrasia, wakipigwa chini na wapiga kura wasitapetape na kutumia mabavu wakubali matakwa ya wananchi waliowaweka madarakani, vinginevyo wanaiweka nchi pabaya. Kunyimwa msaada ni jambo dogo lakini kubwa ni kuivuruga amani.
 
..ndivyo inavyokuwa kwa miradi mingi inayopata fedha za ufadhili toka nje.

..China au Japan wakikupa fedha za ujenzi wa miundombinu lazima wakandarasi watoke kwao.
 
Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
exactly ambaye hatokubaliana na maoni yako bas awekewe ubongo wa kichina sina cha kuongezea yamejitosheleza
 
All said, ka wakija Tanzania na mipango yao tukapata umeme vijijini.nchi nzima, barabara zote zikawa na lami, I will never mind their presence anyway as long as I am a free man in the real sense
 
Hongera mkuu kwa maneno kuntu.
Najua umepiga ikulu ya jamaa zetu.
Big up man
 
Tumefika mahali tulipo kwasababu ya watu kama akina Pole Pole. wamefungwa ufahamu, wanafikiria mambo kwenye narrow angel kisha wanatumia our weakest political system to lure our people. Utashangaa kuna watu humu ndani watamsifu Pole pole, kwa kukurupuka bila kufanya a critical analysis ya huu upupu wake.

Unakosea halafu unaanza kufit uongo na reasoning za kitoto to justify the lost game, only resulting from greedy and arrongance iliyochanganyika na chronic ego. That is not patriotism.

Wastage of our time. We need more of brain power in this country, not these cheap politics.
 
Duh, inahitaji ujasiri kweli kuweza kutetea hoja hii. baadhi yetu tumekuwa tukijaribu kumnukuu mwalimu nyerere katika muktadha wa kutunufaisha sisi na kuacha dhana nzima ya mwalimu.

Pamoja na mambo mengine kujaribu kuwaaminisha watanzania kuwa MCC 2 ililenga kunufaisha sektba binafsi ya marekani hapa ndugu yangu umeamua kujitoa ufahamu kuliko unavyofahamika kwa wengi.
Wakati wa kampeni Mgombea wa CCM wa nafasi ya urais John Magufuli alikuwa akijinadi kuwa umeme utafikishwa vijijini kwani wamarekani wamekubali kutoa fedha za MCC wakati ikionekana wana mwelekezo huo.
Huyo mgombea wa CCM alikuwa nafanya kampeni katika nchi gani na vijiji ambavyo vilikuwa vikipelekewa umeme ni vya marekani? Nakubaliana na mchangiaji hapo juu kuwa umesahau hadithi ya SIZITAKI MBICHI HIZI.
Mtajaribu kutafuta maneno yote mabaya kwa sasa juu ya MCC lakini ukweli unabaki palepale kuwa sisi ndio waathirika zaidi. Iweje leo ndio tulione hilo la mradi huo hautunufaishi sisi? na kama ukweli ndio huo wa misada hii haitufai kwanini hatutamki moja kwa moja katika sekta nyingine lukuki. Mbona kila siku tunasikia "..... kwa hisani ya watu wa marekani", si inajulikana kuwa anayempila mpiga zumari ndiye anayechagua mziki, iweje leo Polepole aone ubaya wa msaada ambao ni lazima uambatane na mahsrti hata kama unatoka kwa mjomba.
Kama MCC ni wabaya kwanini tuendelee na wamarekani katika maeneo mengine si tuwakatae tu ili tuendelee pekeyetu kama tunao uwezo hata wa kutoa dawa za ARV na TB kwa watu wetu.
Inahitaji b usara sana kujitoa ufahamu kutetea upande wa tanzania kukosa msaada huu.
 
Back
Top Bottom