Umemaliza kabisa, fedha za kigeni zikipungua kwenye mzunguko uchumi wetu utaathirika sana na tutazidi kuingia kwenye mikataba mibovu ya kuuza rasilimali zetu.Tangu lini muajiriwa wa kitengo akaipinga serikali yake?? Je tunafahamu umuhimu wa fedha za kigeni kwenye mzunguko?? Je unafahamu mataifa ya nje yakiacha kutoa nsaada thamani ya shilingi itashuka dhidi ya dola?? Je unafahamu uwezo wa nchi yetu kuuza nje ili kupata fedha za kigeni upo chini sana kiasi kwamba misaada ya wahisani ndio inaongeza fedha za kigeni kwenye mzunguko wetu, je unafahamu hali hii ikiendelea ya kukosa misaada ya wahisani bidhaa za nje zitakuwa ni ghali sana kiasi cha watanzania wengi kushindwa kuzipata?
Je wajua asilimia 50+ ya bajeti inahitaji fedha za wahisani, je wajua kukiwa na mdororo wa kiuchumi hayo makusanyo yatashuka hadi aibu? Yapo mengi ila ngoja nichangie taifa hapa kwa kunywa castle lager ya baridi