Mtazamo hasi wajamii yetu kuhusu makabila haya . . !!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,712
Ni jana tu jamaa yangu mmoja aliambiwa na baba yake kuwa;"nitakusapoti kwenye ndoa yako lakini usimuoe huyo mwanamke ulie nae",kijana alipomuuliza baba yake sababu ya kumkataa mchumba wa kijana wake,mzazi alisema eti kabila la huyo mwanamke hawajatulia.Mzee yule akamuorodhezea makabila mengine kwamba asijidanganye kuoa,makabila hayo ni Wanyiramba(hili ndilo kabila la mchumba wake),Wahaya,Wasukuma wa Nasa na Wachaga wa Machame.Mzee yule alidai kuwa Wahaya na Wanyiramba wanasifa zinazofanana yaani vicheche.Wasukuma wa Nasa na Wachaga wa Machame nao wana sifa zinazofanana yaani Uchawi,wanakawaida ya kuwaua waume zao baada ya kupata mafanikio.Kwanza nikiri kuwa hoja hizi zina ukweli.Lakini pia ukweli huo ulikua una nguvu sana zamani sio sasa.Ni vyema jamii ikaacha kuyahukumu makabila hayo leo.Nasema hayo kwani leo ni vigumu sana kumjua mwanamke mwadilifu kwa misingi ya kabila.Tabia za kupenda kufanya ngono hovyo na kwenda kwa waganga iko karibu kwa kila mwanamke,kama ni karibu kila mwanamke basi inayahusu makabila yote(hata wanaume wana tabia hizi ila kwa malengo tofauti).Nadhani huu ni wakati wa kubadilika na kuishi kiuhalisia na sio kimazoea!!
 
ni kweli mkuu, mfano zaman wanawake wa pwan ndio walikuwa wanasifika kwa mambo ya chumban lakini sasa kutokana na mchanganyiko wa makabila, utandawaz huu mambo mengi yamebadilika kuna haja ya kuacha kuoa au kuolewa na kabila na badala yake kuoa ama kuolewa na mtu binafsi, hii kitu imepitwa na wakat. Inawezekana kuna ambao bado wana hzo tabia bt ni wachache na hawatoshi kufanya kabila zima lihukumiwe.............

vijana wengi sana saa hz wanaumizwa kwa kushindwa kuwa na wale wawapendao kwa sabab ya mtazamo huu...............
 
Nambe umesomeka vyema sana!!
 
Last edited by a moderator:
Ilikuwa kawaida yetu zamani kuwachagulia wenzi watoto wetu. Kulikuwa na vigezo vinavyoangaliwa, ikiwa ni pamoja na mila na desturi za huyo mwenzi, pamoja na tabia. siku hizi vijana mnadai hayo yamepitwa na wakati. Pamoja na hayo, inabidi mfahamu kuwa ndoa huunganisha watu wawili, na vile vile familia mbili. kutokana na vijana kujichagulia wenzi kwa vigezo vichache (Mfano:- ukubwa wa makalio) bila kujali tabia, mila na desturi, ndoa nyingi zimeishia kuwa matatizo,

USHAURI WANGU

Vijana mkubali sisi wazazi wenu tuwachagulie wenzi
 
Kuna tabia zpo katika makabila fulani ambazo zipo tu hata kama kuna wachache waliostaribika bado asili inaendelea kuwepo we can't escape nature
 
Sasa si muoe makabila yenu (dada zenu) kwa nini mnatanga tanga???
Kwa sababu kama mtu huwezi kuacha upori pori huwezi kuoa kabila lisilo la kwako kwa kuwa kutakuwa na tofauti tu za kitamaduni ambazo zina affect tabia pia ...hiyo ni piga ua galagaza. Ila kama mambo ya culture ulishatupa kule unaweza oa kabila lolote.

Mi kuna watu wengi nawajua wa makabila tofauti ambao walishaapa hawataoa mke toka kabila lingine...na nawapa BIG UP sana kuliko kujidai ku mix wakati unakataa kukubali tofauti.
:eek2:
 
nyumba kubwa,hebu nifafanulie u-pori pori ni upi ulimaanisha hapo?
 
Last edited by a moderator:
hahaa.! yaani umeshindwa kusema kuwa huo ndo mtizamo wako ukamsingizia mzee wa watu.Wajifanya kuambia watu eti waache hizo fikra na wakati huo huo unatetea hizo fikra unazotaka watu waachane nazo? unachekesha.
 
Machame again? Am proud to be mwanamke wa Kimachame, wachaga maarufu kuliko wote, title tu inadipict kuwa Mmachame ni mwanamke strong, fighter, not ready to be oppresed, beautiful, intelgent and God fearing. Kwa yote hayo najua am marketable ni kiasi cha kuamua cuz pamoja na makelele yote ya kuwasema vibaya we still ROCK kuanzia hapa Jf mpaka mtaani! Wadada wote wa Kimachame hapa Jf thumbs up!! Teh!
 
Back
Top Bottom