Mtangazaji mpira Azam Tv anaboa sana

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,342
4,801
Jamaa maneno meeeengi hata hayahusiani na game yenyewe. Akimtaja mchezaji ataanza kumchambua weeee hadi club alizopita, badala ya kutangaza mpira unaochezwa uwanjani yeye ni ujuaji na story tu. Yaani utafikiri yupo kwenye kipindi cha majadiliano.

Too much boring.

Halafu hata tone/sauti yake haiko kiutangazaji wa soka, utafikiri anaimba shairi
 
Nurdin Seleman
 
Nurdin Seleman ndio mtangazaji bora kabisa kwa taarifa yako, style yake ya utangazaji inatukosha wengi, jana niliposikia anatangaza yeye nikaangalia gemu ya saa 5 azam sports 3, kumbuka mechi zote za afcon naangaliaga Dstv channel 222.Nikimsikia Nurdin nard azam tv.Acha wivu wa kike.
 
Labda kama unashida na tune yake... Lakin ukija upande wa historia hata watangazaji wakubwa huko ulaya wanatabia za kutoa historia za wachezaji na binafsi navutiwa sana na inaonesha kuwa mtangazaji kabla ya Mechi kafanya homework yake vizuri
 
Jamaa maneno meeeengi hata hayahusiani na game yenyewe. Akimtaja mchezaji ataanza kumchambua weeee hadi club alizopita, badala ya kutangaza mpira unaochezwa uwanjani yeye ni ujuaji na story tu. Yaani utafikiri yupo kwenye kipindi cha majadiliano.

Too much boring.

Halafu hata tone/sauti yake haiko kiutangazaji wa soka, utafikiri anaimba shairi
labda useme sauti mbaya,lakini kumtaja mchezaji na kutoa historia yake ndio mtindo wa kisasa wa kutangaza mpira
 
Jamaa maneno meeeengi hata hayahusiani na game yenyewe. Akimtaja mchezaji ataanza kumchambua weeee hadi club alizopita, badala ya kutangaza mpira unaochezwa uwanjani yeye ni ujuaji na story tu. Yaani utafikiri yupo kwenye kipindi cha majadiliano.

Too much boring.

Halafu hata tone/sauti yake haiko kiutangazaji wa soka, utafikiri anaimba shairi
Kwa vile hakumsifia gwede wenu???
 
Kwa vile hakumsifia gwede wenu???
Kama ni wewe nakushauri unapotangaza mpira jaribu kukaza sauti, pia focus kwenye mchezo uwanjani na sio kuanza story za na maneno ya MIPASHO. Jifunze kwa manguli kama Chales Hilary. Pia fuatilia watangazaji wa ligi kubwa kama EPL au Laliga uone wenzako wanapojikita na yanayoendelea kwenye pitch.

Eti mtangazaji unatangaza mpira unaanza kusema " huyu Keita anazuia pale na kumuambia wewe siwezi kukuruhusu kirahisi unipite, kwanza hujui mimi ni kisiki cha mpingo waulize wenzako, mimi nimeaga kwetu na taifa linanitegemea kwahiyo hapa ni ngome ya vifaru na mizinga, huyu keita ni mzaliwa wa .... ni baba wa watoto watatu japo hii ni ndoa yake ya pili, pia kijiji Chao kinaitwa.....alikuwa kwa tabu sana huyu".

Imagine umbea wote huo anaoeleza wakati huo game inaendelea na haizungumzii. Halafu anarudi tena kwa mchezaji mwingine anaitwa labda Koulbaly utasikia " Koulbaly anapiga chenga pale anamuambia beki utanijua mimi ni nani, huyu ni mzaliwa wa kijiji kinachoitwa.... alianza mpira kwa kupelekwa academy na mjomba wake ambaye alikuwa na wanawake wanne"
 
Labda kama unashida na tune yake... Lakin ukija upande wa historia hata watangazaji wakubwa huko ulaya wanatabia za kutoa historia za wachezaji na binafsi navutiwa sana na inaonesha kuwa mtangazaji kabla ya Mechi kafanya homework yake vizuri
Siyo kabla ya mechi ni kwamba wanafuatilia soka haswa, Mimi namkubali sana Nurdin Seleman pamoja na Nazareth Upete wa TBC 1 Hawa wanachambua haswa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom