Mtambo wa kwanza wa umeme wawasili

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Mtambo wa kwanza kati ya ile mitatu iliyoagizwa na serikali kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura umewasili.Mtambo huu unatumia gesi na una uwezo wa kuzalisha megawatts 34.Matarajio ya serikali ni kupata megawatts 100 baada ya kuwasili na kufungwa kwa mitambo yote mitatu.
 
Vipi gas wamekuja nayo au na wao tunawanunulia kama tunavyowanunulia IPTL mafuta ya kuendeshea mitambo yao tunawalipa vilevile gharama ya kuweka mitambo yao kwenye aridhi yetu. Sijajua huu mkataba aliuingia Ngeleja au kalamagi. Jamani kesho ijumaa ni bajeti ya ngeleja.
 
Pia Ngeleja mbona huwa ana jibu moja tu! La megawatts 300 mara megawatts kadha Somangafungu,songo songo! Hanaga kingine cha kujibu!
 
Mtambo wa kwanza kati ya ile mitatu iliyoagizwa na serikali kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura umewasili.Mtambo huu unatumia gesi na una uwezo wa kuzalisha megawatts 34.Matarajio ya serikali ni kupata megawatts 100 baada ya kuwasili na kufungwa kwa mitambo yote mitatu.

Sasa Mbowe alikuwa anataka tume ya nini, wakati mambo yako wazi kabisa, mitambo ndio hiyo!
 
Megawat 100 ndiyo suluhisho la matatizo ya umeme? Kweli jamaa kazi imewashinda, that is the problem we have in tz bookish education tanesco kuna watalamu wa kutosha lakini!!
 
Eer...aam,tupo katika mchakato wa kuunda tume ya kuchunguza hili suala la upatikanaji gesi songo songo na tutafanya upembuzi yakinifu ili ikibidi tuagiza pia mitambo ya kuzalisha gesi ya dharura itakayotumika kuendesha mitambo ya umeme wa dharura!
 
hivi majirani zetu wanafanyaje? Kwanini akina Ngeleja wasidese(wasiige) hapo kenya kama ambavyo walikuwa wanadesa mashuleni huh
 
Si ajabu hati hii mitambo inayoletwa sasa hivi ina ufisadi ndani yake pia maana ufisadi ndiyo mishipa ya damu ya hawa watu! Let us wait and see. vKwa kiasi kikubwa procurements zinazofanywa wakati kuna dharura kama hi ya umeme huwa zina loopeholes nyingi za kufisadi kwa kisingizio cha dharura.
 
Si ajabu hata hii mitambo inayoletwa sasa hivi ina ufisadi ndani yake pia maana ufisadi ndiyo mishipa ya damu ya hawa watu! Let us wait and see. Kwa kiasi kikubwa procurements zinazofanywa wakati kuna dharura kama hi ya umeme huwa zina loopeholes nyingi za kufisadi kwa kisingizio cha dharura.
 
Back
Top Bottom