Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Hii picha ilinisikitisha sana, nimeipiga Juzi tu katika hilo eneo la Makuti (Zimbabwe) ni umbali wa Km 63 kutoka Chirundu border post (Border ya Zambia na Zimbabwe)
Katika hicho kibao Mlima Kilimanjaro unaonyeshwa upo umbali wa 2772km kutoka hapo Makuti, na unaonyeshwa kuwa huo mlima upo Kenya
Nilijiuliza sana, Yaani mpaka wa leo bado Dunia inafahamu Kilimanjaro ipo Kenya?
Kwa kweli sikujisikia Vizuri, nilipofika Harare nilenda moja kwa moja mpaka Umoja House (Ulipo ubalozi wa Tanzania), kwa bahati mbaya sikumkuta Balozi (Hadadi Rajabu), lakini nilikutana na mama Mmoja wa Kizanzibar nae wala hajui kinachoendelea anasema hajawahi kuona hicho kibao, nikamwambia hii ndio picha hebu fatilieni, aliniambia hilo ni jukumu la TANAPA
Nikaaga na kuendelea na Hamsini zangu huku roho ikiniuma sana