Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,748
MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA
YA MABADILIKO YA KATIBA, SHERIA NA. 8 YA 2011
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)
Download nakala ya hotubaMUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA
YA MABADILIKO YA KATIBA, SHERIA NA. 8 YA 2011
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 18 Novemba, 2011 Bunge lako tukufu lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Siku kumi na moja baadaye, yaani tarehe 29 Novemba, 2011, Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha Muswada huo kuwa Sheria kwa mujibu wa ibara ya 97(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, na kanuni ya 92(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007. Kwa mujibu wa kifungu chake cha 1(2), Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 8 ya 2011, ilianza kutumika tarehe 1 Desemba, 2011, yaani siku mbili tu baada ya kupata kibali cha Rais.
Mheshimiwa Spika,
Leo ni siku arobaini na moja tangu Sheria hii ipate kibali cha Mheshimiwa Rais, na siku thelathini na tisa tangu ipate nguvu za kisheria ili ianze kutumika. Tumekutana hapa leo hii ili Bunge lako tukufu lipate fursa nyingine tena ya kuitafakari Sheria hii. Kila mmoja wetu humu ndani, na kila Mtanzania anayefuatilia mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya, anafahamu kwamba tendo la kwanza lililoidhinishwa na Sheria hii, yaani kuteuliwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, halijafanyika hadi sasa. Tumekutana hapa leo hii ili kujadili, na kama Bunge lako tukufu litaridhika, kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 unaopendekezwa na Serikali, na hivyo kumwezesha Mheshimiwa Rais kutenda tendo hilo la kwanza kwa mujibu wa Sheria hii.
MAJADILIANO YA CHADEMA NA RAIS
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 20 Novemba, 2011 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliunda Kamati Maalum ya wajumbe saba iliyopewa jukumu la kuonana na Mheshimiwa Rais kuhusu Sheria hii na mustakbali wa taifa letu. Siku mbili baadae, yaani tarehe 22 Novemba, 2011, ........