Pius Kafefa
Member
- Aug 9, 2011
- 88
- 20
Hebu soma kifungu hiki cha mwishomungu ampe maisha marefu yenye afya...mchango wake kwa maendeleo ya chadema na taifa ni mkubwa sana.
"Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inafarijika kwamba Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge lako tukufu imeridhia na kukubali mapendekezo yote ya Muswada huu na Jedwali la Marekebisho la Serikali. Kwa sababu zote hizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni sio tu inaunga mkono Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011, bali pia inatoa rai kwa waheshimiwa Wabunge wote, bila kujali the narrowness of our political party affiliations, tuungane na Mheshimiwa Rais katika kulipatia taifa letu utaratibu wa kutengeneza Katiba Mpya wenye muafaka wa kitaifa.
Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza, naomba kuunga mkono hoja hii.
---------------------------------------------------------------
Tundu Antiphas Mughwai Lissu (MB)
MSEMAJI, KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
&
WAZIRI KIVULI, KATIBA NA SHERIA
FEBRUARI 9, 2012 "