Msomali

Msomali


Inasemekana katika mataifa barani Afrika yenye wadada wenye ulimbwende wa asili basi mataifa haya matatu; Eritrea, Ethiopia na Somalia, kamwe hayawezi kukosekana katika namba za juu kabisa.


2016, Chuo Kikuu

Nilikwenda pamoja na baadhi ya wenzangu chuoni hapo kutoa mada juu ya soko la ajira kama njia ya kujitoa kwenye chuo kilichotulea wakati tukisoma huko (giving back to your alma mater).

Tulikutana wengi tuliokuwa tumesoma mwaka mmoja na wengine wa miaka ya nyuma na mbele yetu. Ilikuwa siku nzuri sana maana tulikumbushana mambo mengi ya ujana tuliyofanya tukiwa chuoni hapo.

Wengi sasa walikuwa na familia zao – ndiyo, isipokuwa mimi – na wale ambao walibahatika kuwa na wake zao ambao nao tulisoma wote chuo hicho walikuja nao kuturingishia sie. Ilipendeza sana walipokuwa wakiwaambia wanafunzi kuwa wao walikuwa wapenzi miaka kumi na iliyopita na sasa ni familia moja. Waliwatia moyo wanafunzi kuwa kama wanapendana haimaanishi kuwa wakimaliza chuo ndiyo mapenzi yataisha. Niliamua kujiondoa kwenye mjadala huo maana ulinikumbusha machungu tu.

Nilitoka ukumbini na kuanza kutembea bila kuwa na lengo maalum la nilipotaka kwenda isipokuwa tu kwa lisaa limoja lijalo nisiwepo ukumbini kule kwenye mada ya 'ujana na mahusiano'. Nilitakiwa kurudi tena kutoa mada ya 'Morality in the Workplace: How university experience can shape you'.

Nilijikuta nimesimama ghafla baada ya kuisikia sauti, sauti ambayo sikujua kama bado ningeweza kuikumbuka. Nilijua hii sauti nilishawahi kuisikia, miaka mingi iliyopita. Nilitembea kwa kunyata na kuchungulia kuthibitisha sauti ile ilikuwa ya yule niliyemdhania.

Mentor huyu huyu ambaye ndiyo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi pale TIRA? Wewe msomali ulipoteza bahatiee...” ilikuwa sauti ya binti mmoja.

“Ndiyo huyo huyo” ilijibu sauti ile. “Lakini hilo sio la maana.” aliendelea.


2002

“Tulikuwa mwaka wa pili na penzi letu lilikuwa ndiyo kwanza linaanza kuchanua. Nilimpenda Mentor na yeye alionesha kunipenda sana. Alikuwa ni wale wakaka wapole unajua, wao ni kitabu na mpira tu. Hata alivyokuja kunitongoza nilibaki najiuliza alinioneaga wapi?

Basi bwana tukaenda hivyo hivyo hadi hii 2003 wakati tumeenda kwenye mazoezi kwa vitendo (field).

Nikakutana na mkaka ambaye yeye alikuwa anafanya kazi pale. Alikuwa mzuriiii! Basi yeye kila siku anavaa suti tu. Ni wale tunawaita; tall-dark-handsome, halafu anavaa miwani yake full kutabasamu. Halafu hana hata miaka mingi hapo tayari keshapandishwa cheo mara mbili tangu aajiriwe.

Kidogo kidogo akaanza kunizoea, mara akipita kwenye meza yangu aniguse bega, siku nyingine aniletee chocolate, mara biskuti, ali mradi hakosi kitu cha kunishtua kila siku.

Mwanzoni nilikuwa namchukulia poa maana nilikuwa na Mentor lakini kadri siku zilivyoenda nilizidi kumzoea. Alinifanyia mpango hata baada ya kumaliza field niwe naenda kazini kwa masaa machache na ilinisaidia sana kupata uzoefu. Kidogo kidogo hata muda wa kukaa na Mentor ukaanza kupungua maana kule kazi, shule na vimtoko vya kuibia na huyu mpya.

Siku ya siku, bwana yule akanitamkia wazi kuwa ananipenda, anataka kunioa nitakapomaliza tu chuo. Ilibidi nimueleze tu kuwa nina mpenzi mwingine. Akanisisitizia ari yake lakini akanipa wiki moja nimpe jibu.

Nilitaka niwe nao wote maana kila mmoja alikuwa na sifa yake tofauti na mwenzake. Lakini baada ya muda nilikaa nikatafakari nikaona ninachofanya si kizuri, sikulelewa hivyo mimi. Nikatafakari kati ya hawa wawii ni nani nilikuwa nampenda zaidi. Hivyo nikamfuata Mentor nikamueleza kuwa sitaweza kuendelea naye tena kwani nimempata mwanaume mwingine. Nilimuomba msamaha sana maana nilijua nilimuumiza lakini ilibidi nimueleze ukweli.

Ulikuwa ni mwezi mrefu sana kwangu maana ndiyo tulikuwa tumeingia mwaka wa tatu sasa. Mentor kichwani kwake alijua tukimaliza chuo tu ndiyo ndoa. Nakubali nilikuwa nikimpenda Mentor lakini baada ya kukutana na huyu kaka niligundua sikuwa nikimpenda vva kutosha.

Mentor alinisumbua sana akitaka hata nimpeleke kwetu akaongee na wazazi wangu kama shida ni ndoa. Alikuwa tayari kwa lolote maskini kaka wa watu.

Hata hivyo baada ya muda alikubali kushindwa nami nikaanza penzi jipya na huyu mwingine. Maisha yalikuwa nusu mbingu nusu dunia. Alikuwa mtaratibu mno, mcheshi na zaidi alipenda kuzungumzia mambo magumu magumu ya maisha. Alinifanya kila siku nijifunze jambo jipya niangalie habari kiasi kwamba hata masomo yangu yalipanda maana nilikuwa ninasoma mambo hayohayo.

Wakati nikimalizia mwaka wangu wa mwisho nilipata fursa ya kuomba kwenda kufanya kazi makao makuu ya Umoja wa Mataifa maana tukiwa chuo nilikuwa mhudhuriaji mkubwa wa makongamano na miradi yao. Hiyo nafasi hiyo ilipojitokeza wale wawezeshaji (facilitators) wa upande wa Tanzania walinihimiza kuiomba nafasi hiyo na walinithibitishia wataongeza neno lao na nitapata nafasi hiyo.

Ilikuwa kazi ya muda/mkataba wa miaka mitatu tu lakini niliiona kuwa ni fursa nzuri sana. Nilimueleza mpenzi wangu na alifurahi sana. Aliahidi kunisaidia katika mchakato mzima.

Huku shule ikielekea ukingoni, nami nilikuwa namalizia viambatanisho vya mwisho vya maombi yangu. Kama sio yeye sidhani kama ningemaliza maana mambo yalikuwa mengi mno.

Siku moja nikiwa natoka darasani, miezi miwili kabla ya kufanya mitihani ya mwisho, nilisikia kichefuchefu ghafla na nilitapika. Wala bila kuuliza nilielekea duka la dawa na kununua vihusika na kama ilivyokuwa nilikuwa na ujauzito.

Nilipata mawazo mengi; shule, kazi, nyumbani. Mambo haya yalinipa msongo wa mawazo maana kiukweli sikutarajia kupata ujauzito wakati huu. Nilitaka nami nijifungue ndani ya ndoa. Katika msongo wote huo wa mawazo kitu pekee kilichonipa tabasamu ni kumfikiria baba mtoto maana siku zote alikuwa akinitania, “Yani mtoto wetu atatoka mzuri balaa kama shombe wa Kisomali!

Nilitabasamu maana nilimuona anavyofurahia kumuona mwanetu. Nilisahau hata nitawaelezaje wazazi na ndugu zangu maana Msomali mimi ndiyo nilikuwa mfano wa ndugu na wadogo zangu. Kila kitu kizuri lazima Msomali nitajwe kama mfano wa kuigwa. Nilisahau kazi ambayo niliiomba na itakuwaje kwenda huko na ujauzito. Nilisahau yote hayo, nilitoka chooni nikiwa na tabasamu kama vile nimeambiwa Yanga na Chelsea wameshinda ligi! Hahah

Nilichukua simu na kumpigia ili kumtaka kuongea naye baadaye jioni. Alikubali na kama tulivyoongea jioni alikuja na maua mazuri ambayo alinikabidhi, bado nilikuwa nikitabasamu.

Nilimueleza kuhusu ujauzito wangu na hapo ndipo nilipona maajabu. “Hapana Msomali! Siko tayari na kulea mtoto kwa sasa..hapana! Ulipataje sasa na wewe ulisema ulikuwa siku salama? Hapana msomali.

Hata nilipojaribu kuomba msaada kupitia rafiki zake na baadhi ya ndugu alinitukana, alinisema vibaya. Alionesha dhahiri hataki kusikia juu ya mimba wala mtoto.

Kwa jioni ile aliondoka bila kusema zaidi ya hapo na nilijifariji kuwa huenda ni ule mshituko wa kuwa baba. Niliamua kumpa muda ajitafakari na baadaye atatulia.

Hali haikuwa kama nilivyotarajia maana kadri siku zilivyoenda ndivyo alivyozidi kuwa mkali. Alifikia hadi hatua ya kuniambia niitoe mimba. Niliumia sana. “Mimba au mimi”, ndiyo zilikuwa chaguzi zangu.

Kumbe wakati mimi naandika maombi yangu ya kwenda kufanya kazi naye alikuwa anafanya maombi ya kwenda shule nchi ile ile ambayo nami nilikuwa naenda kufanya kazi. Kwa bahati nzuri yeye alikuwa ameshapata na majibu kuwa amekubaliwa na angeondoka mwezi Novemba mwaka huo. Alikuwa ameiweka kama siri ili aje kuniambia baadaye. Sikuwa nimefahamu hadi siku moja kabla hajaondoka ambapo alinipigia kuniambia kuwa anaondoka kesho yake.

Lengo hasa la simu yake halikuwa kuniaga ila kisingizio kutaka kujua kama niliitoa mimba ile au la maana tangu aniache siku ile hatukuwa tumeonana tena.

Nilimaliza chuo huku nikitafakari sana kuitoa mimba ile lakini nashukuru Mungu nilipata rafiki wazuri walionishawishi kutoitoa mimba ile. Siwezi kuelezea yote waliyoniambia ila somo liliniingia nikaamua nirudi nyumbani kwa wazazi wangu niwaeleze lililotokea. Kinyume na matarajio yangu, nyumbani walinipokea vizuri sana tena wazazi na ndugu waliojua mkasa ule walinionea huruma sana. Niliendelea kubaki nyumbani hadi Novemba hiyo aliyonipigia simu.

Baada ya kukata simu yake ndipo nami nikakumbuka maombi yangu niliyoyatuma. Nilifahamu kuwa kwa taratibu za huko hata kama mtu umekosa nafasi ni lazima wakuambie. Hivyo niliingia kwa mategemeo ya kukuta barua pepe yenye kunijulisha nimekosa. Sikuwa nimeingia tena huko tangu jioni ile nilipoachwa maana pia vitu vingi alikuwa akivifanya yeye. Alikuwa na nywila yangu.

Niliangalia barua pepe zote mpya na sikuona yoyote ya kuhusu hilo hadi nilipoangalia vyema na kukuta moja ambayo ilikwishafunguliwa kumaanisha aliiona na hakuniambia. Ilikuwa ikihitaji mimi kuongeza 'referee' mmoja zaidi maana nilikuwa nimeandika wawili tu. Niliumia sana kwamba hakuniambia na hata nilipoenda kwenye 'portal' yao hakuwa ameongeza chochote. Kigezo hicho kimoja, kikawa kimenikosesha kazi, niko nyumbani na ujauzito na siwezi kwenda kuomba kazi mahali kwa hali ile. Nahisi nilikuwa na miezi sita hivi.

Maisha yalienda kama kawaida, nikajifungua vyema mtoto wa kike ambaye nashukuru Mungu alifanana na mimi karibia kila kitu. Sasa yeye ndo alikuwa shombeshombe, msomali, wa ukweli. Nilitamani nimueleze baba yake lakini nilijizuia maana hakutaka kujua chochote kuhusu mwanaye.

Nakumbuka wakati mmoja kabla hajarudi nilijikuta tu nikimtumia picha za mwanaye, walau amuone tu. Nahisi aliona nataka kumuomba pesa au kurudisha mahusiano hivyo aliipuuzia barua ile.

Baada ya muda moyo ulianza kupoa hasa baada ya hasira za kutelekezewa mtoto na hisia za mapenzi kwake kuisha.

Nilianza zangu kazi miezi sita tu baada ya kujifungua na maisha yamekuwa yakiendelea kama kawaida. Sasa hivi nimeolewa na mume wangu tunaishi vyema kabisa na wala sifahamu huyo jamaa yuko wapi.” alimalizia kusimuliza Msomali.

Niligeuka na kuendelea kunyata kurudi ukumbini maana niliyoyasikia yalitosha, yalitosha kunikumbusha miaka zaidi ya kumi iliyopita ambapo nilimpoteza binti niliyempenda. Niliiangalia saa yangu na kugundua nimebakiza dakika kumi kabla muda wangu ufike wa kutoa mada yangu. Niliamua kujikaza kutokukuonesha hisia zozote maana kwa vyovyote vile, lazima maisha yaendelee...


Wasalaam wapendwa,
Mentor.
asante mkuu [HASHTAG]#mentor[/HASHTAG] nzuri, ndefu inayo elimisha.
 
Najua umependa hapa tu...


"Baby Pana
They say you like cassava
I get big cassava
Baby Pana"

Hhahahahahahahahahahhahahahahaaaaaa weewee umeanza kupuliza tena msuba eeehh hhahahahahahhaaa

Umejuaje Kasie mie napendaga hapo tuu, yaani nimeweka repeat all day long nasikiliza baby PANA..... huyu dogo Tekno kanihorojesha Kasie mie na hapa week end mode ndo ishakuwa activated kifuatacho ITV ni ........................... muzikiiiiiiiiii hahahahahahahahhahahaaaaa
 
K

Ila Mentor wewe si Chelsea?Au nimepoteza kumbukumbu?

Weekend njema.

Mimi ni chelsea ila wapenzi wa Pogba wakiucheza huu wimbo utapendeza sana!

UJUMBE: Upinzani si uadui...


Woga tu wa maisha Kiongozi. Mi wangu wa ujanani wala sikumkataa, na niko naye bega kwa bega mpaka leo hii. Yuko Form 4 (boarding) mwaka huu, na she id doing the best katika darasa lake. Nilimwambia niliyekuja kumuoa kuwa, huyu ni wakwetu, akalitambua hilo. Na ssa maisha yansonga.


Man I wish vijana wote tungesoma hapa. Kutelekeza mtoto ni bonge la laana aisee. Kudos bro.


Arsenal oyee. Kesho ushindi mwingine si chini ya goli 3.

Mkuu msijiamini sana...kuna-uchovu!


sijasoma hata

Heee kisa nini tena mamii!??
 
Mimi ni chelsea ila wapenzi wa Pogba wakiucheza huu wimbo utapendeza sana!

UJUMBE: Upinzani si uadui...





Man I wish vijana wote tungesoma hapa. Kutelekeza mtoto ni bonge la laana aisee. Kudos bro.




Mkuu msijiamini sana...kuna-uchovu!




Heee kisa nini tena mamii!??
nimechoka
 
Basi mi nlitamani iendelee sasa upande wa Mentor sasa ha ha haaaa kumbe sterling Msomali kafia kwenye majani!!
Ni story nzuri sana by the way..too realistic
 
Basi mi nlitamani iendelee sasa upande wa Mentor sasa ha ha haaaa kumbe sterling Msomali kafia kwenye majani!!
Ni story nzuri sana by the way..too realistic


Ulitaka kufahamu nini kuhusu Mentor mwana wa majanga?
 
Back
Top Bottom