Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

Zitto hana jipya na hii ni political game wanataka wapite uchaguzi kilain na zitto analiongelea kana kwamba halengi uchaguzi huu mkuu but anajua UKAWA ni kikwazo

Kuna mdau kasema hapo juu kuwa zito ni kama picha tu, haina madhara. Halafu sijui ataenda lini kwa wafadhili wake ccm maana ameng'ang'ania chadema hataki hata kutoka?
 
Zitto ni idiot mwingine ktk hii dunia, unafiki unamuendesha vibaya mpaka anashindwa kujicontrol na uwongo wake.
Anasema hauamini ukawa kwa jinsi walivyoungana ila anatafurahi ikiwa hivyo.
DuuuH!!
Kwahiyo yeye ni CCM au ndiyo anavyojiweka hivyo 50-50.
Ushauri kwa Zitto ni hivi: jitambulishe huko CCM jumla usanii wa kizamani haulipi leo
 
Last edited by a moderator:
na mtaumwa sana ugonjwa uitwao Zittophobiasis. Ukweli ni kwamba Zitto yuko very smart. ndo maana kila siku mko bize humu kumtaja mara kumi kumi kuliko mnavyowataja waume zenu au wake.
Hoja ya Zitto iko very clear hapo ni kwamba anataka katiba ya Warioba ndo ijadiliwe ndo maana anabainisha wazi kuwa hataingia bungeni kama katiba ya lumumba itaendelea kujadiliwa. na mtahangaika sana mataahita nyie.
ZZK hana msimamo kabisa.Ni mnafiki mkubwa.Lumumba Endeleeni kumpamba
 
Zitto ana akili kuliko machadema wote.

Yeah,ikiwa akili ni kusaliti unachoamini basi ZITO ANAZO.

Pia hoja ya fedha kununu dawa nk si hicho ndicho kilichompeleka upinzani? Zito anapolaumiwa kudidimiza ushindani kwa kubank ktk influence aliyojengewa na WTNIA DHAMIRI YAKE I HAI TENA?.
Tupate katiba sasa ndo kinga pekee ya uwajibikaji na mf ni KENYA.
 
zito amethubutu sana kusema,
kiukweli bunge la katiba ni janga la taifa na mamilion yanayopotezwa hapo kwa kuskiliza aina za matusi ni matusi kwa mlipa kodi na mtanzania wa kawaida
 
KIKWETE Na MAKAMBA Wamekuharibu Sana Wewe Dogo. Ukiona Mwanasiasa Yeyote Anasema NIMEFANYA BADALA YA TUMEFANYA Moja Kwa Moja Huyo Ana UBINAFSI NDANI YAKE. ZITO WEWE NI MBINAFSI.
NO CORRUPTION NO CCM
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika.

Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika.

Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.

Zitto alitoa kauli hiyo jana, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.

Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.

Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.

Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.

“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.

Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana.

“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.

“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.

… mchakato wa Katiba Mpya usitishwe

Akitolea ufafanuzi hoja yake ya kusitisha mchakato wa Katiba Mpya, Zitto alisema ni vyema serikali ikausitisha ili kunusuru fedha za umma zisiteketee.

Alisema fedha hizo zinastahili kutumika kununua madawa, kuendeleza miradi ya maji na kusomesha Watanzania, hivyo hakuna sababu fedha hizo kutumika kwa ajili ya kupiga porojo na kutukanana ndani ya Bunge.

“Nashauri tuahirishe mchakato huu mpaka baada ya uchaguzi mkuu mwaka kesho, ndipo hapo tuwe na mamlaka ya kujadili mchakato huu na kumaliza.

“Pia uchaguzi unaweza kuchekecha na ukaondoa baadhi ya watu ambao ni vikwazo katika mchakato kwa sababu uchaguzi hauna muamala, mtu ambaye alikuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema.

Aidha, alisema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Katiba ya sasa inatakiwa kurekebishwa baadhi ya maeneo ambayo ni vikwazo, kama vile Tume huru ya uchaguzi, kipengele cha wagombea binafsi kiwekwe na maeneo ambayo Zanzibar wamekuwa wakiyahitaji katika Katiba mpya, kwa mfano suala la mafuta na gesi yawekwe.

Alisema hakuna sababu ya kugawa nchi na kutumia rasilimali zilizopo kwa kufanya kazi ambayo haina matunda.

…amtetea January

Katika hatua nyingine, Zitto, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema amesikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwa Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba, baada ya kutangaza nia ya kuwani urais mwaka 2015.

Alisema kila kijana anapojitokeza kwa ajili ya kutaka kushiriki katika mamlaka za nchi, hasa katika nafasi kama hiyo ya urais, kumekuwa na mashambulizi makubwa dhidi yake.

“Ni hatua ambayo sio nzuri kwa sababu kwa mujibu wa takwimu, idadi ya watu asilimia 72 wapo chini ya miaka 30, asilimia 65 ya wapiga kura ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40, hivyo vijana wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi, tufahamu changamoto za maendeleo ya nchi yetu zinahitaji uongozi mpya wa kizazi kipya.

“Ni dhahiri neno ujana si sifa, lakini neno uzee pia si sifa, hivyo tunatakiwa kuwapima vijana kwa sifa zilizopo, kama vile za kikatiba na zile za ziada, badala ya kusema vijana hawajakomaa… nilisikitika sana na mashambulizi ambayo yalielekezwa dhidi ya Makamba, natoa wito kwamba tuache, kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi.

“Mtu akigombea na kama akitoa sera zake vizuri wananchi wakamwelewa, akichaguliwa ni wananchi wameamua, hakuna mtu mwenye mamlaka kuwa fulani ni kijana, nadhani lazima tubadilishe uongozi na watu wajue nchi hii ni ya vijana, hatusemi wazee hawawezi ila wao wabaki kuwa washauri kama wao walivyokuwa vijana katika kipindi cha Nyerere nao walikuwa na miaka 40. Hivyo kuna haja ya kuweza kufikia hapo, changamoto za nchi ni kubwa, kuna haja ya aina mpya ya uongozi na mimi naamini aina hiyo itatoka kwa viongozi vijana,” alisema.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zitto, ambaye yuko ndani ya Chadema kwa sababu za kisheria, kuibuka na kuuzungumzia Ukawa.
Mwanasiasa huyo kijana amekuwa kimya kwa muda mrefu, hata kwenye harakati za Ukawa amekuwa aghalabu kuonekana, hali ambayo imekuwa ikiibua maswali yuko upande gani katika mchakato huu wa Katiba Mpya.

Kauli hii ya Zitto inaweza kuibua fikra mpya kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa na imani kubwa na umoja huo unaoviunganisha baadhi ya vyama vya siasa nchini.

Makamba aufananisha na Paka

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ameufananisha Ukawa kuwa ni sawa na paka, kwa kuwa tambo za wajumbe wa kundi hilo zitakwisha mwaka 2015 katika kuusaka urais.

Makamba alitoa kauli hiyo alipozungumza na MTANZANIA Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Alisema Ukawa ni umoja ulioundwa kwa lengo la kuwahadaa wananchi katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya, lakini hautakuwapo mwaka 2015.

“Mimi ni mwana CCM, nasema kwa hali hii tutawachapa kweli wapinzani katika uchaguzi ujao… kwa sababu huu Ukawa ni umoja wa paka, paka walikaa siku moja wakasema jamani tuungane, wakachukua kamba wakajifunga mikia ili wawe wamoja, lakini alipotokea panya wote walisambaratika, kwa sababu kila mmoja alikuwa anamtaka panya.

“Kwa kuwa kila chama kinataka kuwa na rais, nina hakika huu muungano wao hautaendelea, watasambaratika kama walivyosambaratika paka. Wakati wa urais hakuna Ukawa!” alisema.

Alisema hata Ukawa wasiporudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya, Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba iliyopo.

“Nakumbuka vyama vya upinzani wakati mimi nikiwa Katibu Mkuu moja ya hoja walizokuwa waking’ang’ania ni Katiba Mpya na Dk. Slaa alikuwa akiwaahidi Watanzania kuwa wakimpatia nchi atawapatia Katiba Mpya… sasa Rais Kikwete amesema uchaguzi ujao ufanyike na Katiba Mpya, kwanini wanatoka Bungeni? Mnataka nini? Rudini Katiba ipatikane kama kweli mna nia ya dhati!

“Usilalamikie wingi wa CCM kwa sababu ndio uzuri wa kushinda. Hata wao wangekuwa wengi wangefanya hivi ili sera za chama zipite, warudi bungeni katiba mpya ipatikane. Wasikimbie hoja,” alisema.

Aidha alizungumzia mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa ndani ya rasimu ya pili ya Katiba na kusema huo ni mzigo kwa Watanzania.

SOURCE: MTANZANIA

Mimi kwa maoni yangu namuunga zitto mkono kwamba ni vigumu upinzani kuungana kwa sababu zitto yeye mwenyewe ni mpinzani dhidi ya vyama vya upinzani. yeye ndio bingwa wa mipango hii yote wakisaidiana na ccm na ACT yake. eti anataka Lowasa akiwa rais ampe uwaziri mkuu. kwa hiyo tusishangae anachokisema zitto kwa sababu yeye zitto+mwigamba+kitila mkumbo wameanzisha mradi wa kuhakikisha upinzania kaukuwi tanzania.

Vile vile kwenye swala la rushwa zitto hana maadili kuzungumzia vita ya rushwa na ufisadi maana na yeye ameishaanza harakati za kukuza rushwa. wale madiwani wa shinyanga wanaoomba kurudi chadema wamesema zitto anashirikiana na wana ccm kama nchemba+ridhiwani,nape,masele kuhonga madiwani ili waondoke chadema. zitto huna credibility ya kupambana na rushwa.

Zitto nae ni mpinzani?
 
Nakubaliana na Zitto katika swala la kuvunja bunge rasmi ikiwa hawatafikia muafaka wa kurudi Bungeni kwa sababu wote UKAWA na CCM hawana sababu kabisa ya kujadili swala ambalo wananchi hawakuliomba. hakuna mahala popote ktk report ya tume wala rasimu ya Katiba, wananchi wamesema tunataka - SHIRIKISHO hivyo ubishano juu ya serikali ngapi ni ubishani wa kisiasa zaidi ya ukweli uliopo kwa sababu wote hawazingatii UBOVU wa Utawala na uongozi zenyewe. Kila mmoja wao ana hofu ya mwenzake ndiyo imepelekea kuvunjika kwa bunge maalum la katiba. Ni interest za vyama hivyo hata kuundwa kwa UKAWA ni umoja dhidi ya CCM ambayo sio hoja ya wananchi wala katiba mpya.

Swala la Ujana hapo ZZK anapotosha kwa sababu Vijana wengi nchini kwa asilimia 50 wapo chini ya umri wa miaka 18, Je inahalalisha kuwapa uongozi watoto wadogo kwa sababu wao ni wengi? na hata ukitazama Mpira mchezo huo unachezwa na vijana wa umri usiozidi 30. Je ni kwa kufuata mfano huo rais wa FIFA lazima awe kijana? Nafikiri zipo sifa za ujana ambazo wangeweza kuzitumia badala ya wingi kwa sababu hawa vijana bado wapo ktk learning process ya maisha yao hali rais ni kiongozi ambaye anayetakiwa kutoa maamuzi magumu (decision making), huko chini wapo watu wanaomaliza madogo madogo.

Vijana wengi toka miaka 18 hadi 40 wanashindwa hata kujiingia katika maswala ya ndoa kwa kuchelea commitments zake na Urais sii kwenda beach bali ni mamlaka makubwa sana ambayo mgombea yeyote awe kijana au mzee lazima awe na sifa zinazostahiki. Hivyo tunaweza kukubaliana kuwaingiza vijana lakini sio kwa sifa za wingi wao ama wapiga kura wengi kwa sababu sidhani kama kuna takwimu zinazoonyesha vijana wa miaka 18 hadi 39 ndio wanataka kiongozi bora zaidi ya wazee ama kijana ana uzalendo, uwajibikaji, uaminifu, na uwazi zadi ya mzee. Tuwe waangalifu sana ktk maswala ya tofauti zetu hasa pale tunapotaka kuujenga UTAIFA wetu.

Siafikiani na sheria ya rais lazima awe na umri zaidi ya miaka 40 lakini pia siafikiani na mengi ikiwa ni pamoja na umri wa kupiga kura. lakini siwezi kujenga sababu za jumla (generalisation) ikiwa zipo sababu za udhaifu wa vijana kiumri (hekima na busara) katika maamuzi yao hasa pale maisha ya watu wengine yanahusika. Ni facts ambazo tunaona vijana wanavyoshindwa kabisa kuhimili vishindo vya kisiasa.

Kiambatanisho:- According to research, although the brain slows down with age, this simply helpes older men and women develop greater insight.The reason for this is that, unlike the young, the elderly's brains are not ruled by the chemicals that fuel emotion and impulse. So their slower responses really are more thoughtful and 'wiser'.
These showed that what older people lose in reaction times, they make up for in better decision-making.

Professor Dilip Jeste, from the University of California at San Diego, said older people were less affected by dopamine, which helps signals pass between neurons and is involved in the reward system of the brain.
'The fact that older people are slower to respond than younger people is widely seen as a disadvantage. But that's not always the case. The elderly brain is less dopamine- dependent, making people less impulsive and controlled by emotion.

Read more: With age really DOES come wisdom, say scientists | Mail Online
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika.

Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika.

Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.

Zitto alitoa kauli hiyo jana, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.

Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.

Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.

Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.

“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.

Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana.

“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.

“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.

… mchakato wa Katiba Mpya usitishwe

Akitolea ufafanuzi hoja yake ya kusitisha mchakato wa Katiba Mpya, Zitto alisema ni vyema serikali ikausitisha ili kunusuru fedha za umma zisiteketee.

Alisema fedha hizo zinastahili kutumika kununua madawa, kuendeleza miradi ya maji na kusomesha Watanzania, hivyo hakuna sababu fedha hizo kutumika kwa ajili ya kupiga porojo na kutukanana ndani ya Bunge.

“Nashauri tuahirishe mchakato huu mpaka baada ya uchaguzi mkuu mwaka kesho, ndipo hapo tuwe na mamlaka ya kujadili mchakato huu na kumaliza.

“Pia uchaguzi unaweza kuchekecha na ukaondoa baadhi ya watu ambao ni vikwazo katika mchakato kwa sababu uchaguzi hauna muamala, mtu ambaye alikuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema.

Aidha, alisema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Katiba ya sasa inatakiwa kurekebishwa baadhi ya maeneo ambayo ni vikwazo, kama vile Tume huru ya uchaguzi, kipengele cha wagombea binafsi kiwekwe na maeneo ambayo Zanzibar wamekuwa wakiyahitaji katika Katiba mpya, kwa mfano suala la mafuta na gesi yawekwe.

Alisema hakuna sababu ya kugawa nchi na kutumia rasilimali zilizopo kwa kufanya kazi ambayo haina matunda.

…amtetea January

Katika hatua nyingine, Zitto, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema amesikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwa Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba, baada ya kutangaza nia ya kuwani urais mwaka 2015.

Alisema kila kijana anapojitokeza kwa ajili ya kutaka kushiriki katika mamlaka za nchi, hasa katika nafasi kama hiyo ya urais, kumekuwa na mashambulizi makubwa dhidi yake.

“Ni hatua ambayo sio nzuri kwa sababu kwa mujibu wa takwimu, idadi ya watu asilimia 72 wapo chini ya miaka 30, asilimia 65 ya wapiga kura ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40, hivyo vijana wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi, tufahamu changamoto za maendeleo ya nchi yetu zinahitaji uongozi mpya wa kizazi kipya.

“Ni dhahiri neno ujana si sifa, lakini neno uzee pia si sifa, hivyo tunatakiwa kuwapima vijana kwa sifa zilizopo, kama vile za kikatiba na zile za ziada, badala ya kusema vijana hawajakomaa… nilisikitika sana na mashambulizi ambayo yalielekezwa dhidi ya Makamba, natoa wito kwamba tuache, kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi.

“Mtu akigombea na kama akitoa sera zake vizuri wananchi wakamwelewa, akichaguliwa ni wananchi wameamua, hakuna mtu mwenye mamlaka kuwa fulani ni kijana, nadhani lazima tubadilishe uongozi na watu wajue nchi hii ni ya vijana, hatusemi wazee hawawezi ila wao wabaki kuwa washauri kama wao walivyokuwa vijana katika kipindi cha Nyerere nao walikuwa na miaka 40. Hivyo kuna haja ya kuweza kufikia hapo, changamoto za nchi ni kubwa, kuna haja ya aina mpya ya uongozi na mimi naamini aina hiyo itatoka kwa viongozi vijana,” alisema.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zitto, ambaye yuko ndani ya Chadema kwa sababu za kisheria, kuibuka na kuuzungumzia Ukawa.
Mwanasiasa huyo kijana amekuwa kimya kwa muda mrefu, hata kwenye harakati za Ukawa amekuwa aghalabu kuonekana, hali ambayo imekuwa ikiibua maswali yuko upande gani katika mchakato huu wa Katiba Mpya.

Kauli hii ya Zitto inaweza kuibua fikra mpya kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa na imani kubwa na umoja huo unaoviunganisha baadhi ya vyama vya siasa nchini.

Makamba aufananisha na Paka

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ameufananisha Ukawa kuwa ni sawa na paka, kwa kuwa tambo za wajumbe wa kundi hilo zitakwisha mwaka 2015 katika kuusaka urais.

Makamba alitoa kauli hiyo alipozungumza na MTANZANIA Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Alisema Ukawa ni umoja ulioundwa kwa lengo la kuwahadaa wananchi katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya, lakini hautakuwapo mwaka 2015.

“Mimi ni mwana CCM, nasema kwa hali hii tutawachapa kweli wapinzani katika uchaguzi ujao… kwa sababu huu Ukawa ni umoja wa paka, paka walikaa siku moja wakasema jamani tuungane, wakachukua kamba wakajifunga mikia ili wawe wamoja, lakini alipotokea panya wote walisambaratika, kwa sababu kila mmoja alikuwa anamtaka panya.

“Kwa kuwa kila chama kinataka kuwa na rais, nina hakika huu muungano wao hautaendelea, watasambaratika kama walivyosambaratika paka. Wakati wa urais hakuna Ukawa!” alisema.

Alisema hata Ukawa wasiporudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya, Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba iliyopo.

“Nakumbuka vyama vya upinzani wakati mimi nikiwa Katibu Mkuu moja ya hoja walizokuwa waking’ang’ania ni Katiba Mpya na Dk. Slaa alikuwa akiwaahidi Watanzania kuwa wakimpatia nchi atawapatia Katiba Mpya… sasa Rais Kikwete amesema uchaguzi ujao ufanyike na Katiba Mpya, kwanini wanatoka Bungeni? Mnataka nini? Rudini Katiba ipatikane kama kweli mna nia ya dhati!

“Usilalamikie wingi wa CCM kwa sababu ndio uzuri wa kushinda. Hata wao wangekuwa wengi wangefanya hivi ili sera za chama zipite, warudi bungeni katiba mpya ipatikane. Wasikimbie hoja,” alisema.

Aidha alizungumzia mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa ndani ya rasimu ya pili ya Katiba na kusema huo ni mzigo kwa Watanzania.

SOURCE: MTANZANIA

Mimi kwa maoni yangu namuunga zitto mkono kwamba ni vigumu upinzani kuungana kwa sababu zitto yeye mwenyewe ni mpinzani dhidi ya vyama vya upinzani. yeye ndio bingwa wa mipango hii yote wakisaidiana na ccm na ACT yake. eti anataka Lowasa akiwa rais ampe uwaziri mkuu. kwa hiyo tusishangae anachokisema zitto kwa sababu yeye zitto+mwigamba+kitila mkumbo wameanzisha mradi wa kuhakikisha upinzania kaukuwi tanzania.

Vile vile kwenye swala la rushwa zitto hana maadili kuzungumzia vita ya rushwa na ufisadi maana na yeye ameishaanza harakati za kukuza rushwa. wale madiwani wa shinyanga wanaoomba kurudi chadema wamesema zitto anashirikiana na wana ccm kama nchemba+ridhiwani,nape,masele kuhonga madiwani ili waondoke chadema. zitto huna credibility ya kupambana na rushwa.

Kwa vyovyote vile Zitto ni tofauti sana na Hamad Rashid, Zitto amesema kweli kwamba bungeni kwa sasa ni porojo tu hakuna katiba lakini pia hajaonyeshwa kuchukizwa na UKAWA ila alichokuwa anaomba ni kwamba umoja wa ukawa udumu, angeulizwa Hamad Rashid kwanza angewatukana UKAWA alafu angewataka ukawa warudi kujadili rasimu ya CCM ya Serikali 2.,
 
Zitto Ni vigumu kuamini kwamba hafahamu kuwa kinachojadiliwa bungeni ni kitu mchepuko badala ya rasimu ya katiba iliyoratibiwa kitaalamu.

Siamini haoni kwamba bunge hilo linalengo la kupitisha katiba ya ccm kwa kigezo cha wingi wao.

Inashangaza hatoi tamko kuhusu mwenendo wa bunge hilo kwamba hakuna democrasia wala ustaarabu wa kawaida.

Inaonekana ajabu haja comment uharabu wa kikwete alioufanya wa kuasisi uharamia katika matengenezo ya katiba mpya ya wananchi.

Ni mtu wa ajabu asiyeona unyanyasaji na hila zinazofanywa na ccm katika bunge hilo.

La ajabu, anaongea unafiki bila kugusia hoja za ukawa as if hafahamu kwamba wanahitaji kujadili rasimu ya tume na si ya ccm. Mbona hilo halisemi?

Wanafiki na wenye hile mwisho wao ni fedheha.
Umesoma alichosema Zitto kuhusu bunge la katiba kweli wewe! Mi naona umekurupuka kijibu tu, heburudia tena ukiwa huru kabisa kiakili.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
ZZK hana msimamo kabisa.Ni mnafiki mkubwa.Lumumba Endeleeni kumpamba

Tatizo la Zitto ni kutokuwa na msimamo unaojitegemea na hajiamini. Ni kiongozi anaebadilika badilika kwa kupima upepo unamwendeaje. Ni kiongozi anaefanyia kazi matukio ambayo tayari yameshaleta madhara kwake au kwa jamii. Angeonyesha msimamo wake mapema kama alivyofanya sasa asingeandikwa au kutangazwa vibaya kama ilivyokwisha tokea.Ukimya wake alikuwa anapima upepo kisiasa unamwendeaje na huo ni udhaifu.Nakubaliana nae kuwa rasimu ya wananchi ndio ijadiliwe bunge la katiba. Pia kama hautapatikana muafaka na ukawa si tu hatahudhuria vikao hivyo bali bunge liahirishwe hadi baada ya uchaguzi mkuu huku muafaka ukiendelea kutafutwa.
 
..mbona naona kama Zitto yuko kivyake-vyake?

..hata anapotaja Ukawa anawataja kama "wale" na siyo "sisi."

..kwa mfano anasema "viongozi wa Bunge la Katiba wanawabeza Ukawa..." badala ya kusema "viongozi wa Bunge la Katiba wanatubeza sisi tulioko Ukawa..."

..sasa hii inatoka kwenye written statement ya Zitto ambapo alikuwa na muda wa kutafakari maana ya kile alichoandika.

..pia Ukawa wamefanya mikutano kadhaa mikoani na sidhani kama Zitto amewahi kushiriki mkutano wowote ule.

cc Ndibalema, Haki sawa

sikuelewa kumbe ukawa siyo ideology na mawazo sawa, ila lazima uwe front kwenye mikutano n.k

pooooa
 
Back
Top Bottom