Msimamo wa Mtaka wawakuna CCM,CHADEMA

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amewakosoa viongozi ambao wamekuwa na hulka ya kuwaweka rumande watumishi umma na wanasiasa akisema, “Katika mkoa wangu hutoona huo upuuzi.”

Katika msimamo huo ambao umeungwa mkono na viongozi wa CCM, Chadema na wanaharakati, Mtaka amesema kuwaweka rumande viongozi hao si njia sahihi ya kutatua matatizo yanayowazunguka wananchi huku akitaka mamlaka za kinidhamu ziheshimike na kuzingatiwa na si vinginevyo.

Mtaka ametoa kauli hiyo kipindi ambacho wimbi la wakuu wa wilaya (ma-DC) kuwaweka rumande watumishi wa umma walio chini yao, wabunge na madiwani kwa tuhuma mbalimbali likikithiri.

Kwa kauli hiyo, Mtaka anaungana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na aliyekuwa waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kukemea matumizi mabaya ya amri hiyo.

Kauli ya karibuni zaidi imetoka kwa Waziri Jafo ambaye akizungumza na wakuu wapya wa wilaya jijini Dodoma alisema tabia hiyo inasababisha wananchi kuichukia Serikali na kuwaagiza waitumie ilivyokusudiwa na si kuonea watu, akiwataka kuzisoma sheria zinazowaongoza ili wafanye kazi kwa weledi.

Mei mwaka jana, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua katika utendaji wao zinafuata sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa umma.

Aidha, Septemba 25 mwaka jana, Waziri Ummy akizindua majengo ya wodi ya wazazi na matibabu ya dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, alikemea wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makosa ya kitaaluma.

Mwishoni mwa wiki, Mtaka akifunga semina ya madakatari wa mikoa, wilaya na wadau wa sekta ya afya iliyofanyika jijini Dodoma, aliwataka viongozi kuwalinda watumishi wa ngazi ya chini na kubainisha kwamba Simiyu hakuna suala la mtumishi kupelekwa rumande.

“Sisi ambao ni viongozi katika sekta hii, kwanza tuwalinde watumishi wetu, mimi nilipokwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu niliwaambia ma DC, moja ya jambo ambalo sitaki kulisikia ni mtumishi yeyote wa umma kuwekwa lokapu,” alisema.

Huku akishangiliwa na watumishi hao wa sekta ya afya, Mtaka alihoji, “Huyo anayemweka ndani mwenzake, ikitokea kinyume chake angefurahia suala hilo?”

Alisema hakuna aliyezaliwa anajua na kama kuna kiongozi anaona mtumishi mwenzake hajui ni wajibu wake kumpa mafunzo na si kumchukulia hatua za kumweka ndani.

“Wakati mwingine ukiona matamko ya wanasiasa kule kwenye maeneo yenu ya kazi unajiuliza hivi huwa anakaa kushauri haya yatokee, nazungumza ‘with prestige’ (kwa ufahari) kwa sababu katika mkoa wangu hutoona huo upuuzi,” alisema Mtaka.

Akifafanua kauli hiyo jana alipozungumza na Mwananchi, Mtaka alisema kuna makosa madogo ambayo yanajitokeza ambayo wakuu wa wilaya au mikoa wangeweza kuyamaliza kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma.

Alisema kumekuwapo na matukio ya watumishi kuwekwa ndani yanayoshusha molari kwa watumishi.

“Mamlaka ya kinidhamu kwa kila mtumishi zipo na hazipaswi kupuuzwa, zipo namna ya kufanya daktari, mwalimu, ofisi elimu, polisi wanapokosea lakini si kupelekwa polisi,” alisema Mtaka.

“Hivi baada ya kumweka ndani na kutoka kipi kinafuata? Ukitumia mamlaka vibaya huwezi kupata matokeo,” aliongeza, “Kama ni kiongozi unasimamia misingi ya utumishi wa umma? Sisi tunasema huwezi kujenga uchumi wa kipolisi katika mikoa.”

Alisema si watumishi wa umma pekee, bali hata wanasiasa wakiwamo wabunge na madiwani hawapaswi kuwekwa ndani ovyo, “Ukimaliza kuwaweka watumishi wa ndani wakaisha, mtaanza kuwekana wenyewe, huoni kuna wabunge wa CCM nao wanalalamika! Kwa maana watu wa kuweka ndani wameisha mnaanza kuwekana wenyewe na mwisho wa siku unabaki wewe mwenyewe.”

Alisema katika utumishi kuna eneo la mkuu wa mkoa, wilaya, mbunge na diwani ambao kwa pamoja wanapaswa kushirikiana ili kufikia azma ya dira ya Taifa ya maendeleo na vipaumbele vya Rais John Magufuli.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipotakiwa kutoa maoni yake juu kauli hiyo ya Mtaka alisema, “Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na sheria tuliziojiwekea na huu ndio msimamo wa CCM na Rais John Magufuli anasimamia hilo.”

Polepole alisema, “Viongozi wanaofanya kazi CCM au serikalini kwa niaba ya CCM wanapaswa kuheshimu Katiba, sheria na taratibu nzuri. Wachape kazi zaidi kwa sababu muda haututoshi.”

Akitoa maoni yake, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema, “Nampongeza sana Mtaka na hao ndio viongozi au wasaidizi wanaopaswa kumsaidia Rais. Mtaka amekuwa mtu anayeshauri kwani unapokuwa na viongozi wanaowaweka ndani watumishi wa chini inasababisha kushuka kwa morali ya kufanya kazi.”

Sugu alisema mtumishi wa umma anapokosea kuna taratibu za kinidhamu na si kuwekwa ndani jambo ambalo halina tija.

“Kama mtu amekosea kwa nini asiwajibishwe kwa sheria za utumishi? Kwa hiyo alichokisema Mtaka ni kweli kabisa na watendaji wote mawaziri, wakuu wa mikoa wawe kama Mtaka,” alisema Sugu.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za BInadamu (THDRC), Onesmo Ole Ngurumwa alisema, “Tunampongeza sana RC Mtaka na wengine wanapaswa kujitokeza na kukemea vitendo hivi kama alivyofanya Waziri Jafo.”

Alisema matumizi ya kumweka ndani mtu saa 24 au 48, “Yalilenga kipindi cha ukoloni na kwa mtu anayetishia amani, sasa hivi mtu anawekwa ndani kwa kuchelewa au kusimamia mradi visivyo jambo ambalo anaweza kushughulikiwa kwa taratibu za kinidhamu.

“Umefika wakati sasa tukaacha tu kusema na tukaenda kubadili hiyo sheria ambayo imekuwa haitumiki visivyo lakini kwa ma RC na DC wanapaswa kufuata nyayo za Mtaka ambaye amekuwa RC anayejali na kusimamia misingi ya utawala bora,” alisema Ole Ngurumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ndio mkuu wangu wa Mkoa bora kabisa wa zama hizi.
Simiyu ya Viwanda naielewa zaidi ya ''mikoa mingine yote ya Viwanda.''

Namkumbuka jamaa mmoja wa china ambaye baadae akaja kuwa waziri chini ya DENG XIOPING alipopewa Jimbo masikini kabisa awe gavana, Mambo aliyoyafanya kwa vitendo aliishangaza china nzima na kupewa uwaziri mkuu kabisa ili hicho alichokifanya akifanye kkwa nchi nzima.

huyu jamaa pia anafanya vizuri.
 
Huyu ndio mkuu wangu wa Mkoa bora kabisa wa zama hizi.
Simiyu ya Viwanda naielewa zaidi ya ''mikoa mingine yote ya Viwanda.''

Namkumbuka jamaa mmoja wa china ambaye baadae akaja kuwa waziri chini ya DENG XIOPING alipopewa Jimbo masikini kabisa awe gavana, Mambo aliyoyafanya kwa vitendo aliishangaza china nzima na kupewa uwaziri mkuu kabisa ili hicho alichokifanya akifanye kkwa nchi nzima.

huyu jamaa pia anafanya vizuri.
Lakini hapa anaweza kutumbuliwa mchana kweupeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kidogo mna conclude et jamaa ni smart RC kuliko wote Tanzania. Haya subirini rungu jipya linalochongwa huko then mje kutupigia kelele humu jukwaani!

Wanacheza na akili za wananchi hao waangalieni vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hapa anaweza kutumbuliwa mchana kweupeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
sidhani maana anaonekana ni mnyenyekevu. Wengine wengi wanakutana na tumbuatumbua huwa wanamambo mengi na wengine wanatafuta masifa hadi wanapitiliza.
Yule jamaa hata akitumbuliwa nilivyomuangalia kipindi chake kimoja TBC na kauli zake hawezi kuteteleka maana akili zake zimekaa sawa, ni mtu wa maono na mwenye roho ya kijasiliamali ndani yake.
watu wa namna hiyo hata uwakate mikono na miguu watatoka tu.
Simfahamu kiundani zaidi ya maneno, matendo na mipango yake hasa kwenye kauli mbiu ya TANZANIA YA VIWANDA lakini. Wanasiasa wenyewe wanfahamiana zaidi nje ndani
 
Huyu ndio mkuu wangu wa Mkoa bora kabisa wa zama hizi.
Simiyu ya Viwanda naielewa zaidi ya ''mikoa mingine yote ya Viwanda.''

Namkumbuka jamaa mmoja wa china ambaye baadae akaja kuwa waziri chini ya DENG XIOPING alipopewa Jimbo masikini kabisa awe gavana, Mambo aliyoyafanya kwa vitendo aliishangaza china nzima na kupewa uwaziri mkuu kabisa ili hicho alichokifanya akifanye kkwa nchi nzima.

huyu jamaa pia anafanya vizuri.

Mitale na Midimu, Hongereni sana Wanyantuzu kwa kuwa na RC Jembe!!

Anthony Mtaka anaonekana ni KIONGOZI na siyo MTAWALA. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kiongozi na Mtawala....na siku zote Viongozi wanazaliwa hawatengenezwi wala hawachongwi...Uongozi ni kipaji toka kwa Mwenye enzi Mungu....na Uongozi hausomewi darasani you can be even a best Professor or a Doctor and yet you can't manage even your own family...na haya yapo sana.

Anthony Mtaka huenda akawa Kiongozi bora sana katika Nchi ya Tanzania kwa siku za usoni. Kwa namna anavyo uongoza na kuusimamia Mkoa wa Simiyu hakika huyu jamaa anahitaji tuzo.

Ushauri kwa Rais Magufuli:

Kwa vile hata KM wa CCM Bwana Bashiru Ally alitoa pongezi kwa RC Mtaka wakti wa maazimisho ya NANENANE kule Simiyu na kusema Mkoa wa Simiyu unaongoza kwa kuwa na Uongozi Bora usio na migogoro kati ya Viongozi wote wa Serikali, Chama na Upinzani basi ni wakti wa ma-RC wote Tanzania wajifunze kutoka kwa RC Mtaka kwa aidha kuwapeleka mkoani Simiyu wakajifunze kwa vitendo au Mhe. Mtaka apewe muda wa kuendesha Semina kwa ma-RCs na DCs wote nchi nzima ili wawe Viongozi wa mfano wa Anthony Mtaka.

Hongera sana RC Anthony Mtaka.
 
Bwana azidi kumuinua maana ana hofu ya MUNGU ndo maana anayafanya haya,wasio na hofu ya MUNGU hata hapa watamzodoa nakuukataa ukweli, UKIMPENDA MUNGU,HAKI YAKE ITAKA NDANI YAKO,kudos RC MTAKA
 
Kitu kidogo mna conclude et jamaa ni smart RC kuliko wote Tanzania. Haya subirini rungu jipya linalochongwa huko then mje kutupigia kelele humu jukwaani!

Wanacheza na akili za wananchi hao waangalieni vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe acha wivu wa kike wewe.
Yawezekana kabisa wewe una roho ya Paul Makondo(RC-DSM) a.k.a Bashite,Mrisho Gambo(RC-ARS), Alexander Mnyeti(RC-Manyara), Happines Ally(RC-IR) na ma-RCs/DCs wengineo wajingawajinga wenye tabia kama hizo.
Hakika huwezi kujenga Viwanda au kuleta maendeleo popote kwa kuwaweka watu MAHABUSU masaa 24/48....Kwangu mimi huo ni wendawazimu wala si uongozi...!!
 
Wewe acha wivu wa kike wewe.
Yawezekana kabisa wewe una roho ya Paul Makondo(RC-DSM) a.k.a Bashite,Mrisho Gambo(RC-ARS), Alexander Mnyeti(RC-Manyara), Happines Ally(RC-IR) na ma-RCs/DCs wengineo wajingawajinga wenye tabia kama hizo.
Hakika huwezi kujenga Viwanda au kuleta maendeleo popote kwa kuwaweka watu MAHABUSU masaa 24/48....Kwangu mimi huo ni wendawazimu wala si uongozi...!!
Kati ya mie na wewe nani anawivu wa kike, una wataja hao watu wa nini sasa..?

Si furahishwi na hatua wanazo chukua ila hapo Kuna mkakati elewa hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya mie na wewe nani anawivu wa kike, una wataja hao watu wa nini sasa..?

Si furahishwi na hatua wanazo chukua ila hapo Kuna mkakati elewa hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama hujui kwanini nimewataja hao Wakuu wa Mikoa basi darasani ulikuwa unashika mkia..!!
Hapa tunazungumzia utendaji kazi uliotukuka wa RC-Simiyu Mhe. Mtaka. Niliowataja ni kuwataka waache utendaji wao mbovu kwa kujifunza toka kwa RC Mtaka waache upuzi wao wa kuweka watu Mahabusu kwa kuwakomoa Watumishi pasi na sababu za msingi..!!!!sasa wivu wangu ni upi hapo? RC Mtaka anasema huwezi kujenga kiwanda kwa kuwaweka watu mahabusu..!!
RC Mtaka pia anasema ukishawaweka Mahabusu Watumishi wote kwanza unawapunguzia morali ya kazi na pili unajenga chuki miongozi mwa Watumishi matokeo yake ni migogoro isiyo na mwisho.......matokeo yake badaa ya kujenga viwanda unajenga au kutengeza migogoro..hiyo ni akili muflisi na ukichaa....!!
 
Back
Top Bottom