Msimamo: Nitasimama na Majemedari Ninaowajua, Tuliopigana Vita Pamoja Nao...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
40,000
hqdefault.jpg

(Pichani Mwalimu Nyerere akiwa na Majemedari Wake wakati wa Vita ya Kagera)

Neno la Leo: Unapoenda vitani unaenda na makamanda wapiganaji wako, makamanda wako na majemedari wako. Wapiganaji wako wanapoanguka hurudi nyuma unaendelea kusimama, makamanda wakijeruhiwa unawasaidia wanainuka mnaendelea mapambano, na majemedari wenu wakiumizwa mnaendelea kusimama nyuma yao na kuendelea kusonga mbele (charge).

Jemedari wa upinzani anapoamua kubadili kambi na kuja upande wenu hata akiwa maarufu kiasi gani KAMWE hamuwaondoi majemedari wenu na kumpa yeye ukumbi ati aongoze vita kwa sababu mnataka ushindi tu! Zaidi mtamtumia mtu huyo kwa ushauri zaidi, msaada wa maono kutokana na ujuzi wa kule anakotoka.

Ni kweli inawezekana mnautaka ushindi lakini ushindi hauji kwa "gharama yoyote"! Jamani hata vita ina kanuni zake - Rules of Engagement. Kuna baadhi ya mambo hata kama yanaweza kusaidia vita hayaruhusiwi vitani na yakifanyika matokeo yake yanaweza kuwa ni ya hatari sana na ndio maana kuna vitu kama Geneva Convention kusimamia kanuni hizi za vita.

Huwezi kusema ati unataka kushinda vita kwa gharama yoyote hata kama utaua wanawake, watoto na wazee, raia n.k Kusema "tunataka ushindi kwa gharama au namna yoyote" ni kufungua milango ya hatari sana kwani unaweza kujikuta unamkaribisha jemedari wa adui na kumuingiza hadi kwenye mipango yenu ya vita na akawashauri vizuri... na wenyewe mkafurahia hadi mtakapojikuta mmeingia kwenye mtego usioachia.

Ni kwa sababu hiyo, wakati vita tunasimama na makamanda na majemedari wetu tuliokuwa nao, tuliopigana vita pamoja, tuliojeruhiwa pamoja. We DO NOT LEAVE A MAN BEHIND! Tunaweza kuweka imani yetu kwa majemedari tunaowajua hata maisha yetu lakini tutakuwa tayari kufa kwa jemedari tusiyemjua ambaye tulisikia umahiri wake alipokuwa upande wa adui na jinsi alivyowatenda askari wetu walipoangukia mikononi mwake?

Tutakuwa na imani na jemedari aliyehamia kwetu wakati alipokuwa upande ule hakuzuia majeshi yake kuwatenda vibaya askari wetu na raia wetu? Wakati watoto wetu, mabinti na dada zetu, wake zetu na mama zetu wanapigwa na kuuawa na waandishi wetu wanaumizwa hakusimama upande ule kupinga au kuonesha kujali lakini leo aje upande wetu tumkumbatie ati kwa vile tunataka kushinda?

Lakini itakuwaje kama jemedari huyo anakuja na maafisa wake nawapiganaji wake ambao nao wanataka kuchukua nafasi za mbele. Watakuwa kweli wanapigania jeshi letu au wanapigania maslahi yao na nafasi zao? Na ikitokea tukashinda huyu jemedari mahili atakuwa kweli chini ya jeshi letu au itabidi tumfuate anakotaka yeye sasa? Na tukishindwa kweli tutaweza kumlaumu yeye kwa kushindwa kwetu wakati ni sisi wenyewe tulimfuata aje atuongoze vita ambayo tayari tulikuwa tunashinda chini ya majemedari wetu tuliotoka nao mbali?

Ukiniuliza mimi... nitasimama na majemedari ninaowajua hata kama hatutashinda vita lakini najua pamoja nao tumepigana hadi dakika ya mwisho. Jemedari mgeni akija na akatusaidia kushinda vita nyuma ya majemedari yetu mchango wake hautasahaulika. Jemedari mgeni akisimama nyuma ya makamanda wetu na kuunga mkono mapambano kwa kadiri ya uwezo wake tutakubali na kushukuru. Siyo kinyume cha hivyo.

NB: Iangalie hiyo picha juu halafu jiulize; kweli Watanzania wangemwelewa Nyerere na uongozi wa Taifa kumchukua Generali wa Idi Amin (amekosana na Idi Amin au vipi) halafu aje huku achukue nafasi za kina Mwita Marwa, Musuguli na wengine? Kwamba ati huyo Generali kwa vile alikuwa karibu sana na Idi Amin na maarufu sana akiwa Uganda basi atafaa kuongoza majeshi ya Tanzania? Tungeshangilia kweli kweli... kina Musuguli, Kyaro, Kiwelu, n.k wangemwelewa Nyerere ati kwa vile tulitaka kushinda vita "by any means necessary"? Siyo kwamba, pamoja na hela, vifaa n.k alivyokuwa navyo Idi Amin majenerali wetu wenye uzoefu na tulioawamini ndio waliotupatia ushindi?



THERE ARE CERTAIN THINGS YOU DO NOT COMPROMISE... NONE MORE THAN PRINCIPLES.
 
Nakuelewa sana mwanakijiji, lkn kwa muda huu hatuhitaji chadema iliyopasuka. Tunahitaji kushikamana.
Ni vizuri kuwa na reservation kama waliyokuwanayo mitume Paulo alipoongoka; lkn maanndiko yanashuhudia jinsi gani Paulo alifanya makubwa kuliko baaadhi ya mitume (au majemedari if you may) waliokuwepo tangu mwanzo..
 
Adui tunayepambana naye amejijengea mizizi mirefu!! Kila tunapopigana anatumia nguvu za ziada!!! Cha kufanya ni kumpasua na kumpiga kwa silaha za kisasa tulizoziteka kipindi tunampasua.....Ila taadhari kuu tusikabidhi mipango ya kivita yote kwa jemedari mpinzan alitegeuka rafiki......
Utekaji ni moja ya mbinu mathubuti kwenye uwanja wa vita Tena unapomteka mmoja wa majemedari wakuu !! Mi naona tutumie nafasi hii kiuadilifu tusijisahau na kupokea visivyo na tutende kwa akili....
 
.....lengo letu ni kuishinda ccm,hivyo tutawasajili wapiganaji kwa kadri tuwezavyo......wewe hautaki kushinda vita na kufurahi kwanza...then mengine yafuate


Nyie mnafanya mchezo; mnataka tuwe kama Zambia? au Malawi? au Kenya wakati wa Kibaki? Haitoshi tu kushinda vita! Hujaona Sudan ya Kusini; haitoshi tu kushinda vita mkajikuta kwenye mapigano mengine kabisa...
 
mnimekuelewa vema kabisa kunguru rafiki yake hawezi kuwa njiwa,kunguru ana yake na njiwa wanayotofauti kabisa kiota kinapasuka kunguru atajenga chake na njiwa chake kama huko kwa wenzetu ilivyowahi kutokea
 
Nyie mnafanya mchezo; mnataka tuwe kama Zambia? au Malawi? au Kenya wakati wa Kibaki? Haitoshi tu kushinda vita! Hujaona Sudan ya Kusini; haitoshi tu kushinda vita mkajikuta kwenye mapigano mengine kabisa...

Unatumika MM

Mwandishi mwenye ueledi huwezi kuwa bias kama unavyoonesha hapa.

Watanzania walitaraji uwape moyo waondokane na mfumo mbovu unaowaumiza mpaka wazazi wako kule KAMACHUMU mpaka UBARUKU.

Nlishakudharau.
 
Kufananisha siasa na vita ni ujin.ga na upumba.vu...... Ulitakiwa kuchukua mfano mdogo tu kutoka kwa nchi zingine zilizofanikiwa katika kuangusha vyama tawala madarakani

mkuu ocampo four Huyu mzeee huwa kila Siku nasema analaeta siasa za maandiko yake ya kusadikika yy ana chuki binafsi na lowassa ni watu waliofrahi kupata magufuli au ni MTU Wa magufuli ameula Wa chuya. MTU yuko ughaibuni amekaaa kenye nae atoa ushauri ambao hauna hata utafiti bure kabisa. Amsikilize kitila mkumbo Jana alivochambua arrival ya lowassa ameacha ushabiki pembeni na kuongea fact na sio pumba.
 
Last edited by a moderator:
id amin ni tofauti na lowasa....kama chama chote tungekichukua thread yako ingekua na mashiko kwasababu id amin ndio tatizo lenyewe na pale nyerere alipigana nae c waganda non sense
 
Sijui mnatakaje chadema iwe makamanda. Leticia Nyerere ni jemedari tuliesimama nae, zitto kabwe pia, said arfi pia, chiku abwao pia! Leo tumempata jemedari alietendwa vibaya kutoka kwa maadui zetu halafu tunaleta u conservatism! Siasa usifananishe na vita bali mpira wa miguu labda!
 
Back
Top Bottom