Msichana wa kazi za ndani

Ni 22,800 kwa wanaokaa kwa muajiri kwa maana huduma zote hadi medical ziko juu ya muajiri! Sh 60,000 kwa wanarudi makwao! Ila Market price ya Dar ni 40,000 upwards!

kwahiyo mpwapwa tuna market price yetu na dar yenu!

Sisi wengine hatuyawezi haya ya wadada wasaidizi wa kazi za nyumbani. Hata kuwaita ma-house girl tu sipendi. Nawaoneaga huruma sana. Na sijawahi na wala sitegemei kuwa siku moja nitaajiri mdada au mkaka wa kazi za nyumbani kwa sababu yote wanayofanya hao wasaidizi naweza kufanya mwenyewe. Ni kupangilia muda wako vizuri tu na utaweza kufanya. Angalau kwangu hili linawezekana sasa sijui kwa wengine.

Ila kuna watu wengine naonaga kabisa kuwa huwa hawahitaji hao "house girls" lakini unakutata anaye. Tena anaye na anaishi humo humo ndani ya nyumba. Kwangu inasikitisha sana.

Nilikutana na rafiki yangu mmoja Bongo ana mtoto wa mwaka mmoja. Ananambia ana wafanyakazi wa wawili wa ndani. Na wote anawalipa 40,000 kila mmoja. Kisingizio ni mtoto ni mtundu kwa hiyo mmoja kazi yake kumtumbulia macho mtoto tu siku nzima!

Sasa huyu nae atasemaje?

Mimi nakataa kumwita house girl pia. Na nadhani hiyo ni moja ya sababu zinazofanya watu wasiwachukulie serious. Ile notion kuwa wale ni wafanyakazi, na wewe ni muajiri wao, inakuwa haipo.

• Thanks
Reactions: EMT

khaaaaaaaaaaaa!!
Huku pm unampigia pande sister wako halafu hapa unazuga.
Ok, mwambie sister wako ajiandae kwa interview.

Halaf jana msikitini shehe kasema PM haraam, naomba unirejeshee PM zangu tangu januari

Wanasumbua sana siku hizi,mi binafsi kwa mwaka huu wamepita mabei 3 wanne na wameshalala mbele,ukipata wa bush anaweza kaa kidogo.La sivyo uka hire wa kimjini mjini lakini ndo hawatulii,wako ki mishe mishe.

Sio kuwa wanasumbua. Wameamka na kujua haki zao. Housesgirls are the most exploited people in Tanzania. Sheria zetu haziwalindi kabisa. Linganisha na yule Mtanzania ambaye amefungwa huko Uingereza kwa kumfanya housegirl mbongo kama mtumwa.

Ni 22,800 kwa wanaokaa kwa muajiri kwa maana huduma zote hadi medical ziko juu ya muajiri! Sh 60,000 kwa wanarudi makwao! Ila Market price ya Dar ni 40,000 upwards!
Mmh! Lakini hii naona inaapply kwa familia nyingi!
Kama anapata service zote kama mtoto wa familia, zaidi ya 40,000 itakuwa unam overpay!

Lol...Hebu anza kutueleza utakayo yasema tuchangie mawazo usije ukaiadhalilisha JF

Mkuu wewe angalia tu ikifika mida! jibaba nitakula pafyum mtaliskia mpaka kwenye mascreen ya tv zenu! nitamchambua Gaddafi tangu anavaa pampers, halaf namalizia na NATO! nitaongea kwa kimombo nawashauri mkae na dikshineri karib

Nilikutana na rafiki yangu mmoja Bongo ana mtoto wa mwaka mmoja. Ananambia ana wafanyakazi wa wawili wa ndani. Na wote anawalipa 40,000 kila mmoja. Kisingizio ni mtoto ni mtundu kwa hiyo mmoja kazi yake kumtumbulia macho mtoto tu siku nzima!

Yaani ana wasaidizi wawili? Kweli watu tumetofautiana!!

Ila huenda hako katoto kana DNA za ki-Ngabu....heheheeeee

Mlipe kima cha chini. Na chama cha wafanyakazi kilio chao kikijibiwa, kima cha chini kikipandishwa, nawe mshahara wake itabidi umpandishie.

wewe uliona wapi mfanyakazi anapewa uji wa maziwa,chakula cha mchana na jioni,chumba cha kulala.anaskiliza news kwenye tv na radio,analetewa zawadi ya nguo na nmanukato?ukisema upige hesabu hata laki 6 inafika.hiyo elf 30 ni deposit tu.hataitumia coz kila kitu anapata.mia

Gaijin asume you are a single mother, primary school teacher mshahara wako ni 200,000 unaishi jijini Dar! U need a help na jua hakuna day care center mbagala (ulipopanga) na kuna binti katoka Iringa anatafuta kazi za ndani utafanyaje?

Huko nje unapolonganisha, kuna options; kwanza mishahara mizuri, kuna kazi za few hrs, kuna daycare ambazo ziko registered though expensive! Wanaume wako so understanding that wanapeana zamu na wake zao kutake care ya watoto! Hakuna mgao wa Umeme that appliances like washing machines, dish washer etc zinakuwa na meaning that kazi zinapungua! So unappcompare baadhi ya vitu, usiache vingine kwani kila kitu kinaeffect kwa kingine!

Mkuu wewe angalia tu ikifika mida! jibaba nitakula pafyum mtaliskia mpaka kwenye mascreen ya tv zenu! nitamchambua Gaddafi tangu anavaa pampers, halaf namalizia na NATO! nitaongea kwa kimombo nawashauri mkae na dikshineri karib
Hahaha..uhakikishie unatilia na Kanzu maridadi au magwanda ya ukweli ili tuelewe kweli mlizaliwa mtaa mmoja!
Kiarabu hukielewi kidogo? Kimombo pekee hakitoshi!

wewe uliona wapi mfanyakazi anapewa uji wa maziwa,chakula cha mchana na jioni,chumba cha kulala.anaskiliza news kwenye tv na radio,analetewa zawadi ya nguo na nmanukato?ukisema upige hesabu hata laki 6 inafika.hiyo elf 30 ni deposit tu.hataitumia coz kila kitu anapata.mia

Dah! Lawyer wa Husninyo kahuzuria na hasira sana. mia

Gaijin asume you are a single mother, primary school teacher mshahara wako ni 200,000 unaishi jijini Dar! U need a help na jua hakuna day care center mbagala (ulipopanga) na kuna binti katoka Iringa anatafuta kazi za ndani utafanyaje?

Huko nje unapolonganisha, kuna options; kwanza mishahara mizuri, kuna kazi za few hrs, kuna daycare ambazo ziko registered though expensive! Wanaume wako so understanding that wanapeana zamu na wake zao kutake care ya watoto! Hakuna mgao wa Umeme that appliances like washing machines, dish washer etc zinakuwa na meaning that kazi zinapungua! So unappcompare baadhi ya vitu, usiache vingine kwani kila kitu kinaeffect kwa kingine!

ukitulia unakuwa na akili....
hebu nijibu ile pm....lol

Nina miaka zaidi ya 16 nikiishi na HGs mbalimbali na mimi ndio bosi wao si kwamba HG ni wa ndugu yangu bali ni wangu kabisa.
Sikatai nimefanya makosa kadhaa ktk kuishi nao na nimejifunza mambo mengi kupitia kwao. Miaka ya mwanzo ilikuwa ngumu sana maana kiuri na mimi nilikuwa mdogo.
Ila kadri siku zilivyozidi kwenda nimejifunza ni msichana gani ninayemtaka. Na siku hizi sina headache hata kidogo nimesomesha wengi hadi mmoja sasa ni wifi yangu kabisa. Mwingine sasa anasoma chuo kikuu. Nimekuwa na wasichana wenye elimu ya F4 na wa drs 7.
HG ni binadamu. Tusipotambua kuwepo kwao ndio kunakufanya wewe uweze kutengeneza hela basi tutawabadilisha hadi tukome.
Nimeanza kuwa na HG enzi za mshahara ni elfu 6000 tu! Hadi hivi leo mishahara ya kawaida ni 40000 na siko radhi kutoa hiyo 40000 naongeza cha juu ndio maisha yanaenda na yeye anajisikia anathaminiwa na anaitoa kufanya kazi.
Sikatai kuna wendawazimu wachache ila hiyo hainipi shida na wala sibembelezi. Akiwa amechoka namruhusu aende kwao na kwa taarifa kwa wazazi.

• Thanks
Reactions: EMT

wewe uliona wapi mfanyakazi anapewa uji wa maziwa,chakula cha mchana na jioni,chumba cha kulala.anaskiliza news kwenye tv na radio,analetewa zawadi ya nguo na nmanukato?ukisema upige hesabu hata laki 6 inafika.hiyo elf 30 ni deposit tu.hataitumia coz kila kitu anapata.mia

Kwanza elewa kuwa ile ni kazi sio charity. Hayo ya kumletea perfume sijui na vitu vyengine sio ndani ya sheria za kazi. Usipotaka usifanye. Pili unamnyima uhuru wake kama binaadamu wa kuishi anavyotaka na in short anakuwa kama mtumwa wako tu maana hamna masaa ya kazi wala hakuna off day, wala hakuna overtime.

Ile ni ajira, na kila ajira lazima ichukuliwe hivyo, na kuwe na mipaka katika ajira hiyo.

Hahaha..uhakikishie unatilia na Kanzu maridadi au magwanda ya ukweli ili tuelewe kweli mlizaliwa mtaa mmoja!
Kiarabu hukielewi kidogo? Kimombo pekee hakitoshi!

Hapa mtaani wananiita google translator, kibangladeshi pia nachanganya, last week nilifturu kwa mtangazaji wa aljazeera ya kiarabu.

Gaijin asume you are a single mother, primary school teacher mshahara wako ni 200,000 unaishi jijini Dar! U need a help na jua hakuna day care center mbagala (ulipopanga) na kuna binti katoka Iringa anatafuta kazi za ndani utafanyaje?

Huko nje unapolonganisha, kuna options; kwanza mishahara mizuri, kuna kazi za few hrs, kuna daycare ambazo ziko registered though expensive! Wanaume wako so understanding that wanapeana zamu na wake zao kutake care ya watoto! Hakuna mgao wa Umeme that appliances like washing machines, dish washer etc zinakuwa na meaning that kazi zinapungua! So unappcompare baadhi ya vitu, usiache vingine kwani kila kitu kinaeffect kwa kingine!

kwanza tambua kuwa kama system or call it fate if you want imekupa hali mbaya, hai-justify wewe kumnyonya mwengine. Sote tunakimbilia easy way out, get a maid and pay her peanuts bila ya kufikiria options nyengine.

Nitakupa mfano, yupo dada mmoja ambae anafanya kazi na ana watoto wadogo. Wifi yake she works from home na ana watoto wadogo pia. Wanachofanya ni huyu anaeenda kazini, ni kuwa pick up watoto wa wifi na kuwapelekea shule yeye akenda kazini, na kumdrop mtoto wake kwa wifi, akae hapo mpaka jioni akenda kumchukua.

So you can see, kumbe kuna options nyengine lakini watu hatujakaa tukaanza kuzifikiria tu kwa sababu easy option ipo.

Kwanza elewa kuwa ile ni kazi sio charity. Hayo ya kumletea perfume sijui na vitu vyengine sio ndani ya sheria za kazi. Usipotaka usifanye. Pili unamnyima uhuru wake kama binaadamu wa kuishi anavyotaka na in short anakuwa kama mtumwa wako tu maana hamna masaa ya kazi wala hakuna off day, wala hakuna overtime.

Ile ni ajira, na kila ajira lazima ichukuliwe hivyo, na kuwe na mipaka katika ajira hiyo.

HG ni mwanafamilia.mia

Back
Top Bottom