Msichana kaning'ang'ania, nifanyeje?

Acha izo dogo wewe ndo umemganda. Kisa ana kazi unaenda kula kwake buree kitanda unalala bure hujawai kuja kwake hata na kilo 2 za nyama , mnavyopenda kulelewa mpaka kero, leo unakuja kutangaza huku? Wadanganye watoto wenzio,bint wa watu akugande kwa lip ulokuwa nalo?
 
Kuna msichana mmoja niko nae kaning'ang'ania. Nimeshamwambia twende taratibu lakini yeye ana kasi sana, mara ananiita mume. Wakati bado nataka tuchunguzane kwanza. Yaani kajaa matumaini mpaka nashangaa yaani ameshajua kama mi ndio namuoa.

Nifanye ili nimuache?Ushauri

Umeiona Ile Mada Yangu Ya "Are U In Relationship As Marriage Or Just Entertainment"??? Ebu Ingia Kwny Huo Uzi. Acha Kuwa Fisadi Wa Mapenzi
 
Ha ha ha ww unakimbia committment jamaa yangu.Ushaona mwenzio yupo serious wewe kama unaona haupo katika ukurasa mmoja kama yeye inabidi usimpotezee muda wake huyo msichana.
 
Usimpotezee muda mwenzio, muweke wazi kuhusu sababu ya wewe kuanzisha mahusiano naye. Kama ni ku have fun ajue na kama ni commitment za ndoa baadae pia ajue.
Bishara za kusema unamchunguza akati uroda unapata kama kawa siyo powa kabisa.
Muweke wazi achangue mbivu or mbichi
 
kwani kukuita mume ni tatizo mkuu, kuna jamaa Hapo mlango wa pili analalamika kuitwa "WEWE", Au kuna sababu nyingine???. Au humpendi tu? Ushamchoka? Au sio mwaminifu kwako,? unataka mwanamke akufanyie nini ujue anakupenda,?? Au mwenzio ana focus Ndoa, wewe ni Hit and Run?? Kwanini upo katika mahusiano?? Aisee Kama humpendi Mdada wa watu, usimpotezee muda, mwache, wapo wanaoelewa Kwanini wapo katika mahusiano watamuelewa.

mkuu umeongea vzur sana aicee lkn tatzo ni kwamba tunahangaika na ----- wakat wenzake tuna enjoy kuitwa mme na majna mengne mazur lenyewe halitak sjui jtu gan hil jaman?????!!
 
Huyo dawa yake mbona ndogo
We mpe sugari guru halafu changanya na mboga ya mgagani mwambie aweke kwenye papuchi kwa muda wa Masaa 48..halafu mpande kama beberu uone kama atakusumbua tena na wewe kama utamchunguza tena zaidi ya kutangaza ndoa tu kwa utamu wa mgagani..

Sikununu ktk ubora wake mzee wa vituko umepotea sana Mkuu
 
Kuna msichana mmoja niko nae kaning'ang'ania. Nimeshamwambia twende taratibu lakini yeye ana kasi sana, mara ananiita mume. Wakati bado nataka tuchunguzane kwanza. Yaani kajaa matumaini mpaka nashangaa yaani ameshajua kama mi ndio namuoa.

Nifanye ili nimuache?Ushauri
Ana kiu ya kuolewa huyo, wanawake wengi huwa na kasumba ya kujificha nyuma ya mapenzi lakini ukweli hawana mapenzi ya dhati na mtu isipokuwa wanataka kutimiza adhma yao ya kuolewa ili kuficha fedheha ya kukaa bila kuolewa au kukomesha maex walioachana bila kuoana au kaona fursa kwako na wakati mwingine Huwa na nia ya dhati.

Sasa fanya hivi.
1. Mchunguze ni mkweli kiasi Gani.
2.Muombe simu yake ukae nayo siku nzima, akikubali hata usiichukue lkn akikataa anzia hapo kuchunguza kujua anakuficha Nini.
3. Wakati mwingine kuna mtu anayempenda sana alimuacha akaoa mwanamke mwingine hivyo anataka kufanya revenge, kama ni hivyo wewe unatumika tu kama daraja la revenge ila mbeleni utachapiwa tu.

4.Anza kuchunguza kama anazo attributes za kuwa mke ama la, je ni msafi? si mvivu, si mwanaharakati, ni mpambanaji, anaweza kukuvumilia kwa hali zote, angalia ground ya familia yake kama anayeiongoza familia ni mama au baba? namaanisha who is most superior hapo kwao? Kama ni baba anadeserve kuolewa, kama ni mama basi Anza kukagua mitazamo yake kuhusu wanaume.

5. Muombe Mungu akusaidie kuwa na uchaguzi smart, kumbuka "ni heri kuvunja uchumba kuliko ndoa"
 
Mwanaume mpumbafu ni yule anayetongoza harafu anasema ngoja nimchunguze , unamchunguza Nini

Sikiliza kama unataka mke wa kuoa hachunguzwi hivyo , mwanamke huchunguzwa pasipo yeye kufahamu lolote ukijiridhisha ndiyo uingie mazima mazima

Hakunaga kuchunguza wakati mnapigana miti mtindo Mmoja .

Narudia hakuna

Hapo mnapotezeana muda tu
 
Back
Top Bottom