MSIBA:Peter Gachuma,Thomson Msigwa WAFARIKI DUNIA

Na mwenyeji akipata ajali je, inakuwaje hapo?...Madereva wangapi tunasikia wanakufa Tanzania? Au nao wanakuwa wametoka nje?...Mwenyeji anapopata ajali na kufa ndio mta-substantiate ajali haikuweza kuzuilika? People Please!!!

Pumzikeni kwa Amani mliotutangulia. Poleni sawa Wafiwa.

Ukweli ni kwamba wenyeji nao wanajua namna ya kuzivunja sheria. Naam hata wenyeji wanaopoteza maisha katika barabara za Tanzania ni wengi mno. Kama sikosei mwaka 2004 au 2005 kuna vijana wanne au watano katika mwezi june na july walipoteza maisha katika barabara za Tanzania. Hao wote walikuwa wanaishi nje na walirudi Tanzania kwa likizo.

Imagine mtu aliyeendesha Tanzania miaka 10 au 15 tena aliendeshea Dar anajua uhuni wote wa barabara za Dar akwambie aisee naogopa kuendesha maana hiki kizungumkuti cha madaladala na madereva wengine kinaniacha hoi kabisa nisije kuwa statistics. Kwa hiyo ukisikia watu kama hao, unaamini kweli kuendesha bongo inabidi uwe na roho ngumu sana hasa kama ulikuwa nje kwa kipindi kirefu.
 
Maskini Thomson, huyu jamaa nilikuwa namfahamu vizuri sana pamoja na familia yake.

Pole sana bibie na mtoto. Mungu awasaidie na musafiri salama kwenda TZ.
 
Polen Sana Wafiwa ;nawashauri Muuangalie Huo Ujmbe Wa Kuendesha Gari Utawasaidia Sana ,,,else Mtapuputika Kwa Ajali Zinazoweza Kuepukika......
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Mungu ndie ajuae maisha yangu na yako yatakoma lini...

Mimi nipo msibani hapa home kwao Peter Gachuma(Tarime bukenye) mambo yote yanaendelea vema mipango ya mazishi inaendelea vizuri na kwa mujibu wa ratiba mwili wa mshikaji wetu utawekwa ardhini kesho.

Peter Mgendi Zacharia wa London Pole sana Kaka najua ulimpenda sana mshikaji ila mipango ya Mungu hakuna aijue.
mAg.
 
Nape Nnauye wa kitambo kumbe

Habari hzi nilizipata jana usiku,Peter Gachuma ni mtoto wa Mwita Gachuma yule Mjumbe NEC wa Chama Cha Mapinduzi na mfanyabiashara maarufu wa mikoa ya Mwanza na Mara.

Ajali ilitokea karibia na eneo ya igoma mjini mwanza,katikati ya igoma na kisesa,kwa habari nilizopewa ni kwamba waligonga Gari aina ya Fuso ambayo ilikuwa imesimama,ni hivyo kupata ajali mbaya sana sababu walikuwa katika mwendo mkali sana

Kwa niaba ya wana CCM wote na Watanzania Wote wa Hapa JF naomba kutoa salaam Za rambirambi kwa Mhe. Gachuma,

Leo ilikuwa Mhe. Gachuma aende India kwenda kufungua Rasmi Tawi la CCM lizindukliwa wiki ilioyopita na Nape Mnauye.
 
Last edited by a moderator:
Gachuma (Senior) ni mzalendo sana nimemjua nikiwa nasoma pale Tarime secondary. Mungu awatie nguvu familia za marehemu
 
Back
Top Bottom