Mshahara wa Mwenyekiti wa Mtaa na Diwani ni shilingi ngapi?

Habari za saa hizi wanajamii forum.Kwa mtu anayejua mwenyekiti wa mtaa na diwani wanalipwa mshahara kiasi gani na wakistaafu wanalipwa shilingi ngapi?
Mh wa Mtaa Hana mshahara ,
Diwani ndo analipwa posho za vikao na mshahara zamani ulikuwa 300k

Kuhusu mwenyekiti wa Mtaa anapata pesa za Ahsante kutoka kwa watu mbalimbali kwaiyo Kama yupo mjini hawezi kukosa hela ya kula ndo maana mtu hawezi kukubali kustaafu kirahisi .
 
Habari za saa hizi wanajamii forum.Kwa mtu anayejua mwenyekiti wa mtaa na diwani wanalipwa mshahara kiasi gani na wakistaafu wanalipwa shilingi ngapi?
Gombea tu hao wanakula keki ya Taifa. Kikokitoo hakiwahusu
 
Gombea tu ulambe asali katani mkuu. Kuna kakiinua mgongo baada ya miaka 5
 
N

Mwenyekiti wa Mtaa hakosi hela Mimi Babu yangu Ilikuwa mwenyekiti ,na Mama yangu so naelewa hizi Kazi Zina fursa that way sio Rahisi mtu akatae kugombea.
Mwenyekiti hana dili labda Mtendaji wa Mtaa ambate ni Mwajiriwa.

Hao wanapiga dili tu
 
Umewaza mbalii. Ni maamuzi mazuri lakini, pambana maana ni mwakani tu hapo.
 
Habari za saa hizi wanajamii forum.Kwa mtu anayejua mwenyekiti wa mtaa na diwani wanalipwa mshahara kiasi gani na wakistaafu wanalipwa shilingi ngapi?
MWENYEKITI WA MTAA;-
Mwenyekiti wa Mtaa hana Mshahara isipokuwa anapata posho ya simu Sh. 5,000 kila mwezi toka Kwa Mkurugenzi pia ana posho ya madaraka kwenye Mtaa ambao una vyanzo vya mapato.

Posho hiyo inaweza ikawa kati ya 20,000 mpaka 50,000 Kwa kila mwezi kutegemeana na mapato ya Kijiji au Mtaa husika.
Kikubwa huwa wanafanya madili Fulani Fulani ili kupata pesa
Anapostaafu hana chochote anacholipwa.

DIWANI
Diwani anapohudhuria vikao vya Halmashauri hulipwa posho kati ya 200,000 hadi 300,000 kila mwezi kwa kikao kimoja.

Akienda kukagua miradi hulipwa posho.

Akienda kwenye sherehe za Mwenge hulipwa posho.

Akienda katika Sikukuu za nane nane hulipwa posho.

Akienda mafunzo Wilaya au Mkoa fulani hulipwa posho.

Huwa wana madili pia.

Anapostaafu hulipwa kati ya 10,000,000 hadi 15,000,000 kwa miaka 5.
 
Yaan baba na mama wote wenyeviti mtaa mmoja
Nimekuambia Babu yangu na Mama then Bukoba watu wengi wanakuaga Wana vyeo viwili Mfano udiwani uenyekito so mimi Mama ni diwani na mwenyekiti as the same Babu yangu alikuwa mwenyekiti na pia diwani aligombea Hadi ubunge unfortunately hakupata .
 
MWENYEKITI WA MTAA;-
Mwenyekiti wa Mtaa hana Mshahara isipokuwa anapata posho ya simu Sh. 5,000 kila mwezi toka Kwa Mkurugenzi pia ana posho ya madaraka kwenye Mtaa ambao una vyanzo vya mapato.

Posho hiyo inaweza ikawa kati ya 20,000 mpaka 50,000 Kwa kila mwezi kutegemeana na mapato ya Kijiji au Mtaa husika.
Kikubwa huwa wanafanya madili Fulani Fulani ili kupata pesa
Anapostaafu hana chochote anacholipwa.

DIWANI
Diwani anapohudhuria vikao vya Halmashauri hulipwa posho kati ya 200,000 hadi 300,000 kila mwezi kwa kikao kimoja.

Akienda kukagua miradi hulipwa posho.

Akienda kwenye sherehe za Mwenge hulipwa posho.

Akienda katika Sikukuu za nane nane hulipwa posho.

Akienda mafunzo Wilaya au Mkoa fulani hulipwa posho.

Huwa wana madili pia.

Anapostaafu hulipwa kati ya 10,000,000 hadi 15,000,000 kwa miaka 5.
Hii nchi inaliwa na kutafunwa kwa kila njia - 'halali' na/au haramu
 
Back
Top Bottom