Msemakweli asakwa na polisi

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
KUNA ofisa mwenzetu wa polisi kituo cha Kijitonyama ametumwa na Yuauf Manji amkamate mwanasheria na Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria, Kainerugaba Erick Msemakweli, kwa madai kwamba alimuomba rushwa ya Sh Milioni kumi, hatua ambayo sisi katika polisi tumeiona kwamba inalenga kuzima harakati zake za kufichua wizi ulifanywa kupitia kampuni ya Kagoda Agricltural Limited.

Bahati mbaya sana ni kwamba mtu anayetumiwa na Manji kufanya mambo hayo ana uhusiano mkubwa na Mkurugenzi wetu (DCI), Robert Manumba, lakini mara nyingine mtu huyo hutumia vibaya jina la DCI kwa maslahi binafsi.

My take: Sasa Tanzania ni nchi pekee ya ajabu maana mtuhimiwa ndiye anatoa amri kwetu tumkamate mtoa taarifa. Hali hii ikiendelea, yale mauaji yaliyopewa jina la "wananchi wenye hasira kali" yatahamia katika ngazi ya juu kama hatua kali dhidi ya watuhumiwa wakuu hazitachukuliwa na wananchi wataamua kuanza kuchukua sheria mkononi. Serikali isipuuze hii hali si nzuri hata kidogo kwa usalama wetu kama Taifa la amani kwa miaka 50 iliyopita.
 
Tanzania!kila moja anasauti na kutoa amri!yaana inaenda kama gari isiyokuwa na dreva.
 
tunakokwenda, wananchi lazima watajua jinsi ya kutengeneza na kutumia Molotov cocktail tu!!!
walahi bilahi nakwambieni.
 
Yusuf ule mchezo wenu wa kununua viongozi haujaacha kaka?mimi ninashida ya mtaji wa biashara Million 25 tuu.
 
Nchi hii inakuwa kama vile wanyama porini , watu wenye fedha wameiweka serikali mifukoni!! Mfano ni pale Jangwani Beach mtu kajenga na kuziba barabara, wananchi wamepiga kelele halmashauri wamekuja na kuvunja kuta alizozibia barabara lakini kwa jeuri ya pesa jamaa kaziba tena barabara na halmashauri wanamtazama tu!!Hii ni aibu kwa serikali kama raia wanaweza kuvunja sheria na hawachukuliwi hatua.
 
Hii si hatari tu kwao ni hatari kwa Usalama wa Nchi, maana watu wakianza kuchukua sheria mkononi kwa watuhumiwa wakubwa kama ilivyo kwa vibaka ndio utakua mwanzo wa kutoweka kwa amani tunayojivunia Afrika nzima. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu walaani mafisadi.
 
Mh!! Kusema ukweli hawa ndugu zetu viongozi wasipokuwa makini mambo siku si nyingi yatakuwa magumu sana.
 
Nchi hii Waizi na Majambazi wana influence kubwa kuliko Watakatifu
 
Hatari ni kwamba amevifumba mdomo vyombo vya habari kwa fedha na kwa kutumia mahakama, amewazima MwanaHalisi, Raia Mwema, Dira, Mwananchi, Tanzania Daima na ... Kwa hiyo hakuna wa kuandika ila JF tu.l
Mahakama imeamuru kitu gani kuhusu Manji na magazeti?

Ipo siku Watanzania wataamka na kusema sasa inatosha kwa Dhulumati, sasa inatosha kwa Ufisadi, sasa inatosha kwa Wawekezaji Wezi(katika madini, gesi n.k), sasa inatosha kwa hawa Wahindi Koko kututawala na kuweka mifukoni mwao vyombo vya kutetea haki zetu kama Mahakama n.k. Siku hio ipo inakuja muda si mrefu.
Mungu ibariki Tanzania
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni sawa na jangwani beach kuna mtu anajitaa mkoroma anazuia upimaji wa viwanja vya watu. Huyo muhindi atakutana na nguvu ya wananchi na wanajeshi wastaafu kanali. Utapeli umezidi ramani tunayo mpima wa manispaa anabadili wakati ardhi ukweli upo mashamba yamefuta 2004 na wanyeji walikuwepo kabla
 
KUNA ofisa mwenzetu wa polisi kituo cha Kijitonyama ametumwa na Yuauf Manji amkamate mwanasheria na Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria, Kainerugaba Erick Msemakweli, kwa madai kwamba alimuomba rushwa ya Sh Milioni kumi, hatua ambayo sisi katika polisi tumeiona kwamba inalenga kuzima harakati zake za kufichua wizi ulifanywa kupitia kampuni ya Kagoda Agricltural Limited.

Bahati mbaya sana ni kwamba mtu anayetumiwa na Manji kufanya mambo hayo ana uhusiano mkubwa na Mkurugenzi wetu (DCI), Robert Manumba, lakini mara nyingine mtu huyo hutumia vibaya jina la DCI kwa maslahi binafsi.

My take: Sasa Tanzania ni nchi pekee ya ajabu maana mtuhimiwa ndiye anatoa amri kwetu tumkamate mtoa taarifa. Hali hii ikiendelea, yale mauaji yaliyopewa jina la "wananchi wenye hasira kali" yatahamia katika ngazi ya juu kama hatua kali dhidi ya watuhumiwa wakuu hazitachukuliwa na wananchi wataamua kuanza kuchukua sheria mkononi. Serikali isipuuze hii hali si nzuri hata kidogo kwa usalama wetu kama Taifa la amani kwa miaka 50 iliyopita.

Amani yenyewe imekwisha toweka kwa hali ya mambo inavyokwenda
 
Manji utakuja kuumbuka tu muda sio mrefu hata kama mambo yako yana mkono wa Rais au mawaziri kwani siku zote haki itasimama
 
Mahakama imeamuru kitu gani kuhusu Manji na magazeti?

Mahakama imeamuru kitu gani kuhusu Manji na magazeti?

Mahakama mbalimbali imezuia magazeti ya Dira, MwanaHalisi, Raia Mwema, Mwananchi na Tanzania Daima kutoandika chochote kuhusu Manji kiwe kibaya ama kizuri.
 
Back
Top Bottom