Msemaji wa Serikali amedhihirisha uelewa Mdogo wa watendaji wengi wa Serikali

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,086
Nimeshangaa sana leo kusikia kuwa eti msemaji wa Serikali, Ndugu Msigwa, amesema kuwa Rais ametoa uhuru wa kujieleza.

Mtu kuwa msemaji wa Serikali tunategemea awe na uelewa angalao wa kiwango cha kutosha kuhusiana na katiba ya nchi, sheria za nchi na mamlaka ya ofisi mbalimbali, ikiwemo ofisi ya Rais.

Kauli ya Hii bwana Msigwa inaonesha haelewi kabisa kuwa uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari, vimetolewa na katiba ya nchi, na siyo Rais. Rais ni zao la katiba. Rais analazimishwa na katiba kuhakikisha Serikali yake inalinda uhuru wa watu wa kutoa maoni, uhuru wa vyombo vya habari na kuheshimu haki za raia. Mambo haya siyo ya hiari kqa Serikali na Rais bali ni takwa la katiba.

Kama watanzania wasingekuwa waoga, wangeweza hata kumwondoa Rais na Serikali yake, kama itadhihirika kuwa Serikali yake au yeye binafsi anaminya uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari na haki za raia.

Uhuru wa maoni au uhuru wa kujieleza hautolewi kama zawadi na Rais bali katiba inampa hiyo haki kila raia, na Serikali na Rais, wajibu wao ni kuulinda.

Tukiwa na fikra kama hizi za ndugu yangu Msigwa kuwa eti uhuru wa maoni unatolewa na Rais, kuna siku tutakuja kusema hata haki ya kuishi inatolewa na Rais. Msigwa atakuja kusema kuwa Rais amewapa wananchi haki ya kuishi, lakini siyo kuishi mpaka mnapitiliza. Kuishi ni mwisho miaka fulani.

Ndugu zangu, hakuna ukomo wa uhuru wa maoni. Hakuna mahali ambapo utasema huyu ametumia uhuru wa maoni kupita kiasi. Kiasi kinawekwa na nani? Na kipimo chake ni kipi?

Kama mtu ametenda jinai, ashtakiwe kwa kutenda jinai. Tendo lolote la jinai wala halimaanishi uhuru wa maoni uliopitiliza.

Nikisema mtu fulani au kiongozi fulani ni mwizi, wakati huyo mtu huyo siyo mwizi, huwezi kusema kuwa nimetumia uhuru wa maoni vibaya. Hilo ni kosa la kumvunjia mtu heshima, wala siyo ķupitiliza kwa uhuru wa maoni.

Lakini nikisema Muungano wetu ni mbaya kwa sababu Wazanzibari wananufaika zaidi kuliko watu wa Tanganyika. Hiyo siyo jinai, wala sijapitiliza kwenye uhuru wa maoni. Huo ni mtazamo wangu. Na anayetaka kujua zaidi, ataniuliza ni kwa namna gani upande mmoja unanufaika kuliko mwingine. Sababu nitakazozitoa, unaweza kuzikubali au kuzikataa. Watu wengine wanaweza kuniunga mkono au kunipinga.

NB: Uhuru wa maoni, hautolewi na Rais, bali umetolewa na katiba ya nchi ambayo Rais aliapa kuilinda. Rais anapoulinda uhuru huo, anatekeleza takwa la katiba, na anatimiza wajibu wake wa kikatiba. Akifanya vinginevyo,.maana yake amekiuka katiba na amekiuka kiapo chake. Rais akikiuka kiapo, anatakiwa kuondolewa kwenye nafasi yake kwa sababu amekiuka mkataba mkuu ambao aliapa kuuishi.
 
'Ahh' kwa sauti ya SSH akiwa Jukwaani! Haijalishi.


Ni Utumwa haswa!
Ni utumwa! unaotokana na rushwa! Kwani Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya rushwa na utumwa.

sasa basi, inakuwa rahisi kwangu kuunganisha nilichounganisha na kichocheo(rushwa) kinachohusishwa na utumwa huu. Na kama kuna kundi la watu ambao wanahisi kuwa nguvu zao za kimadaraka zinakaribia kuvutwa chini ya miguu yao ni za wale waliomo chini ya utawala huu.

Kulazimisha uwekezaji wa D P W kutawamaliza wengi kisiasa na kiroho .

Kwa mujibu wa wanasayansi, rushwa hutumika kama njia ya kupata furaha(kula bata) kwa kutumia au kupitia nguvu.

Watu wanao au vikundi vinavyohusishwa mara nyingi na rushwa hutumia mbinu haramu au za ukandamizaji kupata nguvu au kushika madaraka na kukumbatia ulaji bata..
Mfano mdogo hapa ni kuwa 'tumepewa ruhusa ati kulonga maoni! Tunajua wanayo madaraka ila sasa wanahitaji kubakisha hayo madaraka kwa nguvu bila ya kujali Katiba...Sheria Mama Haswa!




Mimi kwa maoni yangu, naona wameamua kutumia mbinu chafu, hasa ukizingatia kauli za hivi karibuni zilizotolewa na Masauni, Nape na wengine; ni dalili chache tu za kikundi kisichofurahishwa na kinachohusishwa na Utumwa ambao unawezekana kabisa umetokana na rushwa. Kundi ambalo nia yao ni kufanya chochote na lelote lile ili kumaintain (status quo) hali hiyo.

Yaani tuukubali Mkataba kwa shari.

Sasa tumeletewa Gerson M kupigilia misumari.....

Aikambee....Mpaka kieleweke Turudishieni Bandari yetu.​
 
Muoneeni tu huruma. Maana huyo kiumbe hana tofauti na yule Profesa alisema ameokotwa jalalani.

Watu wa aina hii siku zote hufanya kazi kwa kulinda matumbo yao tu (na hasa kwa kumfurahisha yule aliye wateua)!! Na siyo kufanya kazi kwa weredi.
 
Kweli kabisa, nilivyosoma kauli ya Msigwa ndio amezidi kutengeneza matatizo, vile anavyosema wanaopinga mkataba wa bandari na waarabu ni wezi waliokuwa wakinufaika bandarini siku za nyuma, mtu unashangaa, kama.walikuwa wakiwafahamu hao wezi kwanini hawakuwapeleka mahakamani?
 
Back
Top Bottom