masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
- Asema hajui kanuni, amepitwa na wakati
- Mtaturu(katibu CCM Mwanza): heshima ya Kingunge imeshuka
Makamu Mwenyekiti Mstaafu CCM Pius Msekwa amesema tuhuma zinazotolewa na mwanasia mkongwe nchini , Kingunge Ngombale Mwiru dhidi ya vikao vya juu vya chama hazina ukweli wowote.
Msekwa alisema, tatizo linalomkumba Mzee Kinunge ni kuganda kwenye utartibu uliokuwa ukitumika wakati yeye alipokuwa Mjumbe wa Kamati Kuu miaka mingi iliyopita
Aliongeza kuwa Mzee Kingunge hana habari na kanuni zinazotumiaka sasa na hajataka uzifaamu.
Katika hatua nyingine. Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza. Miraji Mtaturu, amesema Mzee Kingunge amejipotezea heshima aliyojijengea kwa miaka mingi kutokana na kauli zake.
"Nashangazwa na kauli iliyotolewa na Mzee Kingunge akiwatuhumu (wazee) kuendesha vikao vya mchakato wa kumpata mgombea urais kwa mizengwe na ajenda ya siri"
"Ukiona mtu anabadilika ujue amenunuliwa...!
Chanzo: Gazeti la Uhuru 1, pg4
MY TAKE
Kingunge anatikisa mzinga wa nyuki!
(mods thanks for the clarity)