Elections 2010 Msanii atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la ilala

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,415
398
oberlin2+023.jpg

Msanii wa Filam Tanzania Juma Chikoka ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi {CCM}.Juma chikoka ambaye ameshiriki movie nyingi kama vile My Dream,Fake Promise,Danger Zone na nyingine nyingi vilevile ni Producer wa movie nchini.Akitangaza nia hiyo Juma Chikoka ama Chopa ambaye ana elimu ya Digrii ya Sanaa katika chuo kikuu cha Bangalore nchini India amesema kuwa "Maendeleo kusuasua katika kila nyanja ndio yaliyomsukuma kama kijana kujitolea kwa hali na mali kuwatumikia wananchi wa Ilala..naomba support yenu wanachi wa ilala na wasanii wenzangu".Huyo ndiyo Juma chikoka tumuunge mkono jamani katika mbio zake hizo za kuwania ubunge

oberlin2+034.jpg

Hapa akiwa masomoni nchini India

kumbe wana siasa ni wengi san Tanzania...............Best of luck kwake
 
Halmashauri ya kichwa chake imemwambia kwamba anaweza ushindani ndani ya chama hiki kwa wakongwe waliopo au anafanya usanii tu?
 
Halmashauri ya kichwa chake imemwambia kwamba anaweza ushindani ndani ya chama hiki kwa wakongwe waliopo au anafanya usanii tu?
hamna lolote mtakafurusa tu huyoo na umaarufu ila hana dhamira ya kweli kama kijana wa kisasa kwa maovu ya chama hicho hicho then anathubutu kupeleka miguu yake huko ........
 
Tumechoka wasanii kuingia katika medani za siasa. Kuna mmoja aliyetoka chuo cha Bagamoyo anatuendesha Watz kwa pua kwa miaka mitano sasa!
 
Nikiona mtu anataka kugombea kupitia CCM huwa siamini sana kuwa mtu huyo anataka ..... kuwatumikia wananchi wa Ilala

Kwa sababu mbili: (a) ni CCM hiyohyo ambayo haikuwatumia watu hao;. (b) hata akichaguliwa, yeye atakuwa nii kijitishari tu mbele ya meli kubwa za CCM, kwa hiyo uwezo wake wa kuibadili CCM ni mdogo sana; hayuko kwenye NEC na hata CC hafiki.
 
Hana nia njema msanii huyo, unatamanije kufanya kazi ****** wakati nia yako ni kuondoa harufu mbaya?

Angegombea kwa vyama hivi vingine isipokuwa CCM ningemwelewa. Tatizo la Tz ni mfumo mbovu wa utawala ulioasisiwa na CCM. na ni vigumu kubadili mfumo huu ukiwa ndani ya CCM kwani CCM inafaidika na mfumo huu mbovu.

Simuungi mkono
 
Ni msanii,kwa hiyo tutegemee usanii pia.kama kuna tofauti basi atuelezee tofauti ya siasa na usanii,mawazo yangu yote sawa tuu.
oberlin2+023.jpg

Msanii wa Filam Tanzania Juma Chikoka ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi {CCM}.Juma chikoka ambaye ameshiriki movie nyingi kama vile My Dream,Fake Promise,Danger Zone na nyingine nyingi vilevile ni Producer wa movie nchini.Akitangaza nia hiyo Juma Chikoka ama Chopa ambaye ana elimu ya Digrii ya Sanaa katika chuo kikuu cha Bangalore nchini India amesema kuwa "Maendeleo kusuasua katika kila nyanja ndio yaliyomsukuma kama kijana kujitolea kwa hali na mali kuwatumikia wananchi wa Ilala..naomba support yenu wanachi wa ilala na wasanii wenzangu".Huyo ndiyo Juma chikoka tumuunge mkono jamani katika mbio zake hizo za kuwania ubunge

oberlin2+034.jpg

Hapa akiwa masomoni nchini India

Mbona Komba ni msanii muacheni aenda huko huko CCM kwa full wasanii kila kitu kwao ni maigizo tu
 
Huyo ni msanii tu, hawezi kwenda mbali.

Ningeshauri kama unania ya kugombea uanze na mambo kadhaa katika sekta yako ya sanaa.

Pigania haki za wasanii wenzako. Je umeshawahi kushiriki katika vuguvugu za kudai,kuelimisha wasanii au kuungana na wasanii wenzako kuondoa , ufisadi ulioingia kunyonya jasho la wasaniii.

Mfano, tumeona jinsi Mr.2 alipovyoporwa tamasha lake!!!

Wenye vyombo vya habari kuwa ndio promoters, producers wa kazi za sanaa, na kutumia nafasi zao kupendelea kazi za wasanii ambao wana mahusiano nao?

Sina haja ya kutoa mifano, inaeleweka katika radio za bongo na sasa itahamia katika luninga.

Kwanini kila mtu anataka kwenda kuwa mbunge? ati ninataka kupeleka maendeleo, kuleta mabadiliko, maendeleo!! Mbona yapo maeneo anuai ambayo mngeanzia, ikithibitika kweli uwezo na nia mnazo, basi huhitaji kusema sana, kwani unakuwa unao mtaji tayari, wananchi wana track record yako.
 
Hivi siku hizi anybody can become a politician?? Duh hata mimi basi itabidi nianze kugombea ubunge kwenye jimbo za huku Arusha, lakini seriously hamna hata requirement ya a degree in political sciences?? Naomba mtu anielimishe kwenye haya mambo manake kama Nakaaya anagombea ubunge pia then can any Tom, Dick or Harry do it??????
 
Akiwa Mtanzania ana kila haki na sababu za kugombea ubunge. Ila kwa sababu ni MSANII na kwa kuzingatia degree yake ya sanaa(usanii) ingefaa zaidi akagombee kwenye vyama au kwenye mambo yanayowahusu wasanii ambako atawatumikia vizuri zaidi kuliko kwenye mambo SIASA ambako uwezekana ya kuwaletea USANII wapiga kura wa jimbo la ILALA ni mkubwa sana.
 
Bora angegombea Mr 2, ana a lot of WASHABIKI Mr 2 uko wapi? 2ngaza nia 2takupa kura
 
Back
Top Bottom