Msando awaweka mezani Gigy Money na Amber Lulu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,505
9,286
Mwanasheria machachari na kipenzi cha wasanii wengi Albert Msando ambaye mara nyingi hujitokeza kuwatetea kwenye masuala ya kisheria, amefunguka kuhusu kuwa karibu na Gigy Money na Amber Lulu, ikiwa mmoja wao alishampa skendo chafu.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio, Albert Msando amesema anawakubali wasanii hao kwa sababu ni mabinti ambao wanapigana kupambana na maisha.

"Bado nawakubali kama wasanii, nawakubali kama watu ambao wanapambana kwenye maisha, kwa sababu ni wapiganaji, unajua kwenye maisha kuna njia nyingi ambazo ukipambana unaweza kufikia malengo yako, na ni mabinti ambao wanafanya vizuri kwenye kile ambacho wanakifanya", alisema Albert Msando.

Albert Msando aliwahi kupata na kashfa ya kuwa na mahusiano na msanii Gigy Money ambaye ni maarufu kwa kupiga picha za utupu, kitendo kilichomsababishia kuachia ngazi nafasi yake ya mshauri wa masuala ya kisheria katika chama cha ACT -Wazalendo .


EATV
 
Msando bwana.. eti anawapenda kwasababu ni mabinti wanaopambana na maisha..
Wanapambana na maisha kupitia uuzaji wa papuchi sio..!!
 
Huyu nae lofa tu. Watu wanapiga kimyakimya yeye mpaka ajichoreshe Instagram.
 
Back
Top Bottom