Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi, atambulisha kampeni ya Amani kuelekea uchaguzi Mkuu

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, pamoja na majukumu yake ya msingi, inayo pia jukumu la kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba. Ukuaji wa demokrasia hauwezi kuwepo kama wananchi ambao ndio wafuasi wa vyama vya siasa wanakuwa na uelewa mdogo juu ya ushiriki wao kwenye siasa za kistarabu na zenye staha.
Wakuu,

Leo Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi, leo ameitisha mkutano na waandishi wa habari asubuhi ya leo kutambulisha kampeni ya amani iitwayo "Amani Yetu Fahari Yetu".

Mkutano huu unafanyika hapa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama, Pia nitawaletea kile kinachoendelea moja kwa moja hadi atakapomaliza kuzungumza.

Karibuni.

================

Anaanza kuongea, anasema Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini pamoja na majukumu mengine yake ya msingi, inayo pia jukumu la kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria.

attachment.php



Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi akiwa na Mrisho Mpoto na Christina Shusho

Anasema kwa kawaida amezoea kuzungumza lakini kwa leo atasoma tamko lake atakaolitoa ili jumbe ufike kwa hadhira kama inavyokusudiwa kwamaana yeye kama msajili yeye ndiye anayevisajili lakini kama vitaharibu jambo lolote yeye ndiye anayehusika/kulaumiwa.

Ujumbe wake wa leo umejikita katika Amani Yetu, Fahari yetu, anawatambulisha Mrisho Mpoto na Christna Shusho na kwamba wao watazungumza baada ya yeye kumaliza kuongea kama mabalozi wa kampeni hii.

Anasema kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba. Ukuaji wa demokrasia hauwezi kuwepo kama wananchi ambao ndio wafuasi wa vyama vya siasa wanakuwa na uelewa mdogo juu ya ushiriki wao kwenye siasa za kistarabu na zenye staha.

-Anasema mbali na tahadhari zinazotolewa katika kipindi hiki cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa Amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa.

-Makundi hayo yanadiriki Kutoa maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana hata kujeruhi makundi mengine ambayo siyo ya upande wao.

-Hivyo, hali hii budi iachwe mara moja ili kuiweka nchi yetu ya Tanzania katika hali ya amani na kuiepusha nchi yetu kuingia kwenye vurugu, mfarakano na machafuko yasiyokuwa na ulazima wa kutokea.

-Ni vyema Watanzania tutambue kwamba utofauti wa itikadi wa vyama ndio ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na kufanya siasa za kistaarabu.

-Anaeleza kuwa kipindi hiki ni cha mpito tu tusikiruhusu kikavuruga amani yetu kwani kuna maisha baada ya uchaguzi na mwisho wa uchaguzi huu ndio mwanzo wa chaguzi zingine kama hizi.

-Kila mmoja wetu kwa nafasi yake hajachelewa kuhakikisha kuwa nchi yetu inabaki salama.

-Kutovumiliana kwa utofauti wetu wa itikadi za kisiasa kunaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kupata athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi, njaa na maradhi.

Anafafanua kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaamini kuwa, Viongozi wa kisiasa wanao ushawishi mkubwa kwa wafuasi na mashabiki wa vyama vyao. Tumieni nafasi hii kusisitiza Amani.

-Dhamana ya nchi hii iko mikononi mwenu, ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa letu la Tanzania ama italiingiza taifa katika vurugu na mfarakano.

-Anaasa na kuwataka viongozi wote wa Vyama vya Siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa Amani.

-Tumieni vyema dhamana ya uongozi mliopewa na mwenyezi Mungu kuivusha salama Tanzania yetu.

-Anatoa rai kwa Waaandishi wa Habari, kwamba watumie kalamu zao vyema kuhubiri Amani.

-Anawataka kuwa waepuke kuandika habari za uchochezi bali wasaidieni Watanzania kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya maamuzi kuchagua viongozi wao.

-Msikubali kalamu zenu zikawa chanzo cha mfarakano na vurugu bali ziwafanye muwe mabalozi wazuri wa amani.

-Mwisho natoa wito kwa watanzania wote. Dumisheni Amani na kamwe tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na uvunjifu wa Amani.

-Kumbuka kuna maisha baada ya uchaguzi na Amani ya Nchi yetu ni fahari yetu sote.

-Sisi tunasisitiza kudumisha amani, hatufungamani na chama chochote, sasa Mpoto na Christina Shusho, tumewaomba wajitolee kusaidia kueneza amani.

-Mnaweza kusema ni kwanini tumeanza leo, hii ni mkakati tu, tumeamua tutumie mabalozi japo umebaki muda mchache ili kufanyika kwa uchaguzi,.

-Utitiri wa wasimamizi wa uchaguzi nchini ni kwasababu wanajua Tanzania ni nchi ya amani

Jaji Mutungi amemaliza kuzungumza.


Mpoto anazungumza.

-Kokote duniani kinachovuruga amani ni kalamu na sauti, ndugu zangu waandishi wa habari, tuisimamie nchi yetu, watu wanazalisha silaaha ili mambo yakivurugika waingie nchini na wafanye mambo yao.

-Tujitahidi kuelimishawananchi ili tunu tuliyo nayo iendelee kudumu

attachment.php


Christina Shusho
, anasema ni wakati wake kwa moyo wa dhati amekubali kuitumikia nchi yake.

-Naahidi kuitumikia nchi yangu bila tamaa, sina chama na sina mpango wa kuhubiri chama bali nitamhubiri Kristo kwa Watanzania ili hata tukivuka mipaka tutunze heshima yetu.

-Nawaombeni mtakapowaona Mpoto au mimi na Msajili wa siasa tusiwachukie bali tuwapende na kuwaunga mkono.

Jaji Mutungi anaulizwa maswali, kuwa ni kwanini Ofisi yake haikemei viashiria vya uvunjifu wa amani ambayo vimeanza kujitokeza nchini?

-Anajibu kwa kusema "Watu wanshindwa kutofautisha majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa.
-Anasema Ofisi yake haijawahi kupokea malalamiko ya aina yoyote hadi sasa kwa kuwa yeye ndio msemaji wa mwisho na pia hata vyama vya siasa vinajua Ofisi yake ina jukumu gani na kwamba malalamiko mengi ambayo yanaweza kutolewa yatatatuliwa na NEC.

Amemaliza kuzungumza na waandishi wa habari wanajiandaa kuondoka.
HOTUBA YA UFUNGUZI YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA NEW AFRICA HOTEL TAREHE

12/10/2015.


Viongozi wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi, Waheshimiwa Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Inspekta Jenerali wa Polisi, Msajili wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Serikali, Watendaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Demokrasia (DEP), Watendaji wa Tume, Waandishi wa Habari, Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,Pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yenu kisiasa ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa ni Wadau muhimu wa Uchaguzi ambapo mkishirikiana kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.Viongozi wa Vyama vya Siasa,Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii, Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii nzima ya watanzaniaViongozi wa Vyama Vya SiasaKuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 64,736, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 156 na Zanzibar ni Vituo 1,580.

Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500. Hata hivyo Kituo kinapokuwa na wapiga Kura zaidi ya 500 kinabidi kigawanywe ili viwe viwili yaani Kituo "A" na Kituo "B" na namba ya Wapiga Kura itakuwa nusu kwa nusu.

Wapiga Kura wanashauriwa kwenda katika vituo walivyojiandikishia kupiga kura siku nane (8) kabla ya siku ya kupiga kura ili kuweza kujua Vituo vyao halisi vya kupigia kura. Sambamba na hilo wananchi wataweza kupata taarifa zao zilizoko kwenye kanzidata (Database) kwa kutumia simu zao za kiganjani kupitia ujumbe mfupi wa maneno ‘sms' bila wao kulazimika kufika vituoni, namba hiyo ni *152*00# na kufuata maelekezo. Au kupitia Tovuti ya Tume ambayo ni (www.nec.go.tz) Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imekuwa ikifuatilia kampeni za Vyama vyenu vya Siasa, hata hivyo Tume inasikitika kuona kuwa baadhi ya Vyama vya Siasa vimekuwa vikitumia majukwaa yao vibaya. Tume kwa namna ya pekee inawaomba katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kutumia nafasi zenu majukwaani kuelezea sera za Vyama Vyenu ili kuweza kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi baada ya kuwa na taarifa sahihi.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imekuwa ikisikia katika vyombo vya Habari malalamiko mengi kuhusu uvunjifu wa maadili ya Uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni, naomba nitumie nafasi hii kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa kupeleka malalamiko yenu katika kamati za maadili na si kukimbilia katika Vyombo vya Habari kama ambavyo baadhi ya Vyama vya Siasa na Wagombea mmekuwa mkifanya.Viongozi wa Vyama Vya SiasaTume inawaomba kuepuka kutoa taarifa na shutuma sisizo sahihi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala yake mjikite katika kufikisha taarifa zilizo sahihi na zilizokusudiwa kwa Wafuasi wenu na wananchi wote kwa jumla, na pia kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.Viongozi wa Vyama Vya Siasa,Tume imejipanga kuhakikisha kila Mpiga kura mwenye sifa za Kupiga Kura anapiga Kura yake pasipo kubughudhiwa.

Ili kuhakikisha jambo hili linafanyika kwa ufanisi, Tume imetoa maelekezo kwa Makarani waongozaji vituoni kutoa upendeleo kwa watu wanaoishi na Ulemavu ili kuwasaidia waweze kupiga kura. Kwa wale wasioona Tume imeandaa kifaa maalumu cha nukta nundu ‘Tactile Ballot Folder' ambayo itawasaidia katika upigaji kura kwa urahisi. Viongozi wa Vyama Vya SiasaBaadhi ya wagombea wamekuwa wakiwashawawishi Wapiga Kura wao kutoondoka katika Vituo vya Kupigia Kura baada ya kumaliza zoezi la Upigaji Kura, naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kinasema nanukuu"Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura katika au ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita 200 ya jengo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi." mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kinasema, nanukuu:"Hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa na umma ndani ya umbali wa mita tatu ya mlango wowote wa kuingilia katika jengo atavaa au kuonyesha au kuonyesha kadi, upendeo au nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi" mwisho wa kunukuu. Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaeleza maana ya njia ya Umma. Nanukuu:"Public way includes any highway, market place, square, street, bridge or other way which is lawfully used by the public" Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa au nafasi kwa wananchi kukusanyika, zinapiga marufuku na kukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasa siku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300 sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.Hivyo niwaase Wanasiasa kuzingatia Sheria na taratibu za uendeshaji wa Uchaguzi, kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania.

Aidha uzoefu unaonyesha kwamba, katika Kampeni zinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa Vyama tofauti wanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa na sehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafa, majeruhi na uharibifu wa mali.Hivyo, endapo kila chama kitaamua kuwaelekeza wafuasi wake kubaki kwenye Vituo vya Kupigia Kura uwezekano wa kutokea vurugu ambazo zinaweza kupelekea kuwatisha, kuwabughudhi, kuwatia hofu na kuwasumbua Wapiga Kura ni mkubwa hivyo kuhujumu zoezi la Upigaji Kura,Zaidi ya hayo, maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu cha 126 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292 na kifungu2.1 cha Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yanasistiza kwamba kiongozi yeyote wa Chama cha Siasa anapaswa kuheshimu na kufuata maagizo yote ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama Vya SiasaKwa kumalizia ninapenda tena kuwashukuru wote kwa kuhudhuria Mkutano huu na Tume inaahidi kuyachukua mawazo yenu na kuyafanyia kazi yale yaliyomo ndani ya uwezo wetu ili kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa amani na utulivu.

Baada ya kusema hayo kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, natamka kuwa Mkutano huu umefunguliwa rasmi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

 

Attachments

  • Msajili.jpg
    Msajili.jpg
    57 KB · Views: 2,812
  • Mpoto akizungumza.jpg
    Mpoto akizungumza.jpg
    44.7 KB · Views: 3,291
Tupo pamoja!

Ila sharti atambue hili:

1. Kukaa mita 200 kulinda kura zetu sio ombi, ni lazima. Kura yangu moja itabadilisha maisha ya watz milioni 50!
2. Wapinzani hawajawahi kupiga watu mabomu, wao ndo wanapigwa that means wao hawana silaha wenye silaha ni CCM
3. Mwaka huu ni UKAWA hata shetani ageuze mbingu kuwa nchi!

Ahsante sana!
 
Baada ya uhakiki wa kazidata ya wapiga kura NEC imesema wapiga kura halali wamebaki milioni 22 na usher badala ya milioni 23 na ushee waliokuwepo katika kazidata ya Tume!

Hivyo idadi imepungu kwa kiasi cha wapiga kura milioni moja ambao imegudulika kuwa na kasoro mbalimbali!

Source: EA Radio
 
Vituo 64,736 Na kila kitu kitahudumia wapiga kura kati ya 450 -500,isizidi 500. Sasa tuchukulie minima possible voters per center 450*64736=29,131,200. Je Hawa ndo waliojiandikisha? Bao la Mkoni hili!! Arguably............
 
Baada ya uhakiki wa kazidata ya wapiga kura NEC imesema wapiga kura halali wamebaki milioni 22 na usher badala ya milioni 23 na ushee waliokuwepo katika kazidata ya Tume!

Hivyo idadi imepungu kwa kiasi cha wapiga kura milioni moja ambao imegudulika kuwa na kasoro mbalimbali!

Source: EA Radio

Hakika nimeamini moderators wengine ni mburula na vodafasta kweli kweli!!

Uzi wangu huu na kampeni ya amani wapi na wapi?!
 
Wananchi wanataka mabadiliko hukiwazinguwa hawatakubali.na mzee wa busara na timu yake ndio wenye sauti ya mwisho ya nchi hii wakisema tume kubali tumeshindwa .hitakuwa safi sana nahomba hiwe hivyo.mungu ibariki tanzania amani hidumu tanzania. Naipenda nchi yangu. Mungu tusahidie
 
Vituo 64,736 Na kila kitu kitahudumia wapiga kura kati ya 450 -500,isizidi 500. Sasa tuchukulie minima possible voters per center 450*64736=29,131,200. Je Hawa ndo waliojiandikisha? Bao la Mkoni hili!! Arguably............

Hesabu ngumu sana.......zitakua D za O'level hizi.
 
Hesabu ngumu sana.......zitakua D za O'level hizi.
You're a disgrace dude. Nitake radhi. You're nowhere around my Algorithm prowess.
Tume imesema "Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500." Na vituo umeambiwa vipo 64,736. Kutoka na data hizo hebu nipe total number of Voters.
 
Ninachoshangaa wasemaji wengi ni wanafiki.

Huyu hawezi kuhubiri amani na democrasia bila kuzungumzia haki na sheria.

Unafiki mtupu!
 
Jaji mstaafu Damian lubuva na watendaji wako watanzania tuliwapa heko mlipiruhusu kura za raisi ,wabunge,madiwani zote kubadikwa kituoni.
Kwanini msituruhusu kulinda kura zetu baada ya kupiga ?? Sisi kama wananchi tunaanza kuwa na maswali kichwani sasa kwanini mmesimama kidete kuzuia kulinda kura wakati 2010 lilifanyika hili
Ngoja niseme kidogo kwanini tunataka kulinda kura zetu
Wananchi wanaenda kupiga kura na perception za kuibiwa vichwani mwao,je tukipiga kura then tukiondoka tutawezaje kuwajua mamluki wanaokuja kupiga kura(wapiga kura hewa) tunataka tulinde kura zetu kwa sababu mamluki wote watakao kuja tutaweza kuwajua na roho zetu zikapata amani
Kumbuka chaguzi zilizopita kulikuwa na tuhuma baadhi ya mawakala kuhongwa hela na kubadilisha matokeo kwa mwaka 2015 sisi wananchi tunasema we won't allow this(BIG NO)
Shime NEC tuacheni tulinde kura zetu

Mwanamabadiliko
 
Nilitegemea ufubguke zaidi nani aliwaweka hao mawakala walouza kura zenu ni NEC au CDM??Kwa nn msitafute mnaowaamini??? Hilo jukumu ni lenu usisahau nchi hii inaendeshwa kwa sheria wala siyo SACCOS YA MTEI.. Pia perception ya kuibiwa kura mnayijitahid kuishikia kidedea mnayo ninyi tu??? Hujui hata upande wa pili wanajua jinsi mlivyojiandaa kufanya fujo siku ya uchaguz kwa kisingizio cha kuibiwa kura?? Au unafikir niny ndo mna haki ya kusikilizwa tu na si vinginevyo??? Jilisheni upepo ila mwishowe mtaumbuka sana...ni wenye level ya ufaham kama wako ndo wanaweza kuafiki ujinga wako huo na siyo wenye uelewa na wanaojua maana ya kupiga kura..hiyo DO OR DIE mliyoapishana lazima itawatokea puani tu..niny subirieni tu
 
Kumbuka chaguzi zilizopita kulikuwa na tuhuma baadhi ya mawakala kuhongwa hela na kubadilisha matokeo kwa mwaka 2015 sisi wananchi tunasema we won't allow this(BIG NO)
Shime NEC tuacheni tulinde kura zetu

Mwanamabadiliko

Mwanamadiliko gani kituko.

Unasema mawakala walihongwa.Wakala mwanamadiliko naye huwa anahongwa? Hao mawakala ni wanamabadiliko wenzenu hamuwaamini? Kama hamuwaamini ina maana hamuuamini mfumo unaowaweka hao mawakala ndani ya vyama vyenu.Sasa kama hata huo mfumo wenu tu hamuuamini hayo mabadiliko ya mfumo ilibidi myafanye huko ndani ya vyama vyenu kwanza.(mtoe boriti la mfumo wenu usioaminika unaoteua mawakala wanaohongeka kwanza)

mtawezaje kuleta mabadiliko ya mfumo mwingine wakati huko kwenu tu mfumo wenu wenyewe hamuuamini?


Mawakala ndio walinzi wa kura na wawakilishi wako na hawateuliwi na tume hata siku moja ni vyama husika na wagombea wao.Sasa kama wewe huwaamini hata mawakala wako basi usipige hata kura jilalie tu nyumbani kwako.

Au wewe ndio wale wapiga kelele wasemao tunataka mabadiliko na unazungusha mikono na makalio wakati hujui hata ni mabadiliko gani unayoyataka?
 
Mi nitabaki kituoni mpakieleweke,wanataka kubadili masanduku ya kura
Eneo la kituo ni la wapiga kura tu walio kwenye foleni .Ukipiga kura unatakiwa kuyeyuka eneo hilo.Jeshi la polisi limeshaonya shauri yako!

Wakikudunda polisi hao unaowatetea hutawaona hata kuja kukuwekea dhamana.Watahangaika ndugu zako na wazazi wako wakati wao unaowatetea watakuwa tu wanatoa matamko ya kulaani kwenye vikao na waandishi wa habari kwenye mahoteli makubwa kama BAHARI BEACH nk huku wakitafuna kuku kwa mrija wanapotoa matamko hayo ya kulaani,wakati wewe uko nyang`a nyang`a mahabusu na familia yako ikiwa hata haijui ile nini maana hawana kitu.
 
Mwanamadiliko gani kituko.

Unasema mawakala walihongwa.Wakala mwanamadiliko naye huwa anahongwa? Hao mawakala ni wanamabadiliko wenzenu hamuwaamini? Kama hamuwaamini ina maana hamuuamini mfumo unaowaweka hao mawakala ndani ya vyama vyenu.Sasa kama hata huo mfumo wenu tu hamuuamini hayo mabadiliko ya mfumo ilibidi myafanye huko ndani ya vyama vyenu kwanza.(mtoe boriti la mfumo wenu usioaminika unaoteua mawakala wanaohongeka kwanza)

mtawezaje kuleta mabadiliko ya mfumo mwingine wakati huko kwenu tu mfumo wenu wenyewe hamuuamini?


Mawakala ndio walinzi wa kura na wawakilishi wako na hawateuliwi na tume hata siku moja ni vyama husika na wagombea wao.Sasa kama wewe huwaamini hata mawakala wako basi usipige hata kura jilalie tu nyumbani kwako.

Au wewe ndio wale wapiga kelele wasemao tunataka mabadiliko na unazungusha mikono na makalio wakati hujui hata ni mabadiliko gani unayoyataka?

Wanasema kumjibu mjinga kuna hitaji busara sana sina haja ya kukujibu
 
Back
Top Bottom