Msajili wa Vyama abariki Mbatia kufukuzwa NCCR Mageuzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,799
Ikiwa imepita miezi mitano tangu kuibuka kwa mvutano wa makada ndani ya Chama cha NCCR Mageuzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imebariki kung’olewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia.

Mei 21, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi iliitisha mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu Kurasini na miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kumsimamisha James Mbatia kujihusisha na shughuli za chama.

Hata hivyo, Septemba 24, mkutano mkuu maalum wa NCCR Mageuzi uliofanyika jijini Dodoma ulimvua uanachama James Mbatia na kumfuta uongozi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Angelina Rutairwa.

Mwananchi limeiona barua iliyotoka ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa nchini na kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza ikihalalalisha mabadiliko ya viongozi hao wakuu wa chama hicho kikongwe cha upinzani nchini.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Oktoba 24, msajili ameeleza kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 23, 26, 28 na 31(2) ya Kanuni na Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa, vikao hivyo vya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na katiba ya NCCR Mageuzi.

“Msajili wa Vyama vya Siasa ameridhika kuwa kikao cha halmashauri kuu ya chama chenu cha Septemba 23, kikao cha halmashauri kuu cha Septemba 24 na mkutano mkuu wa Septemba 24 uliofanya mabadiliko ya uongozi na katiba ya chama chenu yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyotolewa na msajili.

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa NCCR (Bara) Joseph Selasini alisema sasa umefika wakati mtu yeyote atakayeongea na kujitambulisha kama kiongozi wa chama kinyume na utaratibu, sheria itafuata mkondo wake.

“Imefika wakati sasa msajili afuate sheria, kuna mkakati uliopo kuhakikisha vurugu ndani ya chama hiki haziishi, tunamwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) kuyafanyia kazi malalamiko yetu,” alisema Selasini.

Kuanzia Novemba 7, alisema chama hicho kitaanza ziara ya kwenda mikoani na kumtaka IGP pamoja na wasaidi wake kushughulikia taarifa zilizopo mezani kwake kwa kuwa maisha yao yapo rehani lich ay akutekeleza wajibu wao wa kikatiba kufanya shughuli halali.

“Baada ya kukamilisha vikao vyetu jijini Dodoma ukiwamo mkutano mkuu, sheria inasema kabla ya mkutano unatakiwa kupeleka taarifa kwa msajili siku 28 kabla ya kufanyika mkutano na tulifanya hivyo,”

“Lakini, siku 14 baada ya mutano unatakiwa kupeleka taarifa ya kilichojiri ambapo sisi tulipeleka taarifa ya mkutano na mabadiliko ya uongozi Septemba 28,” alisema Selasini.

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyesema hayupo ofisini, hata hivyo Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alikiri kuwa barau hiyo imetoka ofisini kwao.

Alipotafutwa Mbatia alisema jambo lolote linapokuwa mahakamani hawezi kulizungumzia kwani hata Bunge lenyewe haliwezi kuzugumzia jambo hilo.

Alisema kwa kitendo kilichofanywa na ofisi ya msajili, ni kuingilia mahakama na akataka wananchi kujifunza ukweli kwamba tawala wa sheria haupo wala kuzingatiwa nchini.

“Mimi niseme tu haya niliyategemea, kama msajili amefanya hivyo, anatangaza kila mtu ajichukulie sheria mkononi, sitaki kuwa sehemu ya kujadili mambo yaliyoko mahakamani,” alisema Mbatia.

Kwa mujibu wa kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho, miongoni mwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mbatia ni pamoja na kuuza mali za chama kinyume na utaratibu yakiwamo mashamba na nyumba zilizopo maeneo tofauti nchini pamoja na kuchochea migogoro ndani ya chama hicho jambo ambalo h alikubaliki kwa mujibu wa katiba yao hata sheria za nchi.

MWANANCHI
 
Mbatia ni mmoja WA watu ambae Hana kabisa uelewa WA siasa.

Alipaswa kujua nguvu yake iko wapi ...kundi lipi lilimpa ubunge na kulisikiliza...badala yake akaanza kulipiga vita kundi lililomsaidia Hadi kumpa ubunge akidhani atapata faida. Leo wamemnyoosha.

Hao anaogombana nao wala sio maadui zake
 
Mbatia kwaheri kwenye siasa rasmi, alipoingia Rais Samia ukaanza kumnanga ukisahau kabisa Samia yuko kundi lililokupa ubunge wa kuteuliwa, ulisaliti wapinzani wenzako ukataka upewe majimbo kadhaa uongoze kambi rasmi ya upinzani ukapewa pesa kwenda mikoani wakaona hauna tena ushawishi na hauna watu wakakupiga pini bado haukuelewa, Mama Tanzania upumzike humuoni mwenzako zitto anayejua kuchanga karata zake vizuri aliumia nao na sasa anakula nao meza moja, umefukuzwa kama mbwa na watu uliowakaribisha mwenyewe, kwaheri Mama Tanzania
 
Halafu kikosi kazi cha akina Zitto ndo kimetoa mapendekezo msajili wa vyama vya siasa awe na mamlaka ya kusimamia chaguzi za vyama kwa hali hii?

Mbatia alifikia hatua ya kupokelewa na wakuu wa mikoa nchi hii leo yuko wapi? Tulimwonya sana hakusikia.

Nakukumbusha tu Vyama vyote vya upinzani waanzilishi ni hao wachaga kwa asilimia kubwa na vyama vyote vilivyowahi kupata nguvu nchini ni vya kwao wachaga sema sio wakabila wamefikisha vyama hivyo maeneo yote nchini
CUF haikuanzishwa na wachaga.

NCCR kama ulifikiri ni Mrema, basi hujui kitu.

CHADEMA ni Bob Makani (sukuma) na rafiki yake Edwin Mtei (chaga).

Au unataka kusema TLP ya Mrema? Maana nilivyokutajia hapo juu ndio vyama vimewahi kuwa super power ya upinzani nchini.

Note: nimeandika tu kwa lengo la kukusahihisha, mimi si muumini wa mambo ya kabila fulani ni kadha wa kadha.
 
Ikiwa imepita miezi mitano tangu kuibuka kwa mvutano wa makada ndani ya Chama cha NCCR Mageuzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imebariki kung’olewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia.

Mei 21, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi iliitisha mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu Kurasini na miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kumsimamisha James Mbatia kujihusisha na shughuli za chama.

Hata hivyo, Septemba 24, mkutano mkuu maalum wa NCCR Mageuzi uliofanyika jijini Dodoma ulimvua uanachama James Mbatia na kumfuta uongozi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Angelina Rutairwa.

Mwananchi limeiona barua iliyotoka ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa nchini na kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza ikihalalalisha mabadiliko ya viongozi hao wakuu wa chama hicho kikongwe cha upinzani nchini.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Oktoba 24, msajili ameeleza kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 23, 26, 28 na 31(2) ya Kanuni na Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa, vikao hivyo vya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na katiba ya NCCR Mageuzi.

“Msajili wa Vyama vya Siasa ameridhika kuwa kikao cha halmashauri kuu ya chama chenu cha Septemba 23, kikao cha halmashauri kuu cha Septemba 24 na mkutano mkuu wa Septemba 24 uliofanya mabadiliko ya uongozi na katiba ya chama chenu yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyotolewa na msajili.

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa NCCR (Bara) Joseph Selasini alisema sasa umefika wakati mtu yeyote atakayeongea na kujitambulisha kama kiongozi wa chama kinyume na utaratibu, sheria itafuata mkondo wake.

“Imefika wakati sasa msajili afuate sheria, kuna mkakati uliopo kuhakikisha vurugu ndani ya chama hiki haziishi, tunamwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) kuyafanyia kazi malalamiko yetu,” alisema Selasini.

Kuanzia Novemba 7, alisema chama hicho kitaanza ziara ya kwenda mikoani na kumtaka IGP pamoja na wasaidi wake kushughulikia taarifa zilizopo mezani kwake kwa kuwa maisha yao yapo rehani lich ay akutekeleza wajibu wao wa kikatiba kufanya shughuli halali.

“Baada ya kukamilisha vikao vyetu jijini Dodoma ukiwamo mkutano mkuu, sheria inasema kabla ya mkutano unatakiwa kupeleka taarifa kwa msajili siku 28 kabla ya kufanyika mkutano na tulifanya hivyo,”

“Lakini, siku 14 baada ya mutano unatakiwa kupeleka taarifa ya kilichojiri ambapo sisi tulipeleka taarifa ya mkutano na mabadiliko ya uongozi Septemba 28,” alisema Selasini.

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyesema hayupo ofisini, hata hivyo Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alikiri kuwa barau hiyo imetoka ofisini kwao.

Alipotafutwa Mbatia alisema jambo lolote linapokuwa mahakamani hawezi kulizungumzia kwani hata Bunge lenyewe haliwezi kuzugumzia jambo hilo.

Alisema kwa kitendo kilichofanywa na ofisi ya msajili, ni kuingilia mahakama na akataka wananchi kujifunza ukweli kwamba tawala wa sheria haupo wala kuzingatiwa nchini.

“Mimi niseme tu haya niliyategemea, kama msajili amefanya hivyo, anatangaza kila mtu ajichukulie sheria mkononi, sitaki kuwa sehemu ya kujadili mambo yaliyoko mahakamani,” alisema Mbatia.

Kwa mujibu wa kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho, miongoni mwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mbatia ni pamoja na kuuza mali za chama kinyume na utaratibu yakiwamo mashamba na nyumba zilizopo maeneo tofauti nchini pamoja na kuchochea migogoro ndani ya chama hicho jambo ambalo h alikubaliki kwa mujibu wa katiba yao hata sheria za nchi.

MWANANCHI
Bado chadema napo kunahitajika mabadiliko. Uenyekiti wa kisultani au kiongozi kumiliki chama kama kampuni yake haifai.
Chadema wale wakereketwa watajidai wana imani na mwamba ila ukweli wanamuogopa wamechoshwa na hawana la kufanya kwa ubabe wake. Utasikia 'mwamba tuvushe' ila hawavuki popote.
 
bado Zitto Kabwe.
Zitto ni mwamba kwenye game ya siasa, utasubiri sana. Huyo jamaa huaga hakurupuki. Lema kilasiku anapandikiza chuki kwa Misukule yake, lakini wapi Zitto hakamatiki anazidi kuwachanganya.
 
Bado chadema napo kunahitajika mabadiliko. Uenyekiti wa kisultani au kiongozi kumiliki chama kama kampuni yake haifai.
Chadema wale wakereketwa watajidai wana imani na mwamba ila ukweli wanamuogopa wamechoshwa na hawana la kufanya kwa ubabe wake. Utasikia 'mwamba tuvushe' ila hawavuki popote.
nenda kashangilie ndege iliyobeba bendera ya sensa wewe taga la ccm
 
Ikiwa imepita miezi mitano tangu kuibuka kwa mvutano wa makada ndani ya Chama cha NCCR Mageuzi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imebariki kung’olewa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia.

Mei 21, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi iliitisha mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Jeshi la Wokovu Kurasini na miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kumsimamisha James Mbatia kujihusisha na shughuli za chama.

Hata hivyo, Septemba 24, mkutano mkuu maalum wa NCCR Mageuzi uliofanyika jijini Dodoma ulimvua uanachama James Mbatia na kumfuta uongozi aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Angelina Rutairwa.

Mwananchi limeiona barua iliyotoka ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa nchini na kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza ikihalalalisha mabadiliko ya viongozi hao wakuu wa chama hicho kikongwe cha upinzani nchini.

Katika barua hiyo iliyoandikwa Oktoba 24, msajili ameeleza kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 23, 26, 28 na 31(2) ya Kanuni na Usajili na Ufuatiliaji wa Vyama vya Siasa, vikao hivyo vya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na katiba ya NCCR Mageuzi.

“Msajili wa Vyama vya Siasa ameridhika kuwa kikao cha halmashauri kuu ya chama chenu cha Septemba 23, kikao cha halmashauri kuu cha Septemba 24 na mkutano mkuu wa Septemba 24 uliofanya mabadiliko ya uongozi na katiba ya chama chenu yalifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyotolewa na msajili.

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa NCCR (Bara) Joseph Selasini alisema sasa umefika wakati mtu yeyote atakayeongea na kujitambulisha kama kiongozi wa chama kinyume na utaratibu, sheria itafuata mkondo wake.

“Imefika wakati sasa msajili afuate sheria, kuna mkakati uliopo kuhakikisha vurugu ndani ya chama hiki haziishi, tunamwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) kuyafanyia kazi malalamiko yetu,” alisema Selasini.

Kuanzia Novemba 7, alisema chama hicho kitaanza ziara ya kwenda mikoani na kumtaka IGP pamoja na wasaidi wake kushughulikia taarifa zilizopo mezani kwake kwa kuwa maisha yao yapo rehani lich ay akutekeleza wajibu wao wa kikatiba kufanya shughuli halali.

“Baada ya kukamilisha vikao vyetu jijini Dodoma ukiwamo mkutano mkuu, sheria inasema kabla ya mkutano unatakiwa kupeleka taarifa kwa msajili siku 28 kabla ya kufanyika mkutano na tulifanya hivyo,”

“Lakini, siku 14 baada ya mutano unatakiwa kupeleka taarifa ya kilichojiri ambapo sisi tulipeleka taarifa ya mkutano na mabadiliko ya uongozi Septemba 28,” alisema Selasini.

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi aliyesema hayupo ofisini, hata hivyo Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alikiri kuwa barau hiyo imetoka ofisini kwao.

Alipotafutwa Mbatia alisema jambo lolote linapokuwa mahakamani hawezi kulizungumzia kwani hata Bunge lenyewe haliwezi kuzugumzia jambo hilo.

Alisema kwa kitendo kilichofanywa na ofisi ya msajili, ni kuingilia mahakama na akataka wananchi kujifunza ukweli kwamba tawala wa sheria haupo wala kuzingatiwa nchini.

“Mimi niseme tu haya niliyategemea, kama msajili amefanya hivyo, anatangaza kila mtu ajichukulie sheria mkononi, sitaki kuwa sehemu ya kujadili mambo yaliyoko mahakamani,” alisema Mbatia.

Kwa mujibu wa kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho, miongoni mwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mbatia ni pamoja na kuuza mali za chama kinyume na utaratibu yakiwamo mashamba na nyumba zilizopo maeneo tofauti nchini pamoja na kuchochea migogoro ndani ya chama hicho jambo ambalo h alikubaliki kwa mujibu wa katiba yao hata sheria za nchi.

MWANANCHI
CCM INAPAMBANA KUWEKA MAMLUKI KTK VYAMA VYA UPINZANI KUMPITIA MSAJILI WA VYAMA
 
Usisahu sura ya Katiba mpya kwenye kitabu chako hicho
Nipo mbioni kuandika kitabu chenye jina la: UDIKTETA NDANI YA VYAMA VYA SIASA NI GIZA LA KUFIFISHA DEMOKRASIA
 
Back
Top Bottom