Msaada wa mawazo tafadhari

Mmea Jr

JF-Expert Member
May 20, 2016
551
1,222
Habari zenu wakuu , tafadhari naombeni msaada wa mawazo katika hili tatizo lilomkuta mdogo wangu.

Moja kwa moja kwenye maada . Hapa nyumbani ninapoishi ninaishi na mdogo wangu wa kiume . Lengo la kuishi naye ni ili aweze kunisaidia katika biashara yangu ya duka nililolifungua hapa nyumbani .

Sasa huyu mdogo wangu katika hii biashara ya duka imetokea ameanzisha mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi (beki tatu )wa jirani ya yangu mahusiano ambayo yalikuwa ya siri baina yao .

Sasa katika siku ya jumapili ( tarehe 3/7/. jirani yangu alinifuata na kuniambia kuwa mfanyakazi wake wa kike kamuibia kiasi cha pesa cha shilingi laki nne . Ukweli nilistaajabu na kumpa pole za dhati kabisa huyu jirani yangu na kumuuliza sasa amechukua hatua gani ?.

Akaniambia kutoka na uchunguzi aliyofanya amegundua huyo mfanyakazi wake wa kike (ambaye bado anaishi naye ) ana mahusiano ya kimapenzi na mdogo wangu. Hivyo anahisi baada ya binti huyu kuiba pesa kiasi cha tsh 400,000/= . basi amempa huyu mdogo wangu wa kiume amfichie ( ukweli nilishangaa sana ) .

Ikabidi tumuite mdogo wangu wa kiume na kuumuliza juu ya shutuma zinazomkabili , mdogo wangu kweli kajibu alikuwa ana mahusiano na huyo binti (mfanyakazi wangu ) na katika mahusiano yao mdogo wangu wa kiume ndiyo amewahi kumpa binti tsh 5000/= tu . Na siyo kinyume chake .

Sasa changamoto inakuja hapa huyu jirani yangu moja anatangaza kwa watu kuwa huyu mfanyakazi wake wa kike anayemuhisi kamuibia pesa amempa huyu mdogo wangu wa kiume amfichie , lakini pia aenda mbali zaidi na kuwaambia watu anaenda polisi kumfungulia kijana wangu wa kiume kesi ya wazi , kuwa ameshirikiana na mfanyakazi wake wa kike kumuibia kiasi tsh 400,000/= .

Sasa naombeni ushauri wanaJamiiForums mnishauri ni hatua gani za kuchukua juu ya huyu mtu maana binti wamemuuliza kataa kuwa hajaiba, wamempiga lakini pia binti kagoma pia . Sasa nifanyaje juu ya huyu kiumbe
 
aisee !! mimi sipo tayari kabisaa juu ya huu upuzi huyu jirani nilikuwa na muona ana akili lkn sasa naye namuona kiazii tu maana nimegundua naye ana tabia za uswahili ovyo kabisa huyu mzee.
 
Pole mkuu, uchofu, mambo yote yatakuwa sawa.
 
aisee !! mimi sipo tayari kabisaa juu ya huu upuzi huyu jirani nilikuwa na muona ana akili lkn sasa naye namuona kiazii tu maana nimegundua naye ana tabia za uswahili ovyo kabisa huyu mzee.

Hapana Mkuu usimchukie jirani ana haki ya kulalamika kwani laki 4 ni hela nyingi kwa kuibiwa mara moja

Simtetei ila na yeye hana haki ya kumtuhumu moja kwa moja dogo kuwa kashiriki wizi bila kuwa na uhakika

Anajipalia makaa tu kama sio kweli mdogo wako hajashiriki Basi ataeleza alikozipata hizo habari

Lakini nawe pia usiwe upande wowote bali fanya uatafiti na mdogo wako unamjua vizuri
Kukusaidia duka tu kaanza na mahusiano Sasa huyo si atakufilisi
Au Vipi muozeshe ziende halali
 
Usiwalie yamini beki tatu hashinfwi kufanya hayo. Subiri aende polisi utajua huyo jirani kayatolea wapi hayo maneno.
 
Hapana Mkuu usimchukie jirani ana haki ya kulalamika kwani laki 4 ni hela nyingi kwa kuibiwa mara moja

Simtetei ila na yeye hana haki ya kumtuhumu moja kwa moja dogo kuwa kashiriki wizi bila kuwa na uhakika

Anajipalia makaa tu kama sio kweli mdogo wako hajashiriki Basi ataeleza alikozipata hizo habari

Lakini nawe pia usiwe upande wowote bali fanya uatafiti na mdogo wako unamjua vizuri
Kukusaidia duka tu kaanza na mahusiano Sasa huyo si atakufilisi
Au Vipi muozeshe ziende halali
nisiwe muongo , kusema ntampenda huyu jirani siwezi, dogo nimekaa naye nimeongea naye mbaka nimemtishia kumrudisha nyumbani , kasema ananiambia ukweli toka moyoni huyo binti hajampatia pesa.

binti wamempiga ili aseme amekubali , wanamuuliza pesa kaweka wapi hasemi , wamempeleka polisi binti anasema yeye alikubali ili waache kumpiga tu ila ukweli hakuna pesa alizochukua .

kingine nilichosikia , ni kuwa huyu binti aliaga na kudai ifikapo tarehe 10 anataka aende nyumbani kwa wazaz wake hivyo alikuwa anasubilia msharaha wake. Sasa hapa nimewaza sana kwmba inamaana huyu jirani kaliibua ili sekeseke ili amdhurumu huyu binti haki yake au ili ajipatie pesa kwa nyia haramu ya kusingizia kuwa binti kakabidhi pesa kwa mdogo wangu .

both ways. Sikubliani na anachokifanya huyu jirani yangu ukweli kichwa changu kinafikiria mengi sana juu ya huyu mtu.
 
Huyo jirani kabila gani?
 
hyu binti eneo nalo ishi ana ndugu (dada yake ) . inakuwaje jirani kashindwa kufikiria kuwa binti yake wa kazi baada ya kuiba pesa alipeleka kwa dada , lakin yeye moja kwa moja ana mshuku mdogo wangu ?.. au kwa vile dogo yupo dukani basi anaamini hapa pesa zipo kwamba ntaogopa ntalipa mimi hzo pesa anazodai kaibiwa
 
nisiwe muongo , kusema ntampenda huyu jirani siwezi, dogo nimekaa naye nimeongea naye mbaka nimemtishia kumrudisha nyumbani , kasema ananiambia ukweli toka moyoni huyo binti hajampatia pesa.

binti wamempiga ili aseme amekubali , wanamuuliza pesa kaweka wapi hasemi , wamempeleka polisi binti anasema yeye alikubali ili waache kumpiga tu ila ukweli hakuna pesa alizochukua .

kingine nilichosikia , ni kuwa huyu binti aliaga na kudai ifikapo tarehe 10 anataka aende nyumbani kwa wazaz wake hivyo alikuwa anasubilia msharaha wake. Sasa hapa nimewaza sana kwmba inamaana huyu jirani kaliibua ili sekeseke ili amdhurumu huyu binti haki yake au ili ajipatie pesa kwa nyia haramu ya kusingizia kuwa binti kakabidhi pesa kwa mdogo wangu .

both ways. Sikubliani na anachokifanya huyu jirani yangu ukweli kichwa changu kinafikiria mengi sana juu ya huyu mtu.

Mkuu nimekuelewa sana sasa
Na kuhusu huyo msichana naona hajaiba chochote kama amepigwa sana na hajakubali kosa Basi huyo jirani atafute mchawi wake

Na wewe mchane live asikufuate fuate akatafute sababu zingine
Kama ni hivyo unavyowaza inaweza kuwa kweli anamdhulumu mshahara wake

Simamia haki ipatikane hata kama ni polisi nae ageuziwe kibao Mbona kazi rahisi hiyo
 
Huyo jirani yako kweli hana akili hata kidogo mpaka anafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa kutumia hisia
 
Habari zenu wakuu , tafadhari naombeni msaada wa mawazo katika hili tatizo lilomkuta mdogo wangu.

Moja kwa moja kwenye maada . Hapa nyumbani ninapoishi ninaishi na mdogo wangu wa kiume . Lengo la kuishi naye ni ili aweze kunisaidia katika biashara yangu ya duka nililolifungua hapa nyumbani .

Sasa huyu mdogo wangu katika hii biashara ya duka imetokea ameanzisha mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi (beki tatu )wa jirani ya yangu mahusiano ambayo yalikuwa ya siri baina yao .

Sasa katika siku ya jumapili ( tarehe 3/7/. jirani yangu alinifuata na kuniambia kuwa mfanyakazi wake wa kike kamuibia kiasi cha pesa cha shilingi laki nne . Ukweli nilistaajabu na kumpa pole za dhati kabisa huyu jirani yangu na kumuuliza sasa amechukua hatua gani ?.

Akaniambia kutoka na uchunguzi aliyofanya amegundua huyo mfanyakazi wake wa kike (ambaye bado anaishi naye ) ana mahusiano ya kimapenzi na mdogo wangu. Hivyo anahisi baada ya binti huyu kuiba pesa kiasi cha tsh 400,000/= . basi amempa huyu mdogo wangu wa kiume amfichie ( ukweli nilishangaa sana ) .

Ikabidi tumuite mdogo wangu wa kiume na kuumuliza juu ya shutuma zinazomkabili , mdogo wangu kweli kajibu alikuwa ana mahusiano na huyo binti (mfanyakazi wangu ) na katika mahusiano yao mdogo wangu wa kiume ndiyo amewahi kumpa binti tsh 5000/= tu . Na siyo kinyume chake .

Sasa changamoto inakuja hapa huyu jirani yangu moja anatangaza kwa watu kuwa huyu mfanyakazi wake wa kike anayemuhisi kamuibia pesa amempa huyu mdogo wangu wa kiume amfichie , lakini pia aenda mbali zaidi na kuwaambia watu anaenda polisi kumfungulia kijana wangu wa kiume kesi ya wazi , kuwa ameshirikiana na mfanyakazi wake wa kike kumuibia kiasi tsh 400,000/= .

Sasa naombeni ushauri wanaJamiiForums mnishauri ni hatua gani za kuchukua juu ya huyu mtu maana binti wamemuuliza kataa kuwa hajaiba, wamempiga lakini pia binti kagoma pia . Sasa nifanyaje juu ya huyu kiumbe
Aende polisi
 
aisee !! mimi sipo tayari kabisaa juu ya huu upuzi huyu jirani nilikuwa na muona ana akili lkn sasa naye namuona kiazii tu maana nimegundua naye ana tabia za uswahili ovyo kabisa huyu mzee.
Mambo rahisi sana kwa waswahili hao. Tafuta laki 4, mwite jirani na wahusika, kijana na beki tatu na mjumbe halafu weka fungu la hela katika kitambaa cheusi juu ya meza. Utaanza na stori kama ilivyoletwa, na utasema kuwa unailipa ila kama kuna anayefanya dhuluma hapa, litakalompata shauri yake.
 
Inawezekan pia hajaibiwa hyo hela ni vile amejua kuwa mdg wako anatoka na binti akatafuta pa kutokea..mjini mipango hebu fatilia vzr
 
Huu mtindo wa mabosi uchwara kuwadhulumu mabinti wa kazi sjui utaisha lini?

Binti akisema tu anataka kuondoka wataanza zengwe mara ulivunja kikombe mara bikini ya mama mwenyenyumba ulikata mkanda wa katikati wakat unaosha kwa hyo tunakukata katka mshahara wako

Kifupi huyo dogo alikuwa anakopwa mshahara wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom