Mpigamsuli
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 3,885
- 575
wana jf ninaomba mnipe tafsiri ya maneno ,rajisi,muamala,gombo,mrabaha ,msaada tafadhali,by.mpigamsulioriginal
wana jf ninaomba mnipe tafsiri ya maneno
- rajisi
- muamala
- gombo
- mrabaha
msaada tafadhali,by.mpigamsulioriginal
mpigamsuli
MRAHABA:
1. mrabaha = 1. royalty.
2. mrabaha = 2. proceeds, returns, profit.
GOMBO:
1. gombo = 1. sheet, leaf of a book.
2. gombo = 2. (hutumika sana Mwambao wa Afrika ya Mashariki) offering ceremony.
3. gombo.a = 3. redeem: Ali aligomboa redio yake he redeemed his radio.
Maneno yanayoendana na hiyo namba 3 ni gombolea, (tdew) gombolewa; (tdk)gomboka; (tdn) gomboana; (tds) gombosha.
MUAMALA
1. muamala = 1. one's good relations with others.
2. muamala = 2. business relations.
N.B:
Kuna neno muamala ambalo pia linatumiwa na Kampuni za simu ... kama M-Pesa au Tigo ... huwa wanasema Muamala umekubaliwa au hautoshi ... nafikiri unafahamu.
RAJISI:
Rajisi = Sajili
Kisawe (neno linalofanana katika matumizi) cha kusajili ni kurajisi. Neno rajisi halitumiki sana lakini neno sanifu na linakubalika kutumika.
Tanapata mrajisi/msajili katika wizara, mashirika na kampuni.
Nafikiri mkuu mpigamsuli pia na Gwankaja Gwakilingo umenipata hapo!