johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 725
- 710
Msaada wa kumshitaki mgombea huyu.
Mimi nikiwa ni mkazi wa jiji la Mwanza nakuja haopa jamvini kutafuta msaada ili kuchukuahatua stahiki dhidi ya kitendo kisichofaa cha Mgombea ubunge wa Jimbo la Nyamagana pamoja na washirika wake kwa kuingilia mawasiliano yangu bila ridhaa yangu.
Mnamo oktoba 15 mwaka 2015 muda wa saa tano na dakuika 15 asubuhi nilipokea ujumbe kutoka kwa mtu anayejitambulisha kuwa ni Stanslaus Mabula wenye lengo la kunishawishi nimpigie kura ya ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Ingawa Ujumbe huo aukusema huyo ni mgombea kupitia chama gani lakini ni ukweli uliowazi kuwa mgombea mwenye jina hilo anatokea CCM.
Ujumbe huo umenisababishia usumbufu kwani muda huo nilikuwa natekeleza majukumu yangu lakini nikalazimika kusitisha na kusoma ujumbe huo ambao sikutarajia au kuutaka. Pamoja na matumizi ya njia za kisasa za mawasiliano kufanya kampeni nimeumizwa na ujumbe huo kwani ni ushahidi kuwa Namba zetu za simu SIO SALAMA na mtu anaweza kuzipata na kuzitumia bila kuchukuliwa hatua.
Nimejaribu kuwasiliana na kampuni ya VODACOM ambao ndio naitumia kwa mawasiliano yangu lakini wamesema hawahusiki kutoa namba za wateja wao kwani hicho ni kitu cha siri kati yao na mteja. Suala kubwa ninalojiuliza ni kuwa wapi mtu huyu na washirika wake wake wamepata namba yangu?
Ujumbe uliotumwa umemlenga kijana, akiwa na maana ya kuwa na tgaarifa sahihi za mlengwa kwani nimewauliza wazee kadhaa ambao wameeleza kuwa hawajapata ujumbe huo. Hawa watu wamepata wapi namba yangu. Kuna usalama kweli wa kuendelea kutumia mitando hii ya simu?, kwanini waingilie mawasiliano yangu? Kama sasa wameweza kufanya hivi, huko nyuma wamefanya nini bila mimi kufahamu?, ile sharia ya makosa ya mitandao inawahusu wakina nani?
Naomba kupitia jukwaa hili nipate msaada wa kulifikisha suala hili mahakamani ili iwe fundisho kwa Mgombea huyo na washirika wake kwa kuijngilia mawasiliano yangu