Mimi ni mtumishi wa sekaliri, nipo masomoni kwa sasa lakini mara tu baada ya kuanza masomo yangu nilikatiwa mshahara lakini nashanga 'salary slip' zinaendelea kutoka huku mshahara nikiwa sipati. Walinikatia huo mshahara baada ya mimi kwenda masomoni huku nikiwa sina barua ya ruhusa ingawa nilikuwa na sifa ya kupata ruhusa. Je hizi fedha zangu zinaenda wapi wakati zinatoka kila mwezi huku mimi nikiishia kupata salary slip ambapo pesa haiingizwi kwenye akaunti yangu? Je ninauwezo wa kupata pesa yangu yote pindi nikimaliza masomo yangu na kurudi kazini kwa vile kwasasa namalizia mwaka wangu wa mwisho? Naombeni ushauri wenu!