The FaMa
Senior Member
- Oct 6, 2011
- 125
- 27
Wakuu, salaamu.
Ninaomba msaada wenu wa kisheria au ushauri kisheria kwa jambo hili. Nimeombwa ushauri nami si Mwanasheria, sina ushauri sahihi wa kutoa kwa mtu aliyeniomba ushauri huo.
Jambo lenyewe liko hivi;(mfano) Mimi ninaishi Mwanza, ninahitaji kununua gari toka kwa mtu anayefanya biashara hiyo huko Dar. Bei tuliyoafikiana ni TSh. 7,000,000/- (7.0m/-). Nikaomba nimlipe kwa awamu wakati naye akifanya mchakato wa kuliweka sawa hilo gari (usajili nk). Kwa vile akaunti zetu zipo katika benki tofauti, huyo muuzaji alinipatia akaunti namba ya rafiki yake ambaye iko benki moja na yangu ili iwe rahisi kwangu kumtumia malipo hayo ya awamu ya kwanza. Hivyo, malipo ya kwanza ya TSh. 5,000,000/- (5.0m/-) yakafanyika kupitia akaunti ya huyo rafiki yake muuzaji.
Baada ya muda (say mwezi), nikafika Dar na kuonana na muuzaji katika moja ya Ofisi (siyo yake) na kumkabidhi kiasi cha pesa kilichosalia pasipo kuandikishana popote (yaani kuaminiana) na muuzaji huyo kunieleza kuwa gari husika litakuwa tayari after 2 weeks toka siku hiyo.
Sasa, baada ya hizo 2weeks kupita, huyo muuzaji akaanza kutoa sababu mbalimbali za kwa nini ameshindwa kunipatia hilo gari na kunitaka niendelee kuwa na subira. Tumeendelea kuwasiliana kwa simu (kwa kuwa mimi niko Mwanza na yeye yuko Dar) na kila mara ananiomba samahani kwa kunicheleweshea gari na kwamba anaendelea kuhangaika kulitoa huko bandarini.
Baada ya muda wa miezi 6 kupita pasipo kupata gari yangu, niliamua kumfuata Dar na kumtaka anirejeshee kiasi changu cha pesa nilichompatia (TSh. 7.0m/-). Hivyo, aliniomba tukutane katika ofisi moja ya ndugu yake na kuniomba nimpe muda wa miezi mitatu ya kunirejeshea fedha zangu. Nilikubali na tukaandikishana hapo Ofisini kwa ndugu yake na huyo ndugu yake akiwa shahidi wa makubaliano yetu hayo ya mimi kurejeshewa fedha zangu. Aidha, wakati tukiwasiliana kwa simu (messages na calls), nilikuwa nikihifadhi messages zote tulizokuwa tukiwasiliana wakati nafuatilia gari langu. Pia, siku hiyo ya makubaliano ya kurejeshewa fedha zangu, nilikuwa nikirekodi mazungumzo yetu pasipo wao kujua. Hivyo, ninazo messages na rekodi ya mazungumzo yetu pamoja na ile karatasi ya kuwekea pesa (pay in slip) kwa yale malipo ya kwanza kupitia akaunti ile ya rafiki yake na makubaliano ya kurejeshewa pesa zangu tuliyoandikishana.
Sasa, tatizo nililoombwa ushauri hapa ni, endapo huyo muuzaji akakiuka makubaliano ya kumrejeshea jamaa fedha zake kama walivyoandikishana, je;
1. Atakuwa na nguvu kisheria kumshitaki kudai fedha zake (kwamba anao ushahidi wa kutosha (sufficient evidence))?
2. Kama ndiyo, atamshitaki katika mahakama ipi-ya mwanzo au wilaya au mkazi?
3. Atamshitaki katika Mahakama ya wapi - Mwanza au Dar?
4. Anaweza kuweka Wakili?
Naombeni ushauri ili nimfikishie huyu mtu, kwani ana wasiwasi kuwa huenda ndo keshapoteza fedha zake.
Ni hayo tu, natanguliza shukurani.