mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,576
- 9,816
Ukienda kununua bidhaa ama huduma katika baadhi ya maeneo ya biashara, katika eneo la kuegesha magari anakutana na kibao chenye maneno 'Parking at Your Own Risk"
Hii ikiwa na maana ya kuwa muuzaji wa bidhaa ama huduma hawajibiki kwa ulinzi wala usalama wa gari la mteja wake ambaye amekwenda kufuata mahitaji yake katika eneo lake la biashara.
Mathalani mimi ni mgonjwa, na nimekwenda hospitali kwa ajili ya kupata matibabu. Taratibu za kitabibu zinafahamika, toka katika kujiandikisha, kumuona daktari, uchukuaji wa vipimo, kupata matibabu husika, mpaka kupewa dawa za ugonjwa unaonisumbua. Je, katika muda wote huo wa kusubiri kupewa huduma hizo za kiafya, ni tafsiri ya kisheria kuwa ulinzi na usalama wa gari ni jukumu langu mimi mwenyewe?
Je, Kisheria imekaaje, endapo nikakuta gari langu limeibiwa, baadhi ya vifaa kuibiwa, limegongwa, au kuwaka moto? Mwenye biashara hana jukumu lolote la kisheria kama shahidi wangu muhimu?
Je, kupitia maelezo ya kibao hicho, mwenye biashara hawajibiki wala kuguswa kisheria kwa janga lolote lile ambalo linaweza kutokea katika gari la mteja wake, na linalotokea katika eneo lake la biashara, na pia la mteja wake akiwa katika mchakato wa kupata huduma yake?