Msaada wa internet connection

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Wakuu habari za hapa.
Mimi niko hapa Moshi najaribu kuunganisha maisha na gundi ya maji. Hivi karibuni kijana wangu kanishauri nifungue internet cafe. Nimezunguka na nimepata sehemu. Leo alikuwa busy na kununua computer used of course. Kwa sent nilizompa kapata ka 9 hivi. Nimempa na dell yangu mpya so jumla anazo 10. Kazi kubwa ni connection au server gani atumie. Tutakuwa na kikao leo usiku kama nitawahi ama kesho asubuhi ili nimkamilishie ofice yake. Ana imani kuwa ataweza kunilipa fedha zangu maana namkopesha. Nitumie kampuni gani iliyo fast? Kwetu huku ukiwa na internet fast utafanya kazi mpaka uchoke. Masaada wenu na ushauri unashukuriwa kabla.
Eeka Mangi
 
Tumia ttcl...ndio itakulipa ingawa mmm link inaweza kuwa down kwa ck 3 wala hawastuki hakuna anaejali hata
 
Mkuu sina ujuzi sana kwa hili ila kama mkonga wa mawasiliano huko bongo ushaanza kazi basi unganisha hapo. Vinginevyo najua watakuja wataalam hapa jamvini wakupe data kamili!
 
Check na kampuni zote ili ujue rate zao na malipo.
Nashauri uchukue ile ya kulipa kwa mwezi badala ya kununua bundles
Watembelee Customer service zao utapata mengi sana
 
Wakuu habari za hapa.
Mimi niko hapa Moshi najaribu kuunganisha maisha na gundi ya maji. Hivi karibuni kijana wangu kanishauri nifungue internet cafe. Nimezunguka na nimepata sehemu. Leo alikuwa busy na kununua computer used of course. Kwa sent nilizompa kapata ka 9 hivi. Nimempa na dell yangu mpya so jumla anazo 10. Kazi kubwa ni connection au server gani atumie. Tutakuwa na kikao leo usiku kama nitawahi ama kesho asubuhi ili nimkamilishie ofice yake. Ana imani kuwa ataweza kunilipa fedha zangu maana namkopesha. Nitumie kampuni gani iliyo fast? Kwetu huku ukiwa na internet fast utafanya kazi mpaka uchoke. Masaada wenu na ushauri unashukuriwa kabla.
Eeka Mangi

Uliza watu wenye experince ya business hiyo na uzoefu wao kwa provider mbali mbali. Hivi hivi unaweza kununua huduma nzuri au ya bei nafuu kwenye makaratasi kumbe hailipi kwa bishara yako au haina uhakika.

Usifanye kosa kutegemea TTCL wenyewe wakupe taaarifa sahihi za huduma zao. Au Voda au Benson au wengine.

Na hata sisi wachangiaji kama hatuna uzoefu na huduma ya cafe tunaweza kukupa ushauri mzuri tu lakini usiofaa kwa business na mazingira uliyopo.

Good luck
 
Back
Top Bottom