Msaada Unahitajika: Flash ikiwekwa kwenye CPU nasikia mlio tu lakini haionekani

McCollum

JF-Expert Member
Jan 10, 2023
384
679
Habari kwa wana bodi wa Jf,

Naomba niingie moja kwa moja kwenye mada. Hivi majuzi nilikuwa najaribu kuingiza vitu kwenye flash yangu (8Gb) baada ya kumaliza nilirejea nayo nyumbani.

Kimbembe kilianza nilipoiweka kwenye CPU na kusikia mlio ulioashiria iliingia lakini haikuwa ikionekana, baada ya kujaribu naona bila ila nikijaribu kuiangalia kama hipo kupitia settings naona ipo ila nashindwa kuifungua (haionekani kwenye File Explorer).

Naomba kusaidiwa mawazo ili kupata njia za kuikomboa hii flash ambayo ina mambo ya muhimu (docs).

NB: Nili"copy" vitu kutoka kwenye PC nyingine, wakati nimeichomeka ile flash nili"scan" kabisa
 
Kipindi natafuta elimu kuna “commands” ilikuwa tunaandika na flash inaonekana. Ila kwa sasa sikumbuki chochote maana mtaani situmii tena elimu bali natumua nguvu tu.
 
Kipindi natafuta elimu kuna “commands” ilikuwa tunaandika na flash inaonekana. Ila kwa sasa sikumbuki chochote maana mtaani situmii tena elimu bali natumua nguvu tu.
command ya devmgmt.msc? Nayo imegoma 😂
 
Back
Top Bottom