Msaada tutani....kwa anayejua masuala ya hisa za precission air.

JOYCE PAUL

JF-Expert Member
Jan 8, 2010
1,005
82
Nilinunua hisa za precision air mwaka 2011 walipotangaza kuziuza kwa mara ya kwanza. Ila mpaka leo sijawahi pata barua yoyote wala kuwasikia hawa precission air na sijui naanzia wapi ili nijue kama nina faida au imekula kwangu? Msaada tafadhari kwa anayejua.nawatakia kazi njema
 
Ulinunua kupitia wapi?nenda kamuone stock broker wako..mwambie aziuze akupe pesa...Kabla hujala hasara kubwa
 
Ulichotakiwa kufanya baada ya kununua hisa ni kwenda kwenye Bank or wakala uliponunulia hisa zako, ukawaulize ukiwa na risiti uliyonunulia hisa hizo. Then watakupatia Certificate inayoonesha kiasi cha hisa ulichonunua na thamani yake. Mwaka jana au juzi kama sikosei waliitisha mkutano wa wanahisa wote uliofanyika Ubungo Plaza. Jamani tujaribu kuwa tunasoma na kusikiliza vyombo vya habari. Maana walitoa matangazo mengi saana ya watu kwenda chukua hisa zao na hata kabla ya mkutano wa wanahisa kufanyika.
 
Nenda kwa kuwadi aliyefacilitate wewe kununua hizo hisa utapata certificate yako ya umiliki wa hisa.
 
Ulichotakiwa kufanya baada ya kununua hisa ni kwenda kwenye Bank or wakala uliponunulia hisa zako, ukawaulize ukiwa na risiti uliyonunulia hisa hizo. Then watakupatia Certificate inayoonesha kiasi cha hisa ulichonunua na thamani yake. Mwaka jana au juzi kama sikosei waliitisha mkutano wa wanahisa wote uliofanyika Ubungo Plaza. Jamani tujaribu kuwa tunasoma na kusikiliza vyombo vya habari. Maana walitoa matangazo mengi saana ya watu kwenda chukua hisa zao na hata kabla ya mkutano wa wanahisa kufanyika.

nilikuwa sipo nchini kaka....kwa hiyo nikienda kwa wakala anaweza kunipa hesabu za hisa kama imekula kwangu au lah?
 
Habari JF members
Kwa anayejua nini kinachoendelea kuhusu hisa za kampuni ya ndege ya PRECISION AIR tafadhali anisaidie kunifahamisha....maana toka niliponunua hizi hisa zaidi ya miaka sita(6) iliyopita hakuna gawio....mikutano yenyewe ya wanahisa inafanyika kimya kimya....bei ya hisa zao nimeona imeshuka chini ya bei niliyonunulia badala ya kupanda.....basi naona kama vipi kampuni ifilisiwe turudishiwe pesa zetu tuu.
 
Back
Top Bottom