Msaada: Tatizo la kutosikia vizuri

kibenten

JF-Expert Member
Mar 12, 2018
499
507
Habarini ndugu zangu.

nna mchumba wangu anatatizo la kutosikia vizuri,hali hii imemtokea tu ivi karibuni zamani hakuwa na tatizo hili hata kidogo,

shida ilianza pale alipoenda field pale idara ya maji mwanza, kwa maelezo yake alikuwa kwenye kitengo cha kutibu maji,sasa humo kuna mashine zinaunguruma sana na walikuwa hawapewi headphones (labda walidharauliwa sababu ni wanafunzi wako tu field).

sasa toka aondoke masikio yake hayasikii vizuri hadi uongee kwa sauti, kaenda hospital kaambiwa ngoma za masikio zimeingia ndani kapewa dawa nyingi kinoma kameza zote lakini hali bado.

nmempeleka kwa waganga wa kienyeji kaambiwa eti kuna mwenzie kamroga asifaulu chuo kampa madawa kanywa hadi kachoka,chale za kutosha, n.k.

Ana miezi sita saiv tatzo bado.

Ushauri na msaada anayejua zaid juu ya hili tatizo anisaidie.
 
Pole,
Sauti kali zaidi ya uwezo wa kuhimili wa masikio, kwa umbuali usio sahii na muda mrefu vyaweza kuwa ni sababu ya msingi.

Mpeleke kwa daktari bingwa wa masikio ili kuweza kutanabaisha tatizo la msingi na tiba yake.
 
asante mkuu
 
Aliyewahi kupata tatizo la usikivu hafifu na akapona alete mrejesho hapa, nitatoa zawadi ya elfu 50.

Kwa leo nihitimishe tu kwakusema nchi zetu nyingi za kiafrika bado hatujaweza kupata matibabu sahihi ya masikio.
 
Ni maelezo ya kuvunja moyo, na kama vile unahitimisha hakuna kinachoweza saidika, lakini tujifunze kuwa:

1: Kufahamu tatizo ni nini, ni sehemu ya tiba hivyo bado ni vyema kufika hospitali. Kama angekuwa anajua sababu za kisayansi ingemsaidia kutokwenda kuchanja chale.

2: Kabla ya hitimisho pia ni vyema kujua kama hii ni mechanical au neurological issue na kwa kiasi gani.

3: Nini afanye na nini asifanye kwa hali aliyonayo.

4: Anahitaji support gani kwenye maisha au hatahitaji?
 
Hata nje ni tatizo kubwa sana ni nimepata miaka 6 sasa tangu 2016 kiutani tani sijapona mpaka leo

Natumia ishara somtime nasikia ila sana sna kwenye ishu zangu natumia vimemo natembea navyo mtu ananiandikia ndo life service nilishatupa zilinishinda
 
Habarini ndugu zangu.

nna mchumba wangu anatatizo la kutosikia vizuri,hali hii imemtokea tu ivi karibuni zamani hakuwa na tatizo hili hata kidogo,

shida ilianza pale alipoenda field pale idara ya maji mwanza, kwa maelezo yake alikuwa kwenye kitengo cha kutibu maji,sasa humo kuna mashine zinaunguruma sana na walikuwa hawapewi headphones (labda walidharauliwa sababu ni wanafunzi wako tu field).

sasa toka aondoke masikio yake hayasikii vizuri hadi uongee kwa sauti, kaenda hospital kaambiwa ngoma za masikio zimeingia ndani kapewa dawa nyingi kinoma kameza zote lakini hali bado.

nmempeleka kwa waganga wa kienyeji kaambiwa eti kuna mwenzie kamroga asifaulu chuo kampa madawa kanywa hadi kachoka,chale za kutosha, n.k.

Ana miezi sita saiv tatzo bado.

Ushauri na msaada anayejua zaid juu ya hili tatizo anisaidie.
Mwambie anitafute mimi nipate kumtibia maradhi yake na atapona kabisa.
 
Pole yake sana...

Hata pale IPTL usipovaa za kuzuia sauti masikioni unatoka kiziwi...
 
Hata nje ni tatizo kubwa sana ni nimepata miaka 6 sasa tangu 2016 kiutani tani sijapona mpaka leo

Natumia ishara somtime nasikia ila sana sna kwenye ishu zangu natumia vimemo natembea navyo mtu ananiandikia ndo life service nilishatupa zilinishinda
ulilipataje mkuu
 
Ni maelezo ya kuvunja moyo, na kama vile unahitimisha hakuna kinachoweza saidika, lakini tujifunze kuwa:

1: Kufahamu tatizo ni nini, ni sehemu ya tiba hivyo bado ni vyema kufika hospitali. Kama angekuwa anajua sababu za kisayansi ingemsaidia kutokwenda kuchanja chale.

2: Kabla ya hitimisho pia ni vyema kujua kama hii ni mechanical au neurological issue na kwa kiasi gani.

3: Nini afanye na nini asifanye kwa hali aliyonayo.

4: Anahitaji support gani kwenye maisha au hatahitaji?
Unasema ni maelezo ya kuvunja moyo how? Siku zote ukweli unauma, nimeandika hayo kwakuwa mimi mwenyewe ninatatizo hilo 12 years now
 
Tatizo lako si la mwingine/matatizo hayafananishwi kwa kusikia tu au kuona tu na hayalinganisha.

Kwanza ijulikane tatizo la msingi, ndio tunaenda kwenye maelezo yako, kuwa hili haliwezekani au nini chaweza fanyika kulingana na nature ya tatizo.

Huwezi kusema mgonjwa wa ugonjwa huu huwa haponi akifikia hali hii bila kujua nini kinaendelea kama disease process.
 
Tatizo lako si la mwingine/matatizo hayafanani na hayalingani.

Kwanza ijulikane tatizo la msingi, ndio tunaenda kwenye maelezo yako, kuwa hili haliwezekani au nini chaweza fanyika kulingana na nature ya tatizo.

Huwezi kusema mgonjwa wa ugonjwa huu huwa haponi akifikia hali hii bila kujua nini kinaendelea.
Inshort, hebu utuambie ni nani amewahi kupona tatizo la kutosikia na ni wapi alipata hayo matibabu,

Ndio najua kuna aina nyingi za kutosikia vizuri lakini amini nakuambia hakuna aina hata moja inayotibika bongo, utapewa mavidonge debe moja ukimaliza wanakuambia sasa hapo inabidi utumie kwanza hearing device
 
Aliyewahi kupata tatizo la usikivu hafifu na akapona alete mrejesho hapa, nitatoa zawadi ya elfu 50.

Kwa leo nihitimishe tu kwakusema nchi zetu nyingi za kiafrika bado hatujaweza kupata matibabu sahihi ya masikio.
Daah!.. Mpe pole sana huyo dada.. Mimi nimehangaika kutibu masikio kwa miaka miwili mfululizo hapo muhimbili.. Nashukuru Mungu nipo sawa sasa.. Kiufupi ukiziwi unasababishwa na sababu tofauti kwa kila mtu Kama kuzidisha dozi ya dawa mfano quinine name nyinginezo. Lakini pia kukaa sehemu yenye makelele kwa muda mrefu na hivyo kusababisha masikio yashindwe kuhimili kama alivyosema mdau hapo juice.. Huyu mgongwa aende mhimbili (isiwe sehemu nyigine) kwa kuwa ni madaktari wachache wanaoweza kuhandle issue ya masikio.. Hapo atakutana na daktari bingwa atampima kwa vifaa maalum ili kujua level ya kutosikia kwake.. Then atapewa dawa ambazo atatumia kwa muda mrefu (Mimi nilitumia miaka miwili) ambapo unamrza dawa kila siku kwa miezi mitatu then anasitisha kwa miezi mitatu, ikitimia miezi sita (baada ya mapumziko ya kutotumia dawa kwa miezi mitatu) atarudi tena kwa daktari wake na kupimwa usikivu tena na kuandikiwa dawa nyingine kwa miezi mitatu au zaidi. Kwa hiyo utaratibu Unakuwa ni huo mpaka atakapokaa sawa hata Kama itafika miaka minne..
NB: kadri atakavyokaa muda mrefu bila kupata tiba ya kueleweka ndivyo na uwezekano wa kupona unavyozidi kupungua
ZINGATIA: Sio lazima kila mgonjwa wa masikio atibiwe kwa dizaini niliyoeleza hapa. Inategemea tatizo lake ni kubwa kiasi gani na utaalamu wa daktari.
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Inshort, hebu utuambie ni nani amewahi kupona tatizo la kutosikia na ni wapi alipata hayo matibabu,

Ndio najua kuna aina nyingi za kutosikia vizuri lakini amini nakuambia hakuna aina hata moja inayotibika bongo, utapewa mavidonge debe moja ukimaliza wanakuambia sasa hapo inabidi utumie kwanza hearing device

20220129_141311.png

Unafikiri hii ni kazi bure.
Don't say never in Medicine or science. Pia bado kuna nafasi ya supernatural power.
Tuweke akiba ya maneno.
 
Aise mimi mpaka leo sijapona,nmetibiwa sana tu

Ni kweli, lakini naomba tuelewe kwamba tiba ya mgonjwa yeyote:

1: Ni kukutana na mhudumu wa tatizo husika.

2: Mhudumu wa tatizo husika, mwenye uelewa wa tatizo husika.

3: Mhudumu wa tatizo husika, mwenye uelewa na shida husika na vitendea kazi.

4: Mhudumu wa tatizo husika, mwenye uelewa husika, mwenye vitendea kazi na teknolojia husika.

5: Mhudumu wa tatizo husika, mwenye uelewa wa tatizo, mwenye vifaa husika, mwenye teknolojia husika, yuko motivated na hofu ya muumba.

NB: Hospitali siyo jengo wala jina la hospitali bali hayo hapo juu (mtu uliyekutana naye na alivyowezeshwa).

Watu wengi tunawapoteza au kubaki walemavu kwa kukosa mambo hayo hapo juu.
 
Back
Top Bottom