Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

faokipe

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,017
1,172
Wazee nakuja kwenu nikiomba ushauri,

Kama kichwa cha habari kinavyosema japo mimi sio mtaalamu sana wa kuandika nitajitahidi kuandika machache na ya muhimu, mwaka 2018 nikiwa kwenye safari zangu za kibiashara nilikutana na mwanamke mmoja tukiwa tumekaa siti moja kwenye bus tulilokua tunasafiria pamoja!!

Tulipofika kwenye kizuizi sehemu flan gari ikasimamishwa kwa ukaguzi, kumbe yule mwanamke alikua na mzigo wa magamu(magendo) na akatelemshwa hapo beria.

By then tulikua tushapeana namba za simu na nikataka kujua kulikoni ndipo aliponisimulia mkasa wake na akaniomba nifikishe taarifa kwa ndugu ambaye alinipa namba yake na maelekezo yote!!!

Hata nilipomtafuta yule bwana hakua tayari kuonyesha ushirikiano na yule mdada akawa Hana namna ila kuomba msaada wangu Kama naweza kumsaidia, baada ya michakato yote kufanyika ikawa inahitajika laki 5 ambayo alikua amepungukiwa ili amalize tatizo lake.

Mimi nkaamua kumsaidia kiroho Safi na akatoka ndani , mwanzonii mwa 2020 nkapata kesi ya uhujumu uchumi iliyoniweka gerezani mwaka mmoja na miezi Saba, yule dada nlimpa taarifa siku nakamatwa(alishakua rafiki yangu lakini sio kimapenzi) katika mwanzo wa kesi yangu Hadi natoka gerezani nlikua nae bega kwa bega na hakuna siku hata moja alikosa Kuja kunisalimia nkiwa gerezani (NB gerezani wanasalimiwa siku za wikend tu)

Mungu akasaidia kesi ikaisha na nkatoka, yule dada akanikaribisha nyumbani kwake na katika muda huo wote nlikua sijawahi kufika nyumbani kwake!! Nkakuta anaishi mwenyewe na akaniambia Ana miaka 2 hayuko kwenye mahusiano na pale anapoishi Ni nyumbani
kwake hajapanga

Basi nkatumia nafasi Ile kumuomba awe mwenzangu na akakubali !! Tumekaa kwa upendo na furaha nkiwa naenda kwake kila napohitaji hata Kama Ni usiku wa manane namkuta Yuko peke yake!!

Lakini alishaniambia huko nyuma alikua kwenye mahusiano na mtu japo waliachana sababu ya changamoto za maisha ya hapa na pale Basi kidume nkashika usukani

Yule X wake anasema waliishi pamoja miaka 10 lakini hawakua kwenye ndoa , waliishikimada tu, na walikua wameachana miaka imepita 2 Sasa Hadi mm nakutana nae kimapenzi

Siku moja yule X akapiga simu , akamwambia nasikia una mwanaume hapo nyumbani, Sasa Leo nakunywa KVANT nakuja kukufanyia fujo hapo kwako!! Nkamwambia yule mwanamke huyu X wako Kuna kitu anakudai hapa au alikusaidia kujenga hii nyumba?? akaniambia hajawahi hata kuninunulia glass hapa ndani, vitu vyote Ni jasho langu, Basi nkamwambia Kama Ni hivyo hawezi Kuja Ni mikwara tu!!

Ilipofika saa 5 usiku yule bwana akaja, kumbe alimaanisha, akafanya fujo anapiga madirisha na milango ikawa fujo kubwa wakati huo sisi tuko ndani tumefunga mlango

Asubuhi nkamtaka akaripot police akasema hawezi kumuweka ndani maana Kuna mazuri alimfamyia wakiwa pamoja Ila atamuonya asirudie! Jioni yake akanipigia simu akaniambia nimepata ushauri kwa watu wazima wamesema hapa kwangu nisilete mwanaume, kwa hiyo kuanzia leo usije hapa labda Kama Ni kukutana tukutane juu kwa juu!!

Nkasema sawa sitakuja Wala usiwe na Shaka kuhusu Hilo!!! Nkamuuliza au ndo unamrudisha x wako akasema yule siwezi kurudiana nae maana aliyonifanyia Ni makubwa!! Ntakua na wewe tu Ila nyumbani ndio usije maana namuogopa akisikia Tena uko hapa atakuja kunifamyia kitendo kibaya maana namfahamu Ni mkorofi.

Basi mm nkaamua kukaa kimya Ila Mara kwa mara akawa ananichokonoa kwa msg na simu akitaka tuonane, na mm nkajaa maana niwe mkweli nlijikuta nampenda Sana huyu mwanamke!! Juzi nkampigia simu hakupokea na sio kawaida yake , meseji hajibu nkasema huyu labda atakua na mwanaume ndani !

Nkaenda kwake kufika dirishani nkakuta anaongea na Yule x wake kwa simu ananisengenya na kuniongelea vibaya!! Nkamwambia fungua mlango na kweli akafungua tukiwa ndani nkamuhoji Kama anataka kuendelea na mm au anarudi kwa x wake akasema ananitaka Mimi!!

Basi ukatokea ugomvi Kati yangu na yeye na asubuhi akaita watu wazima tukasuluhisha , jioni hii Nimempigia simu kapokea yule x wake Ila kaongea kistaraabu tukamaliza , baadae nlipopiga Tena akapokea mwanamke akasema bwana yangu ameenda kazini ,namsubiria aje tulale Mimi nlikua na wewe sababu ya shida tu!

Nikihesabu garama na muda ambao nimeuwekeza kwake afu Leo anakuja kunilipa jeuri nakosa Raha kabisa hapa najiuliza nimfamye Nini huyu mwanamke?? Na nitoke vipi kwenye hii Hali niliyonayo maana roho Inaumia Sana , nahisi nlikutana nae naweza kufanya tukio baya maana amenifanyia usaliti mkubwa Sana.

Nawasilisha wakuu naombeni ushauri wenu
 
Wazee nakuja kwenu nkiomba ushauri, Kama kichwa Cha habari kinavyosema japo mm sio mtaalamu sana wa kuandika ntajitahidi kuandika machache na ya muhimu, mwaka 2018 nkiwa kwenye safari zangu za kibiashara nlikutana na mwanamke mmoja tukiwa tumekaa siti moja kwenye bus tulilokua tunasafiria pamoja, !! Tulipofika kwenye kizuizi sehem flan gari ikasimamishwa kwa ukaguzi , kumbe yule mwanamke alikua na mzigo wa magamu(magendo) na akatelemshwa hapo beria
By then tulikua tushapeana namba za simu na nkataka kujua kulikoni ndipo aliponisimulia mkasa wake na akaniomba nifikishe taarifa kwa ndugu ambaye alinipa namba yake na maelekezo yote!!!
Hata nlipomtafuta yule bwana hakua tayari kuonyesha ushirikiano na yule mdada akawa Hana namna ila kuomba msaada wangu Kama naweza kumsaidia, baada ya michakato yote kufanyika ikawa inahitajika laki 5 ambayo alikua amepungukiwa ili amalize tatizo lake
Boss kama huna hela wakati mgumu unatoka wapi?
 
Basi nkatumia nafasi Ile kumuomba awe mwenzangu na akakubali !! Tumekaa kwa upendo na furaha nkiwa naenda kwake kila napohitaji hata Kama Ni usiku wa manane namkuta Yuko peke yake!! Lakini alishaniambia huko nyuma alikua kwenye mahusiano na mtu japo waliachana sababu ya changamoto za maisha ya hapa na pale Basi kidume nkashika usukani
Yule X wake anasema waliishi pamoja miaka 10 lakini hawakua kwenye ndoa , waliishikimada tu, na walikua wameachana miaka imepita 2 Sasa Hadi mm nakutana nae kimapenzi
Mnatoaga wapi ujasiri wa kuthubutu kuingia sembuse kulala nyumba ya mwanamke?
 
Pole sana mkuu.. sehemu ya mwisho umeomba umfanye nini huyo mwanamke .. mimi nakujibu huna chakumfanya na pia amekuwa mkweli kwako mapema so ukweli ni huo na chakufanya ni kuukubali na kuendelea na maisha yako kumpigia pigia ama kumlilia hakukusaidii zaidi ya kumpa bichwa .

NARUDIA : FANYA MAMBO YAKO ACHANA NAE achilia hivyo visasi wapo waliofanya mazuri zaidi yako wakaachwa tena kwe fadhaa kubwa zaidi yako . lakini sasa wana maisha mengine .
POLE SANA KIONGOZI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom