Msaada: Nimetumiwa meseji za matusi

tisa desemba

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
434
114
wadau wa sheria,
naombeni msaada wa hatua za kuchukua endapo mtu atakutumia meseji za matusi makali (sio vitisho) kwenye simu yako... msaada plz jambo hili limekuwa likisumbua sana hapa kijijini kwetu hasa sisi viongozi wa serikali ya kijiji tunaposuluhisha kesi za wanajamii.
 
unamjua aliyekutumia hiyo meseji?

mbona unaleta hoja bila kuielezea vizuri kwa nini unataka msaada au ni hewani imetoka hiyo, na ulifanya nini hadi unatukanwa?
 
kumbe wewe kiongozi wa kijiji? pesa mnazopewa mnazitumia vizuri kwa wananchi wenu au unajifaidisha na familia yako?
 
kumbe wewe kiongozi wa kijiji? pesa mnazopewa mnazitumia vizuri kwa wananchi wenu au unajifaidisha na familia yako?

ndio ni mimi kiongozi wa kijiji (kitongoji) hoja ya fedha za wananchi zinatumikaje sio mda wake sasahivi, hata hivyo wapo wakaguzi wenye wajibu wa kujua zimetumikaje, kwa sasa tujadili issue niliyoiombea MSAADA, ndio ninamfahamu aliyenitukana kwenye hizo meseji, amenitukana baada ya kumzuia kulima shamba lenye mgogoro wa umiliki, ningependa kujua je, sheria inasemaje mtu anapokutukana (sio vitisho) kwenye meseji za simu, ni ushahidi gani unaohitajika zaidi ili kumtia hatiani mtuhumiwa, na je kosa kama hili mtuhumiwa anaweza kupewa adhabu ya ukubwa gani na mahakama.... msaada
 
Kutukana au kudhalilisha utu wa mtu ni kosa la jinai. Kama unaweza kuthibitisha kuwa namba ya simu ni ya huyo unayemfikiria unaenda mahakamani unmfungulia kesi kama kawaida. Siku hizi mitandao ya simu inaweza kuthibitisha mwenye namba fulani kutokana na namba kusajiliwa. Kuhusu ukubwa wa adhabu hilo sijui.
 
We kila siku msaada msaada watakuomba msaada kwenye tuta
watchout
 
ndio ni mimi kiongozi wa kijiji (kitongoji) hoja ya fedha za wananchi zinatumikaje sio mda wake sasahivi, hata hivyo wapo wakaguzi wenye wajibu wa kujua zimetumikaje, kwa sasa tujadili issue niliyoiombea MSAADA, ndio ninamfahamu aliyenitukana kwenye hizo meseji, amenitukana baada ya kumzuia kulima shamba lenye mgogoro wa umiliki, ningependa kujua je, sheria inasemaje mtu anapokutukana (sio vitisho) kwenye meseji za simu, ni ushahidi gani unaohitajika zaidi ili kumtia hatiani mtuhumiwa, na je kosa kama hili mtuhumiwa anaweza kupewa adhabu ya ukubwa gani na mahakama.... msaada

Wewe unamzuia mtu kulima kwa sheria ipi? kama hata sheria ya kutukanwa huijui, unahukumu vipi mtu asilime? si ungewapeleka mahakamani na mwenye kujuwa sheria ndio angehukumu?

Hukumu za matusi ni hizi:

1) Kimila

Inategemea na mila zenu, anaweza chapwa viboko au akalipishwa kuku, mbuzi au ng'ombe, na idadi yao inategemea na matusi.

2) Kidini

Jicho kwa jicho.

3) Mahakama

Usumbufu utakaoupata mpaka ithibitike kuwa amekutukana kweli, unaweza na wewe ukaingia hatia ya kumtukana hakimu na wabunge waliotunga hiyo sheria na serikali iliyoipitisha.

4) Jamii Forums

Unalambwa ban, ikiwa ni mfuasi wa CCM na Muislaam
Ukiwa magwanda na Mkristo, unapeta tu.

5) Mitaani

Unamrudishia ujumbe unaongeza x 2 au 3 au 100, inategemea ulipoupata ulikuwa wapi. Akikukuta upo Karibu ya kanisa au msikiti unamjibu abarikiwe, au amani iwe juu yake. Akikukuta kwenye ulabu unamrudishia x 10000000000
 
We kila siku msaada msaada watakuomba msaada kwenye tuta watchout
kwani kuna kosa kwa member kuomba msaada hapa jamvini, wewe ni jf senior expert member, nilitegemea unapo'reply issue yoyote uta'reply as senior expert member (experienced and knowledgeable), anyway hapa hatupigi siasa, hapa ni professionals chamber kama hujui mambo ya sheria achia wengine watusaidie JF IS OUR FREE SCHOOL... nashukuru kwa walionisaidia na walioni'challenge kwa hoja.
 
Hilo ni kosa la jinai na ni kosa la madai. Unaweza kufungua jalada polisi na namba ya huyo mtu wakaifuatilia halafu akatiwa hatiani na kupelekwa mahakani. Ikithibitika tu mahakama itatoa hukumu kutokana na aina ya kesi uliyofungua kama ni ya jinai watampa adhabu ya jinai ambayo nadhani ni kifungo cha muda fulani au faini au vyote. kama ni madai itategemea umedai nini. Kwani kwenye madai inabidi utamke kiwango unachodai na mahakama itaangalia kama unastahili na huyo mtu amejulikana ataambiwa akulipe vile hakimu ataona inafaa kutokana na mujibu wa sheria. Wala usijali muda kuwa mwingi wa kesi, lakini mwishowe utafanikiwa tu. Kuna mtu alimtukana mpenzi wake wa zamani. Mbona alihukumiwa kufungwa na nahisi alifungwa mwaka yule mama. Iikuwa mkoa wa mbeya kama kumbukumbu zangu ni sahihi.

Na hii imepunguza sana ujinga wa matusi kwenye simu. Kwani wanaweza kufuatilia hizo message hadi wakampata huyo aliyetukana na ni rahisi sana. Pole.
 
Back
Top Bottom