MSAADA: Nimepata kazi Serikalini dereva ila mshahara mdogo kuliko wa Mwendokasi ninakofanya kazi sasa. Nimechanganyikiwa!

Jamaangu alikuwa anafanya Kazi ya mkataba Tanesco alikuwa analipwa kiasi kama hicho na per diem za kuzidi si unajua Tanesco wako busy.

Kaja kupata Kazi Serikalini na salary ni hiyo hiyo uliotaja,alienda kwa madai kwamba job security.

Ila maisha anaganga tofauti na awali,ameishia kumuendesha mke wa Judge 😃😃 na wewe jishauri uamue.
 
Hahahaaa we fikiria ukabidhiwe trekta la kupeleka takataka Pugu mshahara lak3 halaf wenzako wanasukuma VXR V8 ya bosi kila wiki safari anakula nyt za hata ef60 tu lazima kazi iwe chungu
Ni shida kweli na hao wakala wa vipimo sidhani ka wanaajiri mikoani tofauti na walio kwenye miradi. Shida binafsi huwa ni contract fupi na serikali security ya kazi ila unakuwa maskini wallah.
Ila kuendesha trekta si mchezo
 
Nenda kapige kazi ya 300,000/= afu 2023 kama Mwenyezi akikujaalia uzima na afya utakuja kusema ahsante!

Kuna madereva Wana maisha kuliko Maafisa wa TGS F, ambaye huyu ni senior officer katika baadhi ya Kada!

Zingatia: Funga zipu vizuri, vinginevyo utalia na kusaga meno.
 
Nimepata kazi Serikalini dereva mshahara 300,000/ kwa mwezi, wakati Mwendo kasi nachukua 800,000/. Nimechanganyikiwa!

Wanabodi mimi ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na Mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .

Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tuu.

Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yaani nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?

Kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za Serikali tatizo hiyo salary!?

Naomba ushauri.
Sasa wewe huoni kwenye mwendokasi unalipwa vizuri, weee jamaa veeepe? au una uhakika huko serikalini utamwendesha bosi kuu uwe unakula night kama yeye...
 
Security ya ajira ni ujinga ambao unawaponza wengi
Na hiki ndo kinawafanya watumishi wengi wanabaki maskini, hadi anastaafu ni full kumanga manga, mimi nimeshaliona hili na fursa nyingine ya mkopo nitajipanga na vimiradi......potelea pwete.
 
Angalia na benefits pia sio kiasi cha pesa tu mkuu...!
Kuna jamaa zangu yaani marafiki 3 nilikuwa nao job kitengo na ofisi moja.
Wakapata permanent job serikalini wakafurahi, wakaacha huku ambako walikuwa temporary.
Huku temporary walilipwa mara 2 ya wanacholipwa sasa. Kwakweli wanahali ngumu sasa. Check number imewaponza. Huku nako ni government ila wao walikuwa temporary wakati huo. Wansishi kwa kuungaunga Sasa tofauti na walivyokuwa huku.
Binafsi niko government permanent miaka 6 sasa ila nikipata sehemu kuna mkwanja mrefu naacha bila kuomba ushauri hata kwa wife. Ataniona tu nabadili mwelekeo wa ofisi
 
Nani kakwambia serikalini watu wanategemea mishahara??

Tena kwa kazi yq dereva yani unakuwa na per diem za kulala nje ya ndoa kibao ni wewe tu juhudi zako za kusuka majungu uwe unasafiri safiri zaidi ya wenzako
Majungu tena
 
Acheni kumjaza mwenzenu ujinga...uache laki nane ukimbilie laki tatu..ukikatwa hiyo unabaki na laki mbili...ukienda huko utakula msongo wa mawazo to your entire life. Kuhusu ishu ya perdiem wasikudanganye..perdiem inaendana na levo ya mshahara..kwa mshahara huo perdiem yako haitazidi elfu sitini..sasa upate safari ya siku tatu singida utalipwa 240,000. Ukienda huko ulipie guest, msosi, utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.

Ushauri wangu endelea hapo hapo mwendokasi
 
utakutana na watoto wa kiburushi..utakula nao bata..siku ya kurudi mjini utaishia kubeba machungwa na viazi hautabaki na kitu.
Duuh kwani hayo ni lazima kufanya mkuu ukienda safari, just a joke ,
 
Security ya ajira ni ujinga ambao unawaponza wengi
Kweli kabisa, ni kheri ufanye kazi muda mfupi malipo mazuri kuliko muda mrefu( miaka nenda rudi) kwa masirahi kiduchu kisa job security. Kwanza inafikia hatua ubongo una dumaa, haufikirii out the box, kwa ka utafiti kangu kadogo, watu wengi wanaoajiliwa on contract basis (renewal) ufanya ya maana sana tofauti na wale wa kwenye parmanent contract, yaana mtu anastaafu ndo anafikiria kuanza kuwekeza.
 
Nenda serikalini madereva wana fursa kuliko maafisa. Madereva safari ni nyingi mshahara hawagusi.
 
Nimepata kazi Serikalini dereva mshahara 300,000/ kwa mwezi, wakati Mwendo kasi nachukua 800,000/. Nimechanganyikiwa!

Wanabodi mimi ni dereva mzoefu wa daladala kisha nikaajiriwa na Mwendokasi ambapo nakula 800,000/per month .

Wandugu kwa sasa nimevurugwa kwan baada ya interview iliyohusisha watu 760 ambao tuliomba kazi wakala wa vipimo tumepenya na kuajiriwa 57 tuu.

Nimepewa barua Jana napaswa kuripoti kituon kuanzaia 2/7 sasa aisee mbona hii salary Jau!? Yaani nipo kipindi kigumu wandugu hebu wenye uzoefu nisaidieni hill!?

Kiukweli napata wakati mgumu sana barua ninayo ila naipenda ajira za Serikali tatizo hiyo salary!?

Naomba ushauri.

Mzee apo kuna overtime night na mileages utakua tajir itajikuta una M per month
 
Mkuu una uhakika na unachokisema kuwa per diem inaendana na ngazi ya mshahara ndugu...?

Na pia unafahamu kuwa mwenye ajira serikalini anakopesheka mamilioni ya shilingi mkuu...?
Mshahara laki 3 halafu akakope mamilioni ? unajua hata kukopa huko serikalini kuna viwango vyake kutokana na mshahara wako ulivyo? na kama kazi ya mkataba mwaka mmoja mmoja hata kukopa benki asahau ni maumivu tu
 
NENDA HARAKA SERIKALINI, KUNA KITU KINAITWA JOB SECURITY KWA WATUMISH WA SERIKALI, AMBAPO ITAKULINDA HADI KU STAFF KWAKO.
Madereva wa serikal wana mishahara midogo ila wana malulupu mengi unaweza kufikisha hata posho ya Million Moja kwa mwezi...
Hao mwendokasi sio wakuwaamini kesho na kesho kutwa hawapo...

Wizi wa mafuta hiyo posho???
 
Hahahahaaa madereva wanapigana misumari balaa. Ukiwa dereva wa tengo lenye safari sana unaula wakuone unajenga au mnapatana na boss wako lazima ule majungu sana mpaka ukabidhiwe trekta la idara

 
Nani kakwambia serikalini watu wanategemea mishahara??

Tena kwa kazi yq dereva yani unakuwa na per diem za kulala nje ya ndoa kibao ni wewe tu juhudi zako za kusuka majungu uwe unasafiri safiri zaidi ya wenzako😂😂😂😂😂
Ni kweli mkuu, Serikalini bila majungu na unafiki maisha hayaendi!!🤣🤣
 
Dole gumba. Niliachana na mawazo ya kijinga ya security ya kazi zamani sana. Na wala sijawahi kujuta. Kuna sehemu ukifanya kazi miaka 5 unatapa hela yote ambayo ungeisotea serikalini kwa miaka 15-20. Sasa kwa nini ukae huko serikalini kwa miaka 20 wkt kuna nafasi ya kupata hiyo pesa ktk miaka 5? Siyo ujinga huo ni nini? Na wakati natoka serikalini, kaka yangu alitoa machozi akifikiri napotea njia! Yeye yuko serikalini kwenye security miaka nenda rudi lakini amechakaa sana. Hana msaada wowote kwenye familia yetu pamoja kuwa na security ya kazi. Karibu anastaafu sasa.
Msimusikilize uyu ni motivation spika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom