Msaada: NIDA yangu imefungiwa

The_Gooner14

Member
Feb 28, 2024
5
1
Habari. Jana nilikuwa nataka kusajiri line mpya ila imenigomea naambiwa namba ya NIDA imezuiliwa naomba msaada kwa mwenye uzoefu nifanye ili nida yangu ifunguliwe. Na ni mitandao miwili tu niliyosajiria nida yangu VODA NA AIRTEL
 
Nimekwenda sehemu wanaposajiri line, nilitaka kusajiri line ya halotel mhusika baada ya kuanza process mhusika akaniambia namba yangu ya nida imefungiwa hivyo siwezi sajiri line mpya
Angalia namba zilizosajiliwa kwa hiyo NIDA yako Mkuu, usishangae ukakuta namba mpya ujue huyo mhudumu kakuchezea mchezo kasajili line za kuwapa wale jamaa wa tuma kwa namba hii.
 
Huyu ajafungiwa NIDA, ila ameshindwa kutoa maelezo sahihi ya kilichomkuta.

Nimehisi, Namba zake za NiDA zimefikia kiwango cha mwisho cha kusajili line kwa ajili ya matumizi ya simu, inaonekana anasajili line zake vichochoroni au kwa vijana wapita barabarani.

Hivyo, wakatumia NIDA namba zake kusajili watu asio wajue.

Abonyeze *106# kuhakikisha je, namba zilizosajiliwa na NIDA yake ni hizo anazotumia au kuna ambazo hazijui, kama zipo azifute mwwnyewe, walizonazo zitakoma matumizi.

Akishindwa afike kwenye mitandao husika ya hizo namba ambazo hazitambui, wamsaidie kuziondoa.

Asante
 
itakuwa nida imetumika kwa namba 5 hivyo kufanya kushindikana kuongeza namba

tofaut na hapo NIDA inafungiwa vipi
 
Huyu ajafungiwa NIDA, ila ameshindwa kutoa maelezo sahihi ya kilichomkuta.

Nimehisi, Namba zake za NiDA zimefikia kiwango cha mwisho cha kusajili line kwa ajili ya matumizi ya simu, inaonekana anasajili line zake vichochoroni au kwa vijana wapita barabarani.

Hivyo, wakatumia NIDA namba zake kusajili watu asio wajue.

Abonyeze *106# kuhakikisha je, namba zilizosajiliwa na NIDA yake ni hizo anazotumia au kuna ambazo hazijui, kama zipo azifute mwwnyewe, walizonazo zitakoma matumizi.

Akishindwa afike kwenye mitandao husika ya hizo namba ambazo hazitambui, wamsaidie kuziondoa.

Asante
Nida yangu mkuu inaonesha namba mbili tu nilizosajiri na ndio ninazo tumia. Now naenda ofisi zao nijue tatizo
 
Back
Top Bottom