Anayejua jinsi ya kujiunga na Pay Pal

Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
1,956
2,072
Natumaini wote ni wazima wa afya.

Mimi nataka kuagiza gari Japan kuna kampuni inaitwa YOSHIDA AUTO ila nimesikia njia nzuri ili nisitapeliwe initumie Pay Pal.

Sasa naombeni msaada hiyo huduma inatolewa na benki gani hapa Tanzania au nikitaka kujiunga nifanyeje?
 
Usitumie paypal kununua gari, nakushauri ingia tradecarview.com na lipia gari unayoipenda kwa kutumia pay trade, hii ni huduma nzuri na ya uhakika. Inagharimu dola 150 lakini its well woth it.Sina uhakika kama 150 ni flat rate au inavary kulingana na thamani ya gari.

If u insist on using pay pal, fungua www.paypal.com halafu create account, jaza form na soma maelekezo yote utafanikiwa. Hakuna bank yenye huduma ya paypal duniani. Unatakiwa uwe na credit/debit card inayoweza kuprocess electronic transactions kama visa/ mastercard, amex nk.

Kwahiyo utahamisha hela electronically kutoka kwenye ac yako ya bank kwenda kwenye ac yako ya paypal, then hapo ndio utalipia kutoka paypal. Ni kama unahifadhi hela zako kwenye benki nyingine inayofanya kazi online tu.

Wengine wataendelea kama bado hujaelewa au kuridhika na maelezo.
 
Nadhani mkuu kamongo!! umesoma thread flani masaa machache yaliyopita!! pay-pal ni nzuri kwa ununuzi wa vitu vidogo vidogo kama ujuavyo, ebay, amazon na zingine nyingi tu!! mara nyingi provider wa hizi service za online shopping kama vile e-bay huwa wana suggest na kuhimzia watumiaji kujisajili na pay-pal ili kuepuka watu kudhulumiwa na kuanza kutafuta ofisi za e-bay bila mafanikio lakini kwa ununuzi wa magari na nyumba kaka hatufanyi hivi.

Kuna jinsi nyingine za ku secure kitita chako kwa mfano hapo juu Doltyne kakupa upenyo!!
Ngoja waje wataalamu humu wamwage ya kwao... mafundi wengi humu usijali itakuwa tu... good luck
 
Usitumie paypal kununua gari, nakushauri ingia tradecarview.com na lipia gari unayoipenda kwa kutumia pay trade, hii ni huduma nzuri na ya uhakika. Inagharimu dola 150 lakini its well woth it... Sina uhakika kama 150 ni flat rate au inavary kulingana na thamani ya gari.
If u insist on using pay pal, fungua www.paypal.com halafu create account, jaza form na soma maelekezo yote utafanikiwa. Hakuna bank yenye huduma ya paypal duniani. Unatakiwa uwe na credit/debit card inayoweza kuprocess electronic transactions kama visa/ mastercard, amex nk...kwahiyo utahamisha hela electronically kutoka kwenye ac yako ya bank kwenda kwenye ac yako ya paypal, then hapo ndio utalipia kutoka paypal... Ni kama unahifadhi hela zako kwenye benki nyingine inayofanya kazi online tu...
Wengine wataendelea kama bado hujaelewa au kuridhika na maelezo.

hiyo huduma ya PAY TRADE ni salama?
 
nina wasi wasi na paypal coz niliwahi kusikia kuwa paypal iliingia katika matatizo na bank moja ya huko huko JAPAN
 
hiyo huduma ya PAY TRADE ni salama?
Pay trade ni salama kabisa, inasimamiwa na tradecarview.

Ukimlipa muuzaji unawalipa wao kwanza kutoka katika ac yako, ukienda bank na invoice yako, bank wanaelewa nini cha kufanya. Na Trade Car View kupitia Paytrade, wanahakikisha ukidhulumiwa au gari yako isipokufikia kwa sababu zozote zile watakulipa hela zote ulizolipia gari minus their fee (150 usd).

Kumbuka, mawasiliano yako yote na muuzaji gari yafanyike ndani ya mtandao wa tradecarview na sio kungine, msitumiane email direct kwa kupitia huduma kama yahoo mail, hotmail, google mail etc. Create account Trade Car view, na log in kila wakati unataka kuwasiliana na wauzaji ukishaingia kwenye mtandao wao utaelewa zaidi.
 
Pay trade ni salama kabisa, inasimamiwa na tradecarview... Ukimlipa muuzaji unawalipa wao kwanza kutoka katika ac yako, ukienda bank na invoice yako, bank wanaelewa nini cha kufanya. Na Trade Car View kupitia Paytrade, wanahakikisha ukidhulumiwa au gari yako isipokufikia kwa sababu zozote zile watakulipa hela zote ulizolipia gari minus their fee (150 usd).
Kumbuka, mawasiliano yako yote na muuzaji gari yafanyike ndani ya mtandao wa tradecarview na sio kungine, msitumiane email direct kwa kupitia huduma kama yahoo mail, hotmail, google mail etc... Create account Trade Car view, na log in kila wakati unataka kuwasiliana na wauzaji...ukishaingia kwenye mtandao wao utaelewa zaidi.

Thank You Mkuu,Umenielimisha na Mimi pia,JF imesheheni Maarifa!!
Hauwezi kuingia humu halafu utoke kapa!!
Hicho kipengele cha kulipwa fidia mambo yanapokuwa yamekwenda Mrama,nani analipa,TradeCar View au Bank yangu?!!!
 
nina wasi wasi na paypal coz niliwahi kusikia kuwa paypal iliingia katika matatizo na bank moja ya huko huko JAPAN

Fafanua kdogo kaka, waalingia kwenye matatzo gan? Paypal ni mali ya Ebay, na hawa jamaa reputation yao nadhani unaifahamu. Kabla haujajiunga nao na kutumia huduma zao tafadhali SOMA KWA UMAKINI TERMS AND CONDITIONS! watu wengi hatuna utaratibu huo, matokeo yake baadae tunaanza kulalama. Kwa gari Japan pia nisingekushauri kutumia paypal!
 
Thank You Mkuu,Umenielimisha na Mimi pia,JF imesheheni Maarifa!!
Hauwezi kuingia humu halafu utoke kapa!!
Hicho kipengele cha kulipwa fidia mambo yanapokuwa yamekwenda Mrama,nani analipa,TradeCar View au Bank yangu?!!!

Utalipwa na trade car view. Wanachofanya, wanaregister kampuni zote zinazoaminika ili kulipia kwa pay trade. Sasa iwapo kampuni uliyonunua gari imekudhulumu au halijafika, wataifatilia na kuona tatizo lilipo.

Wakishamaliza uchunguzi wanakurudishia hela yako, ndio maana unalipa ile fee ya dola 150, yaani ni kama bima vile. Sasa ninachoona mimi, trade car view watakuwa wameshajiridhisha na kampuni zilizoopt kulipa kwa paytrade na zile fee za wanaolipa dola 150 magari yao yakafika ndio zitakazokulipa wewe lisipofika, halaf wao watawadai wahusika kisheria zaidi.

Bank yako haihusiki na malipo yako, kwani wao ni kama wakala tu wa kusafirisha pesa hapa. Its like m-pesa, hela zikiyeyuka utamdai wakala aliyekutumia au utawadai voda?
 
Fafanua kdogo kaka, waalingia kwenye matatzo gan? Paypal ni mali ya Ebay, na hawa jamaa reputation yao nadhani unaifahamu. Kabla haujajiunga nao na kutumia huduma zao tafadhali SOMA KWA UMAKINI TERMS AND CONDITIONS! watu wengi hatuna utaratibu huo, matokeo yake baadae tunaanza kulalama. Kwa gari Japan pia nisingekushauri kutumia paypal!
In late March 2010, new Japanese banking regulations forced PayPal Japan to suspend the ability of personal account holders registered in Japan from sending or receiving money between individuals and as a result are now subject to PayPal's business fees on all transactions
 
Wakuu,poleni na majukumu,mimi ninahitaji msaada wenu namna ya kufungua akaunti ya PAY PAL .
kazi njema.
 
Wakuu,poleni na majukumu,mimi ninahitaji msaada wenu namna ya kufungua akaunti ya PAY PAL .
kazi njema.

Ni rahisi mno, fungua paypal website www.paypal.com
Sign up new account, inahitaji uwe na email address yoyote ambayo unaitumia tayari kwa sasa. Jaza form kwa viruzi

Ni vizuri tu ukafahamu ili kusajilia email addreaa yako kuwa paypal account ni lazima uwe na credit card kama visa (sio ya crdb), au mastercard. Iwe yako au ya mtu alikukuruhusu kuitumia. This means full access to that account
 
Mkuu kwanini credit card ya CRDB haifai?
 
nenda crdb waambie unataka ku-link card yako na paypal. Wataiwezesha bureee. Kisha kasajili paypal. Kumbuka kutumia password tofauti na nyingine kwa usalama.
 
Mkuu kwanini credit card ya CRDB haifai?
Local banks hapa kwetu wanatoa visa electron ambazo ni kwa ajili ya ATM services pekee

Paypal hawa support card za aina hii kuwa linked kwenye paypal account cause hawataweza kutoa pesa toka kwenye hiyo account since its not an online account

Ila uanaweza wasiliana na bank yako kuona kama wanaweza enable local account ifanye kazi online, niliomba hiyo crdb last year hawakuweza but mambo yanabadilika kila siku, sina hakika kwa sasa
 
VISA electron kwasasa imeshapitwa na wakati, na crdb hawatengenezi tena kadi aina hiyo. VISA CARD NA MASTER CARD wanazotoa crdb zina facilities zote zinazoweza kukupa fursa ya kufanya manunuzi online. Unachotakiwa kufanya ni kwenda tawi lolote la crdb uwaombe unataka hiyo huduma, watakupa utaratibu mzima unaotakiwa. Hawajafanya hii service iwe enabled automatically once unapotengenezewa kadi, kwa sababu ya usalama na ndio maana anayehitaji anatakiwa aombe kwa kuwaona matawini kwao au kwa njia nyingine ya mawasiliano kama wanayo.

Nimetoa hayo maelezo, kwakua mimi ni mteja wa crdb, na nina visa card ambayo niliomba wai-activate niweze kufanya online purchases na waliniwezesha bila zengwe na sasa nina karibu mwaka 1, nafanya transactions zangu online bila tatizo lolote.
 
Back
Top Bottom