Msaada na ushauri : Nashindwa kurudi kwangu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Wandugu, jamaa na rafiki zangu wanyonge.. Nimekuja kwenu rasmi kwa ushauri na msaada.. Nimekwama na niko njiapanda. Msaada wako kimawazo na ushauri ni muhimu sana kipindi hiki kigumu nilichonacho

Mimi ni Mwenyekiti na Mkuu wa Kijiji chetu. Naomba nisikitaje jina kwa sasa. Kwa sababu maalum mbalimbali

Iko hivi mwezi uliopita hapo kijijini kwetu kulitokea tatizo kidogo.. In fact hilo tatizo limetokea huko vijiji vya mbali mpaka kufika kwetu. Basi mimi nikajiongeza. Jioni moja nikamuita kwa siri sangoma wetu mkuu hapo kijijini kwetu.. Tukakaa nje penye giza pembeni ya kilabu chetu cha ugimbi. Nikamnunulia KIPIMO kimoja na mimi nikaagiza KIPIMO

Tukanywa tukafurahi. Mimi nina kautaalam kidogo na vipimo hivyo sangoma alifurahi sana mpaka nikamuongeza na kingine (pengine hapa ndio niliharibu) kwakuwa katika jambo nililomuitia akanishauri kwa kipindi hiki nikimbie maramoja kijijini kuwasalimia wazee na nikirudi lile tatizo litakuwa limekwisha kwakuwa linapita tu tena ni la muda mfupi

Nimeapa kutoamini tena ushauri wa kilabuni.. Maana sasa napata tabu sana... Ubao wa matangazo kijijini kwetu hauishi kuandika vijembe juu yangu.. Naambiwa eti nimekimbia kaya na kwenda kujificha kwetu.. Eti kwamba mkubwa wote mimi bado muoga halafu napenda kudeka sana

Natamani sana kurudi kwangu.. Tena sana lakini sijui naanzia wapi... Hapa nilipo ni usiku mwingi lakini sina usingizi wala amani ni mawazo tele kichwani... Nitarudije kwangu? Naona wana kijiji wanachonga sana juu yangu

Uso umeumbwa na soni kama sio haya.. Lakini hilo sio tatizo.. Tatizo langu kubwa ni hofu je kule kwangu wakati nikiwa sipo hawajanitegea mbigili kweli? Unajua wabaya wapo popote?
Nishauri kwa hekima
Nishauri kwa weledi
Au nishauri vyovyote
Nahitaji msaada wako kimawazo nimechoka kukaa kijijini nataka nirudi kwangu
Kuna bundi analia hapo nje sijui anataka nini tena huyu.. Sijui katumwa?

Jr
 
Wewe rudi tu maana sisi wananchi tulikuchagua ututumikie na ndo maana tulikupa hifadhi kwenye nyumba za serikali lengo tukupate kwa muda muafaka, hakuna chochote ulichotegewa zaidi tunazid kuwa na wasiwasi tu kwa nini unazid kuwa na hofu kila kukicha kwenye kijiji chako mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe rudi tu maana sisi wananchi tulikuchagua ututumikie na ndo maana tulikupa hifadhi kwenye nyumba za serikali lengo tukupate kwa muda muafaka, hakuna chochote ulichotegewa zaidi tunazid kuwa na wasiwasi tu kwa nini unazid kuwa na hofu kila kukicha kwenye kijiji chako mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app


Jr
 
Nimechoka kuwa idle
downloadfile-2.jpg


Jr
 
Hahaah Kijijini hakukaliki!? Waambie wakurudishe kwa ungo lakini angalia wasikudondoshee hapa katikati vijiji vya hapo katikati kuna mchawi mmoja kuzidi wote duniani atamtuma Israel afanye yake ndani ya siku tatu

Ni hivi kijijini moto nyumbani moto mwaga manyanga
 
Nishauri wayforwad mkuu.. Kelele zimezidi kijijini

Jr
Mkuu ukisikiliza binadamu hutoweza kuishi kwa amani. Wewe nenda tu fanya kama vile hakuna kilichotokea. Kwa maana kila binadamu ana makandokando yake. Na pia amini kwamba hakuna anayekusaidia wewe kuishi. Na hicho ulichokifanya ni uamuzi wa maisha yako so long as hujamdhuru mtu.
 
Back
Top Bottom