mapipando
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 2,921
- 3,549
Habari wakuu,
Mwanangu anatimiza umri wa miezi minne keshokutwa,siku ya jumamosi usiku alianza kuharisha na kesho yake tukampeleka hospitali akapimwa na kuonekana hana malaria bali kuna dawa alipewa ya kuzuia kuharisha.
Kwa namna moja ama nyingine dawa zimesaidia angalau kupunguza idadi ya kuharisha kwa siku, mfano usiku wa jana hakuharisha kabisa bali kuanzia mchana hadi jioni aliharisha mara tatu tu.
Usiku wa kuamkia leo pia hajaharisha ila asubuhi kaharisha na mwishoni akawa anatoa choo kilichochanganyikana na damu kwa mbali.
Na hapo ikumbukwe kuwa mara ya kwanza alipoanzakuhara alikuwa akitoa choo chenye damu kwa mbali.
Nimeleta tatizo hili kwenu ili nipate kusaidiwa ushauri.
Jambo lingine,je kumbadilishia mtoto maziwa ya Lactogen1 na kumpa ya ngo'mbe ni sawa?
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wakuu.