Msaada:kwa uzembe nimechanganya terminal connection ya betri ya gari

thebusdriverclassc

Senior Member
Jan 16, 2014
146
66
Wakuu..salaam..

Kama kichwa cha habari kinavyo eleza hapo juu,!!baada ya kusafiri takribani week mbili na kuacha nimepaki gari yangu,nimerudi na kukuta battery ipo down kabisa hivyo kunilazimu kuitoa na kwenda kuichajisha kwa wachajishao.

Sasa katika harakati za kuirudisha nikachanganya terminal yaani + nikaweka - na -nikaweka +,ziliruka cheche nyingi hatari!!baada ya hapo nikagundua kosa langu then nikaifix vile inatakiwa...

Sasa issue ni kwamba gari imewaka lkn hakuna taa yoyote inayowaka zaidi ya zile za mbele kubwa...,mean hakuna Mwanga wowote kwenye dash board,parking light,sport light wala inside the car light inayowaka..

Wadau naomba mnijuze shida itakuwa ni fuse au nimeunguza nini nianze kuandaa kibunda kirefu cha fundi waya???

Natanguliza shukrani kwa wote mtaonisaidia katika hili.

Nawasilisha.
 
Sasa issue ni kwamba gari imewaka lkn hakuna taa yoyote inayowaka zaidi ya zile za mbele kubwa...,mean hakuna Mwanga wowote kwenye dash board,parking light,sport light wala inside the car light inayowaka..Wadau naomba mnijuze shida itakuwa ni fuse au nimeunguza nini nianze kuandaa kibunda kirefu cha fundi waya???
Anza na ukaguzi wa fuse, bila shaka Idadi kubwa ya fuse zitakuwa zimeungua.
Fuse sio ghalama kubwa.
 
Mkuu, kama itawezekana usiliendeshe. Ila mtafute fundi wa umeme wa magari, aje afanye ukaguzi hafu akutajie gharama za matengenezo hafu wewe mlipe tu hela ya ukaguzi wakati unajipanga kutengeneza kama gharama ni kubwa.

Ila kama una utundu pia, fanya kama jamaa alivyokuambia. Pia unaweza kujaribu kubadirisha battery au kuzima gari toa battery kwa dakika kadhaa kisha rudisha.

Gari za zamani sana ukifanya hivyo unaweza kuta umeua Altanetor, au ata ECU.

Pia check fuse box zote unaweza kuona zilizoungua zitakua zimebsdirika rangi au zinanuka kuungua ungua.
 
Asante sana mdau kwa ushauri mzuri
 
kwanza ni gari gani hilo, maana km ni 2018 kuna matoleo kibao mpaka 2020
atupe tu mrejesho maana kuna gari za Vvti
 
Back
Top Bottom