Msaada kwa anayefahamu hili

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Habarini wakuu!
Kumekuwa na udanganyifu mwingi kwa wanaoagiza magari toka Japan kwa kuwekewa mwaka ambao gari imetengenezwa kumbe siyo mwaka halisi bali ni mwaka gari iliposajiliwa na likifika huku watu hulazimika kulipa dumping fee ambayo haikutarajiwa.

Kwa mfano kwenye web gari inaandikwa ni ya 2003, lakini ikifika huku TRA wanakuambia hiyo gari imetengenezwa 2002/12 lakini ilisajiliwa 2003/01 sasa hapo unalazimika kulipa dumping fee lakini wengi wanahongwa na kutoa release order.

SWALI: Kama kuna mtu anajua namna ya kucheck mwaka ambao gari imetengenezwa kwa kutumia chassisna number kwenye website naomba atunijuze, hasa kwa kuiweka hiyo website hapa

Natanguliza Shukrani

Kimbweka!!
 
TRA Hapo wanafanya wizi, ujambazi, mchana kweupe!

Yaani hawakupi release order mpaka mgawane ile damping fee nusu kwa nusu na tena kwenye kadi wanakuandikia mwaka uliopo kwenye invoice hii imekuwa deal kubwa kwao watu wanalizwa vibaya sana huko kwenye bandari ya nchi kavu
 
Habarini wakuu!
Kumekuwa na udanganyifu mwingi kwa wanaoagiza magari toka Japan kwa kuwekewa mwaka ambao gari imetengenezwa kumbe siyo mwaka halisi bali ni mwaka gari iliposajiliwa na likifika huku watu hulazimika kulipa dumping fee ambayo haikutarajiwa.

Kwa mfano kwenye web gari inaandikwa ni ya 2003, lakini ikifika huku TRA wanakuambia hiyo gari imetengenezwa 2002/12 lakini ilisajiliwa 2003/01 sasa hapo unalazimika kulipa dumping fee lakini wengi wanahongwa na kutoa release order.

SWALI: Kama kuna mtu anajua namna ya kucheck mwaka ambao gari imetengenezwa kwa kutumia chassisna number kwenye website naomba atunijuze, hasa kwa kuiweka hiyo website hapa

Natanguliza Shukrani

Kimbweka!!

TRA wamekariri,wao wanaangalia mwaka kwenye mikanda ya usalama,kuna wakati mwaka wa kwenye mikanda unatofautiana na mwaka halisi wa gari kutengenezwa,sababu ni ya wazi kabisa,kama mikanda ilitengenezwa mingi kuliko magari yaliyotengenezwa mwaka huo,mikanda inayobaki huwekwa kwenye magari ya mwaka mwingine huku ikiwa na mwaka wa nyuma kidogo kuliko mwaka halisi wa hilo gari, Ubalozi wa Japani umewahi kutoa ufafanuzi huo,lakini kwa vile TRA ipo kuvuka malengo bila kujali kama ni kwa kuwaumiza wanachi hawataki kufuata ukweli huo.
 
Back
Top Bottom