Msaada kupata mafao NSSF baada ya kuachishwa kazi

primierboy

Member
Jan 27, 2019
15
7
Jamani naomba msaada kwa anaeelewa kuhusu mafao ya NSSF.

Mimi nimewahi kuajiriwa kama professional na baada ya mkataba nilifungua madai NSSF nikalipwa kwa mfumo wa 33.3% ya mshahara wangu kwa muda wa miezi 6 then muda ukapita nikiwa napambana na maisha.

Baada ya muda nikapata kazi ambayo si professional niliajiriwa kama security lakini nikawa nawekewa michango yangu NSSF kama kawaida lakini kwa Sasa nimeachishwa kazi ninahitaji kwenda kufungua madai NSSF.

Swali langu hapa ni je, nitalipwa pesa zangu zote zilizopo NSSF kwa mara moja au nitaanza tena kulipwa 33.3% kama walivonifanyiaga malipo zamani?

Natanguliza shukrani.
 
Jamani naomba msaada kwa anaeelewa kuhusu mafao ya NSSF
Mimi nimewahi kuajiriwa kama professional na baada ya mkataba nilifungua madai NSSF nikalipwa kwa mfumo wa 33.3% ya mshahara wangu kwa muda wa miezi 6 then muda ukapita nikiwa napambana na maisha, baada ya muda nikapata kazi ambayo si professional niliajiriwa kama security lakini nikawa nawekewa michango yangu NSSF kama kawaida lakini kwa Sasa nimeachishwa kazi ninahitaji kwenda kufungua madai NSSF,swali langu hapa ni je,nitalipwa pesa zangu zote zilizopo NSSF kwa mara moja au nitaanza tena kulipwa 33.3% kama walivonifanyiaga malipo zamani?
Natanguliza shukrani
Sidhani kama wataweza kukulipa yote kwa pamoja maana kuna watu wamefanya kazi mpaka kufikia umri wa kustaafu na bado wanapewa madai yao kidogo kidogo
 
Jamani naomba msaada kwa anaeelewa kuhusu mafao ya NSSF.

Mimi nimewahi kuajiriwa kama professional na baada ya mkataba nilifungua madai NSSF nikalipwa kwa mfumo wa 33.3% ya mshahara wangu kwa muda wa miezi 6 then muda ukapita nikiwa napambana na maisha.

Baada ya muda nikapata kazi ambayo si professional niliajiriwa kama security lakini nikawa nawekewa michango yangu NSSF kama kawaida lakini kwa Sasa nimeachishwa kazi ninahitaji kwenda kufungua madai NSSF.

Swali langu hapa ni je, nitalipwa pesa zangu zote zilizopo NSSF kwa mara moja au nitaanza tena kulipwa 33.3% kama walivonifanyiaga malipo zamani?

Natanguliza shukrani.
Baada ya miezi sita ungelipwa zilizobaki, hukufatilia.

Lakini kwa kuwa umefanya kazi sio za profesheni naamini utalipwa zote.

Au kaulize NSSF tawi lingine kabisa na usieleze kuwa ni wewe eleza kwamba unataka kufahamu tu.
 
Namimi pia nahitaji hiyo connection mwenye kujua atujuze,,
Maana kuna hela yangu sijui kwanini hawataki kuweka tangu 27/6 mpaka leo naambiwa tu faili lako lipo uhasibu..lakini mpaka leo sijawekewa mpunga
 
Haya mashirika yaangaliwe upya,maana regulations wanazofanya haziwasaidii raia wa nchi hii,kwa watu waliofanya sekta binafsi ni vema wapewe fedha zao wanapozihitaji.

Ukiritimba wa kuwazuia watu na fedha zao wenyewe ni miongoni mwa sababu zinazoondoa baraka za uchumi nchini,kuzorotesha hali za raia wake na kuchochea umasikini.
 
Kabisa kabisa mkuu! Yaani pesa yako unafanya kuisotea sana kuipata.mimi kwa kweli sitaki tena kusikia hizi mifuko ya hifadhi ya jamii
 
Back
Top Bottom