Msaada...Kuna anayepajua nyumbani kwa Loyd Nchunga?

Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,710
291
Kama kuna kitu kimeniuma ni matokeo waliyovuna Yanga katika mechi ya leo dhidi ya Simba,hivi kweli huyu anayeitwa Loyd Nchunga huko alipo anajisikiaje baada ya timu chini ya uongozi wake kutia aibu ambayo mara ya mwisho ilitokea miongo mi'3 na ushehe nyuma(miaka ya 70) siyo siri nina hasira naye kubwa sana kama kuna mtu anapafahamu kwake anielekeze jamani niende angalau nikapige jiwe 1 ya madirisha ya nyumba yake labda hasira yangu itapungua kidogo,hawezi kututia aibu ya namna hii,
 
mimi hadi nimelia yanga na mimi damu damu but leo imenihuzunisha kiasi kwamba sina raha ya kuwa mshabiki tena
 
tizo la wabongo ndo hilo mkifungwa tu,mchawi ni viongozi kufungwa ni kawaida mbona madrid walipigwa tano na barca,acheni ushabiki wa kipoyoyo hivyo,mbona mlipofungwa na azam na kagera sugar hamkusema haya,ushabiki mwingine wa kipoyoyo sana,igeni ushabiki wa kkbari matokeo kama ulaya
 
Mimi_nina_hasira_sana_na_Azam,huyu_Nchunga_naye_anataka_tumtukane_ili_afurahi. YANGA_MBELE_DAIMA_NYUMA_MWIKO
 
Ujinga mtupu, Arsenal ilifungwa 8, ikaja man u ikapigwa 6, tunajua timu nyingine kubwa tu zinafungwa ije kuwa yanga, tena wachezaji wenyewe hawana hata motisha!,
acheni ushabiki wa usiojenga nyie, jenga timu toa vifaa na motisha kisha lalamika kama haitatenda.
 
yuko kwenye bar moja inaitwa simba kapakatwa anapata bia na nyama choma poleni wanayanga ndiyo soka tena tulikuwa tuwatandike wiki pumbavu zenu...soka hamjui kazi mnayoijua ni kupiga marefa....na wole wenu mnijibu na wapiga Ban
 
Mimi_nina_hasira_sana_na_Azam,huyu_Nchunga_naye_anataka_tumtukane_ili_afurahi. YANGA_MBELE_DAIMA_NYUMA_MWIKO

mmechanganyikiwa eti mbele, mbele kwa kufungwa 5...Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
mimi hadi nimelia yanga na mimi damu damu but leo imenihuzunisha kiasi kwamba sina raha ya kuwa mshabiki tena

na bado kagame lazima tuwafunge kama 10 hivi maana najua sasa hivi mtafukuza wachezaji zaidi ya kumi na tano ukizingatia wengi wamemaliza mikataba...
 
Yanga kubalini tu mpira hamuuwezi nyie zenu ngumi jamani, bora mkajiunge na kina Cheka
 
Hah! hah! hah! badala ya kumshukuru nyie mnataka kumpiga? si mnakumbuka kilichotokea mwaka 1994 baada ya Simba kuirarua Yanga 4-1? au mlikuwa hamjazaliwa bado?

Kilichofuata ni wachezaji wengi kumwagwa na Yanga kusajili wachezaji wengi kutoka Yanga B akina Silvatus Ibrahim aka Polisi, Anwar Awadh na wengineo ambao waliwawakilisha vizuri tu.
 
Ujinga mtupu, Arsenal ilifungwa 8, ikaja man u ikapigwa 6, tunajua timu nyingine kubwa tu zinafungwa ije kuwa yanga, tena wachezaji wenyewe hawana hata motisha!,
acheni ushabiki wa usiojenga nyie, jenga timu toa vifaa na motisha kisha lalamika kama haitatenda.

Huo wako (wa kulinganisha Mbingu na ardhi) ndo ujinga,utalinganishaje Soka la Ulaya na Africa tena Tanzania ya TFF ya Tenga,Ulaya team kubwa kufungwa nyingi ni kawaida sana na ndo maana kila mwaka lazima matokeo ya namna hiyo yatokee,kule ukikaa vibaya wakakuotea unapigwa tu goli nyingi haijalishi ni Man U au Arsenal,lkn kwa jinsi soka letu lilivyo(viwango vyetu havipishani sana) siyo rahisi kwa team 1 kati ya team pinzani(mathalani Simba na Yanga) kumfunga mwenzake goli 5 na ndo maana matokeo ya namna hii kwa team hizi 2 yalitokea kwa mara ya mwisho mwaka 1977 kabla mimi pengine hata wewe hatujazaliwa.
Nitakupa mfano mwaka juzi Yanga ilikuwa kwenye form sana(ile Yanga ya kina Ambani na Mwalala) ilikuwa kila team inayokutana nayo inakula kichapo,tukaja kukutana na Simba iliyokuwa dhorfulhali tena ikitoka kuchapwa na Totot bao 4-1,matokeo yake Yanga ilishinda bao 1-0 bao la Mwalala,na haya ndo matokeo yaliyozoeleka pindi team hizi 2 zinapokutana siyo matokeo ya 5 sijui 6 bila,haya jana Yanga kapigwa 5,ili mtu aje apigwe tena goli kama hizo inaweza kupita miaka mingine 35.
Na hilo uliloongea hapo la team kukosa motisha ndo tunalotaka kummezea Nchunga,team haina motisha mishahara hawapewi kwa wakati makosa kibao ya kiutendaji yanayoigharimu team unataka kuniambia nisimtukane huyo ***** aliyesababisha mazingira hayo.embu think big bwana!!
 
Kwani nchunga ndiyo alikuwa anacheza yanga hakuna wachezaji eti mwape,Nsaijigwa..wamechoka bakizeni nurdin,NIYONZIMA,KIIZA....

Kwa kauli yako hii inaonyesha huelewi chochote,nakusamehe!
 
Kama kuna kitu kimeniuma ni matokeo waliyovuna Yanga katika mechi ya leo dhidi ya Simba,hivi kweli huyu anayeitwa Loyd Nchunga huko alipo anajisikiaje baada ya timu chini ya uongozi wake kutia aibu ambayo mara ya mwisho ilitokea miongo mi'3 na ushehe nyuma(miaka ya 70) siyo siri nina hasira naye kubwa sana kama kuna mtu anapafahamu kwake anielekeze jamani niende angalau nikapige jiwe 1 ya madirisha ya nyumba yake labda hasira yangu itapungua kidogo,hawezi kututia aibu ya namna hii,

Nchunga anaishi Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili mtaa wa sita toka barabara kuu iendayo Morogoro. Nyumba yake haina namba. ila getini kwake kuna bendera ya gamba.
 
Jamani huu ni upepo umepita, ukiangalia kumbukumbu vizuri, Ligi kuu ilianza tangu 1965 pamoja na timu nyingine kutwaa ubingwa Pn,Cosmo,Mseto,Mtibwa, ,Tukuyu nk....YANGA TUMECHUKUA MARA 21 NA SIMBA MARA 17....!!
BADO TUKO JUU, TUTULIE NA TUJIPANGE UPYA sio wakati wa kulaumiana. Nchunga na timu yake ya uongozi wajifikirie kama kweli wanaweza kutuondoa tulipo.
Makundi ya Manji na Kifukwe pamoja na Mosha ni budi sasa yafe tuwe na YANGA MOJA. - YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO. MWANACHAMA WA YANGA.
 
Uongozi ukiwa mbovu, lazima matokeo yawe mabaya. Ni mpira wa watani wa jadi ambao kupokezana kombe imekua kitu cha kawaida sana, sio 5-0, hadi kipa akapata nafasi ya kufunga. Francis Kifukwe baada ya hujuma nyingi, wakati wa uchaguzi akasema "mtoto akilia wembe mpe"
 
tizo la wabongo ndo hilo mkifungwa tu,mchawi ni viongozi kufungwa ni kawaida mbona madrid walipigwa tano na barca,acheni ushabiki wa kipoyoyo hivyo,mbona mlipofungwa na azam na kagera sugar hamkusema haya,ushabiki mwingine wa kipoyoyo sana,igeni ushabiki wa kkbari matokeo kama ulaya

Hatuwezi kuiga ushabiki wa kukubali matokeo ambayo kama kila kitu kingekwenda sawa,kila anayehusika angetekeleza wajibu wake yasingepatikana,Yanga na Simba huwa hazifungani goli nyingi namna hii kirejareja hivyo,Madrid alipigwa 5 huku kila kitu kikiwa shwari,mishahara wachezaji wanapata,posho,motisha na zagazaga nyingine kwa stahi za wachezaji zikiwa katika ubora wa hali yajuu, haya wachezaji wa Yanga wana miezi mingapi sijui hawajapata mishahara yao,wakiwa kambini B'moyo kujiandaa na mechi ya Simba ndo nasikia viongozi wakawapelekea Laki 1,1 hivi laki 1 kwa mtu kama Nsajigwa mwenye familia (mke,watoto na ndugu wengine wanaomtegemea) itasaidia nini? kwanini tusifungwe 5, haya nasikia team ilivyokuwa inakwenda Kanda ya ziwa wachezaji walipewa posho ya kuwaachia familia zao Tshs 10,000,shilingi "ELFU KUMI" jamani,kwanini wasifungwe na Toto na Kagera...hivi pesa zinazotolewa na TBL kwa mishahara zinakwenda wapi,pesa wanazopata kwenye mgao wa kila mechi wanayocheza zinatumikaje? vitega uchumi vyote vile,ada za uanachama za kila mwaka(kwa taarifa yako Yanga ndo team inayoongoza kwa kuwa na Wanachama wengi)bado sisi wenye mapenzi mema na team yetu hatuishi kupiga taff hapa na pale,bwana Nchunga na jopo lake wanapeleka kwenye matumizi gani pesa hizo ikiwa wanashindwa hata kumlipa kocha na kusababisha asuse kufundisha team na kukaa jukwaani kama shabiki.
Bwana Nchunga inabidi ajitathmini toka ameingia madarakani ameifanyia nini Yanga siyo anang'ang'ania tu kukaa madarakani wakati team imeshamshinda kitambo,Yanga ilikuwa na viongozi imara sana wenye fedha na waliokuwa tayari kusaidia team kwa mifuko yao binafsi pale inapohitajika,wote wameondoka baada ya kuona Jamaa anaendesha team ki****e,ona sasa alivyotutia aibu...watu wana uchungu sana na matokeo haya usichukulie juujuu ksbb wewe ushabiki haujakuingia kwenye damu,jana watu wamezimia nimeshuhudia mwenyewe kwa macho yangu na wengine walishindwa hata kuendesha magari yao kurudi makwao wakitokea uwanjani, na ni kweli si kila team inapofungwa mchawi ni viongozi kama ulivyosema lkn kwa matokeo ya jana kama wewe unafuatilia hali ya Yanga basi utakubaliana na sisi kuwa tatizo pale ni Viongozi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom