Msaada: Jinsi ya kupata cheti cha kuzaliwa cha mama

fareed uziel

JF-Expert Member
May 27, 2015
625
646
Habari,

Kijana wenu nahitaji msaada wa haraka wa kupata cheti cha kuzaliwa cha mama, mama ukazaliwa 1962 ocean road.

Je, nawezaje kukipata kupitia Rita kwa njia ya haraka? Mwenye msaada anisaidie.
 
Mkuu cha nini?
Lakini hata hivyo nenda hospitali ya Ocean Road kwanza kujua kama kumbukumbu zake zipo!
Lakini ngoja waje wachangiaji wakuelezee!
 
Kama ni sehemu wanakihitaji unaenda na avidavit ya Mahakamani ya Cheti cha Mama unapewa nenda mahakama yeyote uliyo karibu nayo..iwe Uhamiaji,Polisi au popote pale inatambulika..
 
Habari,

Kijana wenu nahitaji msaada wa haraka wa kupata cheti cha kuzaliwa cha mama, mama ukazaliwa 1962 ocean road.

Je, nawezaje kukipata kupitia Rita kwa njia ya haraka? Mwenye msaada anisaidie.
Inatakiwa uwe na viambata viwili kati ya hivi, kadi ya mpiga kura ya unayemuombea cheti, kadi ya kliniki kama ipo, living certificate ya form four au form six, cheti cha ubatizo, barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa mtaa. Ukiwa na viambata viwili kati ya hivyo nilivyovitaja nenda stationery waviscan Kisha uwaambie unataka kuomba cheti cha kuzaliwa kwa njia ya mtandao.
 
Tumia
Habari,

Kijana wenu nahitaji msaada wa haraka wa kupata cheti cha kuzaliwa cha mama, mama ukazaliwa 1962 ocean road.

Je, nawezaje kukipata kupitia Rita kwa njia ya haraka? Mwenye msaada anisaidie.
Tumia Affidavit kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa ila kama ni lazima cheti nenda RITA ukazingumze nao vizuri hakuna kinachoshindikana
 
Back
Top Bottom