MSAADA: Jinsi ya kufuatilia mirathi ya MWANAJESHI aliyefia kazini

Omwami Nshomile

Senior Member
Jan 26, 2015
132
28
Shikamoo wakubwa, hamjambo vijana?


Mimi nilifiwa na kaka yangu mwanajeshi tangu mwaka juzi, alikuaa akifanya kazi JKT Tabora. Baaada ya msiba tulipewa namba ya afsa mmoja wa jeshi hili ndio atatuelekeza jinsi ya kupata mirathi pamoja na pesa ziliko Benki kwenye account ya marehemu.

Sasa yule afsa amegoma kutusaidia kwani tukipiga simu hapokei. Naomba msaada na maelekezo jinsi ya kushughulikia jambo hili.

Natanguliza shukulani zangu.
 
Mmh hapo kuna Afisa huenda katafuna hiyo mirathi kimtindo ndio maana mpira unarushwarushwa. Hapo ni kukomaa kuanzia kituo chake cha kazi mpaka makao makuu.
 
Kaeni kikao cha ukoo wa familia na mteue msimamizi wa Marathi, mkisha mteua anapashwa kwenda mahakamani kufungua shauri la mirathi kuthibitishwa na nyaraka anazopaswa kwenda nazo mahakamani ni Muhtasari wa kikao na cheti cha kifo cha marehemu. Baada ya Mahakama kumthibitisha msimamizi wa mirathi atajaza fomu ambazo zitamtambulisha na atakukuwa na nguvu ya kisheria kushughulika na mali zote alizoacha marehemu ikiwa ni pamoja na kufuatilia stahili zake alizoziacha marehemu kazini, pesa benk, kukusanya na kulipa madeni na kugawa mali hizo kwa warithi halali wa marehemu.
 
Usumbufu huu mara nyingi wanaupata ndugu wa askari wa vyeo /ngazi za chini.Binafsi kuna ndugu yangu alifariki ilisumbua sana kimsingi naona taratibu zao ni za muda mrefu sana
 
Back
Top Bottom