Msaada: Je unaweza kuandika barua ya kutengua kuacha kazi

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,645
Je unaweza kuandika barua ya kutengua kuacha kazi/kujiuzulu kuna rafiki yangu alipata ajira serikalini mwaka huu kwa iyo akaamua kuacha kazi private na kwenda serikalini sasa anasema ajira yake imesimamishwa je anaweza kurudi tena private kwa kuandika barua ya kutengua kuacha kazi ushauri please
 
Mhhh unanikumbusha mambo ya bwana yule.
 
Je unaweza kuandika barua ya kutengua kuacha kazi/kujiuzulu kuna rafiki yangu alipata ajira serikalini mwaka huu kwa iyo akaamua kuacha kazi private na kwenda serikalini sasa anasema ajira yake imesimamishwa je anaweza kurudi tena private kwa kuandika barua ya kutengua kuacha kazi ushauri please
Sheria ya kuacha kazi haina kipengele cha kutengua maamuzi ya awali ya kuacha kwako kazi.

Ila kama wametangaza nafasi tena za kazi unaweza kuomba kama umekidhi vigezo.

Na pia inategemea na ulipewa Maelezo gani na Management wakati unaacha kazi kutokana na umuhimu wako kama huko ulikoenda kumekushinda na wewe may be ni mchapakazi mzuri na wanakuhitaji.
 
Yes unaweza kama umetoa notice ya minimum ya 24 hrs. Then HR akakuita na kuku convince ui withdraw kabla muda wa notice haujaisha.

Kama ni notice ya mwezi mmoja, unai withdraw kabla mwezi haujafika and only if mwajiri ataridhia.

Lipumba hakutoa notice aliandika kuacha kazi na kutokomea zake. Hawezi tena ku withdraw ile barua hata kama haikujibiwa.

Angetoa notice ya kusudio la kuacha uenyekiti huku anaendelea na kazi, then yuko huru ku withdraw kusudio hilo wakati wowote kabla ya vikao kuipitisha.

Msajili Jaji Mutungi amechemsha big time na ataaibika sana.
Pw
 
Naambiwa Msajili wa vyama ni mwanasheria aliye bobea ndo maana kawekwa pale. Sasa ka alimkubali Ibrahim arudi ofisini tena bila hata barua ya kutengua ile ya kwanza, nadhani mwambie rafikiyo aandike barua na asiipost bali aingie nayo ofisini kwake kwa zamani asubuhi kabla ya watu wote. Wamkute ofisini na akiwa yuko busy kubadili vitasa vya mlango na madroo kuwa ameona wengine wakirudishiwa madaraka yao chini ya mtutu.
Reference yake iwe ni ofisi za Buguruni pale.
 
Je unaweza kuandika barua ya kutengua kuacha kazi/kujiuzulu kuna rafiki yangu alipata ajira serikalini mwaka huu kwa iyo akaamua kuacha kazi private na kwenda serikalini sasa anasema ajira yake imesimamishwa je anaweza kurudi tena private kwa kuandika barua ya kutengua kuacha kazi ushauri please
Itawezekana kama wewe ni Lipumba, kama sio, usijisumbue !!!
 
Awapigie simu aombe kuonana na bosi aende kuongea nao labda watakuwa wanamuhitaji bado.

Kama hawamuhitaji basi atajua huko, sio vibaya kujaribu ila nao watakuwa hawamwamini tena, sababu akipata kazi ingine yoyote as ameonyesha pale hapakumfaa ni ataondoka.

Hapo ni je wapo tayari kupitia mahangaiko ya kutafuta mtu kujazia nasmfasi yake tena au kama hawana mtu bado basi aseme apewe contract ya mwezi kwa mwezi hadi wajaze nafasi au labda ndio atataka kukaa bila kuhama.

Pia kuacha kazi ni muhimu kuhakikisga unakoenda ume sign tayari ili wasikugeuke, as unakuwa umewaeleza kuwa unaenda kutoa notice na utaanza baada ya wiki fulani kutokana na wewe unatakiwa kutoa taarifa ya muda gani huko ili uondoke vizuri.
 
Je unaweza kuandika barua ya kutengua kuacha kazi/kujiuzulu kuna rafiki yangu alipata ajira serikalini mwaka huu kwa iyo akaamua kuacha kazi private na kwenda serikalini sasa anasema ajira yake imesimamishwa je anaweza kurudi tena private kwa kuandika barua ya kutengua kuacha kazi ushauri please
Inawezekana tu endapo barua yako iko ndani ya kipindi ulichotoa notice. Na hii ni katika ajira, si nafasi za kuchaguliwa kwa kura. Notice ziko za aina mbili. Ya masaa 24 au siku 28. Yawezekana ukawa umetoa notice ya masaa 24. Lakini yanapopita masaa 20 toka utoe notice kwa muajiri wako na ukaamuwa kutengua, hiyo inaruhusiwa. Au umetoa notice ya siku 28, baada ya siku 27 machale yakakucheza, inaruhusiwa kutengua. Tena si kwa kuandika barua nyingine. Utaratibu ni unaenda kwa ofisa muajiri au bosi wako na kumuomba akurudishie ile barua. Hapo utaendelea kuwa mfanyakazi halali kabisa. Hata kama imebaki masaa machache na ukaamuwa kuchukua barua yako, utaendelea kuwa mfanyakazi halali. Ila ukitimia muda uliotoa notice............wewe si mfanyakazi tena, ni wakutuma maombi upya na utafanyiwa interview kama hawakujui vile. Anyway, ndivyo sheria zinavyoelekeza. Ila tukija kwa issue ya Prof (issue ambayo wengi wanashehereshea huu uzi) sidhani kama kuna mlinganyo wowote na nilichoelezea hapo juu.
Kwahiyo mleta uzi angalia mchanganuo niliotoa hapo juu na uone jamaa yako anatosha wapi. Halafu utapata jibu. Wakatabahu Infopaedia.
 
Karamu mbili zilimshinda fisi... tamaa mbele umauti nyuma... hicho kinaitwa kifo cha mende...
 
Back
Top Bottom